Anaitwa :Angelica Zambrano binti mdogo
wa ki-Ecuado aitwaye Angelica alioneshwa falme za Mbinguni na Kuzimu, na kurudi
kwake YESUKRISTO mara ya pili.
Kwa kipindi cha masaa 23, Alishuhudia YESU
akilia kwa huzuni aonapo umati wa roho zilizopotea milele, ulimwengu uliomkataa
Yeye, kanisa lisilo tayari kabisa kwa ujio Wake, watu wameacha kushuhudia kwa
walipotea mbali na kweli, na anasa za dunia zimeteka hata watoto kwa shetani.
Alishuhudia watu maarufu wakiteswa katika
moto, waimbaji, wanamuziki na hata Papa.
Angelica alioneshwa jinsi ufalme wa Mbinguni ulivyoandaliwa kwa uzuri na
utayari, utukufu usioweza kufikirika, ambapo hakuna uovu.
YESUKRISTO anakuja kwa ajili ya watakatifu tu;
wengi wa wana wa Mungu hawatakuwa tayari
kwa siku ile, na wataachwa nyuma katika ulimwengu utakaogawanyika vipande
vipande.
Maxima (Mama yake Binti): Jina langu ni Maxima Zambrano Mora, tunasali
kanisa la "Casa de Oracion" huku El Empalme. Tulikuwa katika kufunga
kwa siku 15, na kulia kwa Mungu.
Binti yangu Angelica aliungana nasi pia.
Katika kipindi hicho cha siku 15 cha kufunga, niliweza kupata maono zaidi ya
asili, ambayo sijawahi kuona kabla.
Tulikuwa tunaomba na kufunga katika kipindi maalumu cha
kumtafuta Bwana, tuliendelea kuomba na kulia pale nyumbani, tukisubiri Mungu
aseme nasi.
Bwana alitutia matumaini makubwa sana.
Kwaajili ya majaribu yetu tulikaribia kukata tamaa, lakini Bwana alikuwa pamoja
nasi kutusaidia.
Alitupa
neno la Yeremia 33:3 "Niite, nami nitakuitikia, ame nitakuonesha mambo
makubwa, magumu usiyoyajua.” Binti yangu alitia msisitizo sana katika
neno hili kwa Bwana, japokuwa sikujua kwa wakati huo.”
Angelica (Binti Mhusika): “Jina langu ni Angelica Elizabeth Zambrano Mora. Nina umri wa
miaka 18, na ninasoma chuo cha "Colegio José María Velazco Ibarra",
hapa El Cantón, El Empalme, Ecuador.
Kwanza nilimpokea YESUKRISTO nilipokuwa na
umri wa miaka 12, lakini nalijiambia mwenyewe, "Hakuna hata mmoja wa rakifi
zangu aliyeokoka na nikajisikia aibu miongoni mwao", kwa hiyo nilirudi nyuma mbali na MUNGU
na kuishi maisha mabaya.
MUNGU alinivuta nitoke huko siku ya sherehe ya
kutimiza miaka 15, nirejea tena kupatana na Bwana, lakini nia haikutulia sawa
sawa.
Biblia inasema (Yakobo 1:8), "Mtu wa nia mbili husita-sita katika
nia zake zote" na mimi nilikuwa sawa na mtu huyu.
Baba yangu aliwahi kusema "Hutakiwi kuwa hivyo, siyo
vizuri, ni vibaya mwanangu" lakini nalimjibu, "Hivi ndivyo nilivyo, nataka kuwa hivyo,
hakuna mtu wa kuniambia namna nitakiwavyo kuwa, wala chakufanya, wala namna ya
kuvaa, au mwenendo." Naye alijibu, "Mungu atakushughulikia na
atakubadilisha wewe."
Siku ya sherehe ya kutimiza miaka 17,
nilimkaribia Bwana. Tarehe 28 mwezi Aprili nilimwendea Bwana na kumwambia, "Bwana,
nijisikia vibaya sana, najua kuwa mimi ni mwenye dhambi” na nilimweleza
jinsi ninavyojisikia. Nilitubu na kutoa maisha yangu kwa Bwana rasmi.
Nikaomba “Bwana, naomba unibadilishe, ufanye tofauti
ndani mwangu." Nililia kwa moyo wangu wote, huku nikimwomba Bwana
anibadilishe mimi.Muda ulivyozidi kupita, sikuona madiliko yoyote.
Badiliko
pekee nikuwa nilianza kuhudhuria kanisani, kusoma biblia na kuomba. Hayo tu
ndiyo mabadiliko katika maisha yangu. Ilipofika mwezi Agosti, nilikaribishwa
katika mfungo wa siku 15.
Niliamua kushiriki, lakini kabla ya kuanza
nilisema: “Bwana, naomba unishughulikie hapa. Katika kipindi chote cha mfungo,
Bwana alikuwa anasema na karibu kila mtu, kasoro mimi tu! Ilikuwa kama vile
Bwana hajaniona, na hilo liliniumiza sana. Nikaomba, "Bwana, hutanishughulikia
mimi?"
Nikaomba na kulia peke yangu na kusema tena, "Bwana,
je unanipenda? Je upo hapa? Upo nami hapa? Kwanini husemi nami kama unavyosema
na kila mmoja hapa? Unasema mambo mengi kwa wenzangu, hata maneno ya unabii,
lakini siyo kwangu"
Nilimwomba ishara ya kuwa yu nami, na Bwana
akanipa neno la Yeremia 33:3, "Niite, nami nitakuitikia, nami
nitakuonesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua."
Nikasema, “Bwana, je umesema nami?” Kwasababu
nilisikia sauti yake na kupata maono ya maneno yaliyoandikwa katika Yeremia
33:3. Nikasema “Bwana, hiyo ni kwaajili yangu?”
Tulipomaliza kufunga, kulikuwa na majaribu na
vipindi vigumu na mara nyingine nalijisikia kuishiwa nguvu, siwezi tena
kuendelea na Bwana. Lakini alinipa nguvu.
Nilianza kusikia sauti yake na kumjua vema
zaidi. Tukawa marakifi wazuri. Bwana ni rafiki yetu mwema, na Roho Mtakatifu
pia. Niliwahi mwambia, "Bwana, wewe ni rafiki yangu bora.
Nataka kukujua vema," na nilishirikiana naye katika mawazo yangu
yote.
TAARIFA KUWA ANGELICA
AJIANDAE ANATAKIWA KUONYESHWA MBINGUNI NA KUZIMUNI
Nilimwomba kipindi chote cha mwezi Agosti hadi
Novemba, na mtumishi wa Bwana akaja nyumbani kwetu na kusema, "Bwana
akubariki." Nikajibu, "Ameni." Kisha akasema, "Nimekuja
kukuletea ujumbe toka kwa Mungu…...Jiandae, kwasababu Bwana atakuonesha mambo
makubwa, magumu usiyoyajua. Atakuonesha wewe Mbinguni na kuzimu kama ulivyokuwa”
unamwomba neno la Yeremia 33:3." Nikamwuliza, "Ndiyo, lakini
umepataje kujua? Sijamweleza yeyote." Akanijibu, "Mungu unayemtumikia na kumsifu, ndiye nimsifuye, alinieleza kila
kitu."
Mara tukaanza kuomba,Baadhi akina dada toka
kanisani kwetu na wana familia wangu wakaungana nasi kuomba. Lakini mara
tulipoanza kuomba, nilianza kuona Mbingu zikifunguka.
Mara
nikasema “naona mbingu zikifunguka, na malaika wawili wanashuka kuja tulipo, Mtumishi
wa Mungu akasema “waulize kwanini wamekuja hapa”
Walikuwa warefu na wazuri wakupendeza; wana mbawa nzuri.
Walikuwa wakubwa na wenye kung’aa, na
walionekana wakiangaaza, mng’ao kama wa dhahabu. Walivaa sandozi za vito vya
thamani na walivaa mavazi matakatifu.
"Kwanini
mko hapa?" Wakatabasamu na kusema, "Tupo hapa kwasababu tuna
kazi yakufanya….. tupo hapa kwasababu unatakiwa utembelee Mbinguni na
kuzimu na hatutaondoka mpaka yote yatakapo pita." Nikawajibu “safi
sana, lakini mimi natamani kutembelea Mbinguni tu, siyo kuzimu”
Wakatabasamu na kuendelea kuwepo na hawakusema lolote zaidi.
Baada ya kumaliza maombi, niliendelea kuwaona wakiwepo. Pia nilianza kumwona
Roho Mtakatifu; ni rafiki yangu bora; ni Mtakatifu, amejaa pote na yuko kila
mahali wakati wote.
Ninamwona, anaangaza na kung’aa sana, naona
tabasamu lake na mtazamo wake wa upendo! Ni vigumu sana kumwelezea, kwa sababu
ni mzuri zaidi ya malaika. Malaika wana uzuri wao lakini Roho Mtakatifu ni
zaidi sana kwa yote.
Naweza
kuisikia sauti yake, sauti ilijaa upendo na matulizo makuu. Siwezi kuelezea
kabisa sauti yake; kama radi si radi wakati huo huo yakuvutia. Yeye husema “Niko
pamoja nawe”
Kwa hiyo nalijitahidi kuendelea kutembea na
Mungu, japo majaribu yalizidi kutuzingira. Tulikuwa tunapita kipindi kigumu
sana, lakini chenye ushindi waajabu. Mie husema “Bwana, mapenzi yako yatimizwe.”
Niliendelea kuwaona malaika wale hata nikiwa
shule na pia darasani. Nilikuwa mwenye furaha ajabu kwa sababu niliwaona vema.
Mtumishi wa Bwana, aliyetutembelea, aliniambia nijiandae, kwa sababu nitakwenda kuona
Mbingu na kuzimu.
Lakini pia aliniambia kitu kigumu. Alisema “Nitakufa.”
Haikuwa rahisi niliposikia neno hili. "Nitakufa namna gani? mie
mdogo sana",
Nilimuuliza. Akanijibu, “Usihofu juu ya lolote, Kila kitu Mungu afanyacho hakina makosa wala
mawaa, na atakurejesha duniani, ili utoe ushuhuda juu ya Mbinguni na Kuzimu,
kwakuwa hilo ndilo Bwana anataka sote tujue” Nikasema “Amen, lakini nitagongwa
na gari au nitakufaje?”
Mawazo yalinisonga sana, lakini Bwana
akaniambia nisihofu, kila kitu kiko katika uwezo wake. Nikasema, “Ahsante
Bwana” Ilipofika tarehe 6 Novemba, baada ya kurejea nyumbani toka
shule, malaika wale walikuwa nami, hata nilipokuwa namsifu Bwana.
Wao
walikuwa hawaongei nami; bali walidumu kusema, “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Hallelujah," huku wakimpa utukufu, heshima na sifa Baba wa
Mbinguni. Roho Mtakatifu pia alikuwa na malaika wale huku akifurahi.
Watu wengi husema injili/ wokovu ni wa
kuchosha/kukera, lakini huo ni uongo mkubwa toka kwa mwovu ili kuwafanya watu
wasitafute uwepo wa Mungu.
Nami pia niliamini hivyo hapo kwanza, lakini
baada ya kukutana na Bwana na Roho Mtakatifu, najua injili haikeri wala
kuchosha, niburudisho la ajabu hapa duniani! Ninaweza kumwona; kucheza na
kuongea naye Roho Mtakatifu.
Lakini malaika walikuwa hawaongei nami, ila
walikuwa wakimsifu Bwana. Nikimwambia Roho twende nami nakufanya hili na lile
huja na kuwa nami.
Ninaweza kujihisi na kumwona vema. Japokuwa
wengi hawamwoni, yeye yupo! Mahusiano haya yamendelea, hata hakuna sababu ya
kuyasimamisha, hasa baada ya kuonja radha yake na faida za Roho Mtakatifu……
hakuna njia ya kujitenga naye jinsi alivyo mwema na wafaida, hasa nikikumbuka
alikonitoa, jinsi nilivyokuwa, ninamshukuru sana kwa rehema zake na upendo wake
kwa wanadamu na kwangu mimi!.
Tarehe
7, Novemba, nilipokuwa narudi nyumbani, nikasikia sauti ikisema “Jiandae,
kwakuwa leo utakufa,” Nilijua kuwa ni Roho Mtakatifu kwa vile nilimwona
vema. Niliipuuza sauti yake na kusema “Bwana, Sitaki kufa leo!” Lakini
alirudia, “Jiandae, kwakuwa leo utakufa!”
Mara hii sauti ilikuwa ya juu zaidi na mkazo
mkubwa. Nikajibu, “Bwana, najua ni wewe
unayesema nami; nimeuliza ili kupata uhakika tu, mapenzi yako yatendeke.
Nitafanya kila utakalo niambia, najiachia kwako Bwana, japo naogopa, najua upo
nami, nawe ni wa kweli.”
Niliomba, “Bwana, Yule mtumishi wako uliyemtumia
kunipa ujumbe mara ya kwanza, mlete muda huu, nimkute nyumbani, na umpe tena
neno hili aseme nami kuwa leo ndiyo siku yangu ya kufa.”
Sasa mara zote Bwana hujua ya nyuma, yaliyopo
na yajayo. Alijua kuwa nitamwomba neno hili. Kwa hiyo nilipofika nyumbani
nikamkuta mtumishi wa Bwana ameishafika!.
Maxima (Mama ya Binti): Binti
yangu alipofika nyumbani, tulikuwa jikoni. Mara Angelica alipomwona mtumishi wa
Bwana, akasema, “Bwana akubariki.”
Mtumishi wa Mungu akajibu, “Bwana akubariki nawe. Je uko tayari? Kwa
kuwa leo ndiyo siku Bwana atakayo kuchukua, saa kumi jioni.” Angelica
alisimama na kushikwa na mshangao kwamba Bwana amejibu ombi lake na kufanya
vilevile alivyomwomba njiani.
Angelica: Niliposikia hayo
maneno ya mtumishi, nikasema, “Ameni... lakini sitaki kufa, sitakufa!
Hapana, Bwana, naogopa, naogopa sana, ninahofu kubwa!”
Mtumishi wa Bwana akasema, “Tuombe ili hofu ikutoke sasa kwa jina la Bwana.” Nikasema, "Ameni" na tukaomba. Ghafla
nikajisia hofu yote imenitoka na furaha isiyoelezeka ikajaa ndani mwangu,
nakuanza kuwaza kuwa kifo ni kitu chema kuliko vyote nikitamanicho kinifike! .
Nikanza kutabasamu na kicheka wakati huo kila
mmoja aliyepo akinitazama. Wakaniona jinsi nilivyobadilika toka unyonge
na kuwa mwenye furaha. Nilikuwa natabasamu, narukaruka na kuimba.
: Maxima: Binti yangu ghafla akawa
mwenye furaha ndani ya moyo na kuanza kula. Alionja karibia kila kitu
kilichokuwepo, huku akisema, “Kama
sitarudi, sawa nimeshakula na kushiba.”
Angelica: Kila mmoja akaanza kucheka
na kuuliza, “kwanini uko hivyo badala ya
kuwa na huzuni, unafuraha na mwenye raha?” nikawajibu, “Ndiyo ninafuraha: ninakwenda kumwona Bwana, nitakuwa naye, lakini
sijui kama nitarudi. Kwa hiyo nataka kugawa vitu vyangu vyote.”
Wote
wakastaajabu na kuniuliza, “Unataka
kugawa vitu vyako vyote?” macho ya mama yangu yalinitazama kwa mshangao
zaidi!
Maxima: Binti yangu akaanza kugawa
vitu vyake. Aligawa vyote, vyote! Ma-dada wa kanisani walikuwepo, nao pia
aliwapa baadhi ya vitu kwa kila mmoja. Nilipomuuliza nia yake, alisema, “Kama nikirudi, watanirejeshea vyote, lakini
nisiporudi, watabaki navyo.”
Angelica: Niliwaza huzuni aliyokuwa
nayo mama yangu niliposema maneno hayo. Lakini nilijisikia furaha tupu, kwa
hiyo nikaendelea kugawa vitu: nguo, kitanda, simu ya mkononi, kila kitu, lakini
kwa sharti: kama nikirudi, kila kitu kitarejeshwa kwangu. Wote wakaanza kucheka.
Maxima: Binti yangu alikuwa na
msimamo na nia ya dhati, lakini kama mama nilishikwa na huzuni sana. Haikuwa
jambo rahisi. Niliwaza, “Bwana muda huo ukiwadia, itakuwajekuwaje?”
Sikuweza kuelewa.
Na walipoanza kuomba, nilikuwa napanga vitu
ndani ya nyumba. Walisema, “Dada njoo
tuombe.” Lakini niliwajibu, “Nyie
endeleeni, nitajiunga nanyi muda si mrefu. Ngoja nimalizie kazi hii.”
Angelica: Wote walikuwa wananiangalia
mimi tulipokuwa tunaomba. Niliomba, “Bwana,
nataka kufanya mapenzi yako. Wewe si mwanadamu hata useme uwongo au ujute,
najua wewe ni mkweli. Kama nitakuaibisha, basi vema unichukue moja kwa moja;
lakini kama nitayafanya mapenzi, basi unirejeshe tena, lakini nisaidie kusema
ukweli, niandae mimi, nisaidie kuhubiri na kuwaambia watu kutubu.”
Hiyo ndiyo ilikuwa sala yangu fupi sana.
Nilimwambia mtumishi wa Bwana, “Usimwambie
mama yangu maneno niliyomwomba Bwana.” Naye akajibu, “sitamwambia sasa, lakini mara Bwana atakapokutwa, nitamwambia.”
Maxima: Tuliendelea kuomba na
kuungana katika duara. Ilipofika saa 9:30 jioni, Bwana akamwambia mtumishi wake
ampake mafuta binti yangu. Kwa hiyo baadhi yetu tulikwenda chumbani na kumpaka
mafuta. Alitupa dakika mbili tumpake mwili mzima, toka kichwani hadi chini,
kila mahali, mwili mzima. Akawa mwili wote amepakwa mafuta.
KIFO CHAKE ANGELICA
Angelica: Mama yangu na dada mmoja,
Fátima Navarrete, walinipaka mafuta. Kadri walivyokuwa wananipaka, nilijisikia
kama kuna kitu kinanifunika, kama kioo kilinizunguka mimi. Ni vigumu kuelezea,
nilijisikia kama nimezingirwa na ngao fulani, na nashindwa kuelezea nilivyokuwa
najisikia.
Baada ya hapo kila walipojaribu kunigusa
walishindwa! Maxima: Kadri
tulivyokuwa tukimwombea Angelica, nilijaribu kuweka mkono juu yake,
nilishindwa! Alikuwa amezingirwa na kitu. Ilikuwa ajabu, hakuna aliyeweza
kumgusa tena! Uzio huo ulianzia kichwani hadi miguuni, karibia sentimenta 30
(Inchi 12).
Hilo lilinitisha zaidi mimi. Nimewawekea
mikono wengi kabla, katika huduma ya Bwana, lakini jambo kama hili halijawahi
kutokea! Nikasema, “Oh, kuna jambo lazima linatendeka,” na nikaanza kuomba na
kumshukuru Bwana. Ghafla, nikasikia furaha kubwa sana. Huzuni iliyokuwa moyoni
ikanitoka, maumivu yakakoma na sasa nikasikia raha na furaha ajabu! Tuliendelea
kuomba na ilipofika saa 10.00 jioni, binti yangu akaanguka sakafuni.
Angelica: Wakati wa maombi, nilisikia
kuishiwa pumzi; nikashindwa kupumua. Nikasikia maumivu tumboni na moyoni.
Nilijisiki damu ikisimama, na ghafla maumivu makali mwili mzima. Nililoweza
kusema, “Bwana, nipe nguvu, nipe mimi nguvu!” kwasababu nilijisikia
kushindwa kuendelea zaidi.
Sikuwa na nguvu kabisa, zote zilinitoka! Na
nilipoangalia juu mbinguni, katika roho, si kwa macho ya mwilini, niliona
mbingu zikifunguka. Niliwaona malaika, siyo wawili au kumi, bali kwa mamilioni
wakiwa pamoja wamekusanyika. Katikati yao niliona mwanga, mara 10,000 zaidi ya
jua. Na nikasema, “Bwana ni wewe unayekuja!”
Maxima: Alipoanguka chini,
tulijaribu kumsimamisha, lakini hakuweza kusimama mwenyewe. Muda huu tuliweza
kumgusa. Alikuwa akisema, “Omba. Sina nguvu, mama, sina nguvu na
ninasikia maumivu.” Mwanzo alisikia maumivu tumboni, na baadaye moyoni.
Tuliendelea kuomba na kumsihi Bwana. Bwana
alichukua maisha yake!
Niliweka mikono yangu usoni pake, na kioo
mdomoni kuona kama alikuwa anapumua. Hakuwa na pumzi tena, alitulia kimya
kabisa.
Nilimshika, alikuwa angali na joto kama
kawaida. Nilichukua shuka na kumfunika na kwa muda mfupi akaanza kupoa na kuwa
wa baridi sana. Nywele zake zikalala, kama za maiti na akabadilika ubaridi wa
barafu.
Angelica: Yesu alikuwa anashuka chini,
na nikajisikia mwili ukifa. Kadri Yesu na malaika walivyozidi kukaribia,
nikajisikia kuondoka, na sikuwa mimi tena. Sikuwa hai tena, nilikuwa nakufa na
kugugumia maumivu! Wakati mwili wangu ulipoanguka chini, walikuwa tayari
wamefika.
Nyumba yetu ilijaa malaika, na katikati yao
niliona mwanga mkali kuliko wa jua! Ilikuwa vigumu; nilisikia maumivu makali
wakati roho yangu ilipotenganishwa na mwili. Nilikuwa nalia na kupiga kelele,
kadri nilivyoona mwili wangu sakafuni.
Nilimuuliza, “Bwana, nini kinachotokea?
Nini kinachotokea?” Nilijaribu kuugusa mwili wangu na kuurudia tena, lakini
nilipojaribu, ilikuwa kama kushika hewa: sikuweza kuugusa, mkono wangu
ulipitiliza.
Hakuna kati ya waliokuwa wananiombea
aliyenisikia! Na nikapiga kelele, “Bwana, nisaidie mimi!”
Maxima: Mume wangu alifika
tulipokuwa tunaomba, na alimkuta pale. Bwana alinipa nguvu kwa kuwa sikujua la
kufanya. Ilikuwa kama vile yuko mahututi (kwenye coma), lakini nilijua yuko
salama, kwasababu ilikuwa ni kazi ya Bwana.
Kwahiyo nikasema “Bwana, mapenzi yako yafanyike.”
BWANA YESU KRISTO
Angelica: Wakati huo nasikia sauti ya
Bwana, sauti nzuri kama radi lakini ya UPENDO, “Usiogope, Binti, kwa kuwa mimi
ni Yehova, Mungu wako, na nimekuja hapa kukuonesha niliyokuahidi wewe.
Inuka, kwa kuwa mimi ni
Yehova, ninayekushika mkono wako wa kuume na kukuambia, usiogope, nitakusaidia
wewe." Ghafla, nikasimama. Nilikuwa
nimepiga magoti chini, ninauangalia mwili wangu, nikitaka kuurejea bila
mafanikio.
Niliposikia sauti yake, woga ukanitoka, na
sikuwa na hofu tena. Nilipoanza kutembea, malaika wakaanza kufungua njia.
Kulikuwa na mwanga mkali ung’aao, na nilipouangalia nilisikia amani ya ajabu.
ANGELICA AKIKUTANA NA YESUKRISTO.
Kadri nilivyoangalia, nilimwona mwanaume
mzuri, mrefu, aliyevaa vizuri na kuvutia sana kumwangalia, mwenye siha njema.
Mwanga ulitoka kwake. Kulikuwa na mwanga mkali kiasi cha kushindwa kumwangalia
uso wake! Lakini niliweza kuona nywele zake za dhahabu ing’aayo na vazi jeupe
na mshipi kifuani pake.
Ukisomeka,
“MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA.” Nilimwangalia miguuni pake,
alikuwa amevaa sandozi zenye mng’ao wa dhahabu, dhahabu safi. Alikuwa mzuri
sana! Akaninyooshea mkono wake.
Nilipomshika mkono wake, haikuwa kama
nilipojaribu kuugusa mwili wangu, mkono haukupitiliza. Nikauliza, “Nini
kinachotokea?” naye akasema, “Nitakuonesha wewe kuzimu ili ukirudi
uwaambie wanadamu kuwa kuzimu ni halisi; kuwa ni kweli ipo. Na pia utukufu
wangu nitakuonesha wewe, ili uwaambie watu wangu wajiaandae, kwa kuwa utukufu
wangu ni halisi na mimi pia.”
Akasema, "Binti, usiogope” akarudia
kusema tena na mimi nikasema, "Bwana,
nataka tu kwenda Mbinguni, lakini siyo kuzimu, kwasababu nimesikia kunatisha!”
Akasema, “Binti, nitakuwa nawe. Sitakuacha huko na nitakuonesha huko mahali
kwasababu wengi wanajua kuzimu ipo lakini hawaiogopi.
Wanaamini ni mchezo, na kuzimu ni mzaha, na
wengi hawajui lolote juu yake. Ndiyo maana nitakuonesha wewe huko kwa sababu
wanaopotea ni wengi kuliko wanaoingia katika utukufu wangu.”
Aliposema hayo, niliona machozi yakitiririka
kwenye vazi lake. Nikamwuuliza, “Bwana,
kwanini unalia?” Akanijibu, “Binti, kwasababu wengi wanaangamia, na
nitakuonesha hii, ili uende na uwaambie ukweli na wewe usirudie hapo.”
YESUKRISTO AKANIONYESHA KUZIMU
KUZIMU Ghafla, alivyokuwa anaongea, kila kitu
kikaanza kutembea. Ardhi ilitikisika na kupasuka, na nikaona shimo jeusi tii
chini.
Tulikuwa tumesimama kama kwenye mwamba na
malaika wakituzunguka. Nikasema, “Bwana,
sitaki kwenda mahali huko!” akasema, “Binti, usiogope niko pamoja nawe.”
Kwa sekunde chache tukashuka kwenye shimo jeusi.
Nilijaribu kuangalia lakini kulikuwa na kiza
kikuu. Niliona duara kubwa, na kusikia mamilioni ya sauti. Nilipata moto.
Nikajisikia ngozi yangu kuungua.
Nikamuuliza, “Bwana, hiki ni nini? sitaki kwenda mahali huko!” Bwana akasema “hilo
ni lango tu la kwenda kuzimu”.
Kulikuwa kuna harufu mbaya, yakutisha,
isiyovumilika, na nikamsihi Yesu asinipeleke mimi. Naye akajibu, “Binti,
ni muhimu ufike na kujua sehemu hii.”
Nikalia, “Lakini
kwanini, Bwana, kwanini?” naye akasema, “Ili ukawaambie ukweli wanadamu; wanadamu
wanaangamia, wanapotea na wachache sana wanaoingia ufalme wangu.” (Mat.7:14)
Akishasema hivi, hulia sana.
Maneno yake yalinitia nguvu na kunihimiza, kwa
hiyo nikaendelea kutembea.Tulifika mwisho wa tanuru/lango, nilipoangalia chini
niliona umati umefunikwa na miali ya moto.
Bwana akasema “Binti, nakupa hii.” Ilikuwa ni faili kubwa lenye karatasi ambazo
hazijaandikwa chochote. “Binti, chukua na kalamu hii ili uweze kuandika yote
nitakayokuonesha, utakayoyaona na kusikia. Utaandika kila kitu ukionacho na
utaishi nayo.”
Nikasema,
“Bwana, nitafanya, lakini nimeshaanza kuona mengi mno, Bwana. Ninaona roho
zikiteswa, na kuzamishwa kwenye moto.”
Maxima aliehuku DUNIANI: Muda uliendelea
kupita, na binti yangu alikuwa bado kalala pale. “Bwana, nini kinachotokea?”
Machozi yalikuwa yakimtoka kwenye macho, lakini kila nilipomfuta, yalitoka
tena.
Nikaweka kioo mdomoni pake kuona kama
anapumua, hakukuwa na pumzi. Tuliangalia mapigo ya damu, wapi, hakuna kitu!.
Tuliweka mikono tumboni pake, wapi! Hakuna kitu.
Mtumishi wa Bwana akasema, “mahali
alipo sasa, siyo mahali pa kutabasamu bali mahali pa mateso.”
Angelica: Nikamwambia Yesu,
Nitashuhudia kuwa kuzimu ni halisi, kwamba ipo, lakini nitoe hapa sasa!” na
akanijibu, “Binti, hatuja ingia bado mahali penyewe, na sijakuonesha chochote,
tayari unataka nikutoe huku?”
Nikasema “Bwana,
tafadhari nitoe mahali hapa,” tukaendelea kushuka kwenye korongo/shimo
lakutisha! Nikaanza kulia na kupiga yowee, “Bwana, hapana, hapana, hapana,
hapana……… Sitaki kwenda!” naye hujibu, “Unatakiwa kuona haya.”
Niliona mapepo yakutisha, ya kila aina,
makubwa na madogo. Yalikuwa yanakimbia sana, na yameshika vitu mkononi. “Bwana,
kwanini yanakimbia hivyo na yameshika nini?” akanijibu, “Binti, wanakimbia hivyo
kwasababu wajua muda wao karibu kwisha, kwasababu muda wa kuwaharibu/kuwapoteza
wanadamu, hususani watu wangu.
Na walivyoshika mkononi ni mishale ya
kuwaharibu wanadamu, kwasababu kila pepo amepewa jina na kwa kadri ya jina
lake, ana mishale ya kumharibu mtu na kumleta huku kuzimu; malengo yao ni
kumharibu mtu na kumleta kuzimu.”
Na niliendelea kuona mapepo yakikimbia na
kutoka kuelekea duniani na Bwana akaniambia; “Wanakwenda duniani ili kuleta
na kuwatupa wanadamu huku." Alipokuwa akisema hivyo, Bwana hulia,
hulia sana.,Kila alipolia nami nililia pia.
Maxima alie duniani anaeleza: Binti yangu alikuwa amekufa
kwa masaa 23, lakini sikutoa taarifa kwenye mamlaka yoyote. Niliomba, “Bwana, nitasubiri kwa masaa 24. Kama binti
yangu hatarudi ndani ya saa 24, nitampigia simu Daktari.” Lakini, Bwana
alimrejesha kabla ya saa 24 hazijatimia.
Angelica: Bwana akaniambia, “je
uko tayari kuona nitakachokuonesha wewe?” Nikasema, “Ndiyo Bwana,”. Alinipeleka kwenye sero
moja, ambapo nilimwona kijana akiwa matesoni katikati ya miali ya moto.
WANYWAPOMBE, MADAWA YA
KULEVYA NA KUPITA KATIKA NJIA ZISIZOFAA.
Nikajulishwa namba sero yake, japokuwa
sikuweza kujua ile namba, ilionekana kama imeandikwa kinyume hivi. Palikuwa na
nembo kubwa mle ndani, na kijana alikuwa na namba 666 kwenye kipaji cha uso.
Pia alikuwa na aina ya kipande cha chuma
imebandikwa kwenye ngozi yake. Funza walikuwa wanamtafuna, haikuweza kuharibu
kipande kile; wala moto haukuweza kukiunguza. Akapiga kelele, “Bwana, nirehemu mimi. Nitoe mahali hapa.
Nisamehe mimi Bwana!” lakini Yesu alimjibu, “umechelewa, umechelewa sana:
nilikupa fursa lakini hutaka kutubu.”
Nikamuuliza Yesu, “Bwana, kwanini huyu yuko hapa?” mara nikajulishwa. Akiwa duniani,
kijana huyu alijua neno la Mungu, lakini ghafla akajitenga na Bwana
na kuchagua pombe, madawa ya kulevya na kupita katika njia zisizofaa.
Hakutaka kufuata njia ya Bwana. Yesu alimwonya
mara nyingi juu la litakalompata.
Yesu akasema, “Binti, yuko hapa kwasababu kila
anayeyakataa maneno yangu, anaye amhukumuye: lile neno nilisema naye
litamhukumu siku ya mwisho,” (Yohana 12:48) na Yesu akalia tena. Bwana akilia,
nitofauti nasi tuliavyo na zaidi yetu.
Yeye hulia na maumivu makali moyoni na uchungu
usioelezeka. Bwana akasema, "Sikutengeneza kuzimu kwaajili ya
wanadamu,” Nikamuuliza, “Sasa
Bwana kwanini wanadamu wapo huku,” Akanijibu, “Binti, niliiumba kwajili ya
shetani na malaika zake, ambayo ni mapepo;(Mat. 25:41) lakini, kwasababu ya
dhambi na kukosekana kwa toba, wanadamu huishia hapa, na wengi wangamiao kuliko
wanaofika katika utukufu wangu!" Akaendelea kulia na huniumiza sana
nimwonapo akilia.
"Binti, nalitoa maisha kwaajili ya
wanadamu, ili wasiangamie, ili wasiishie hapa [Kuzimu]. Nalitoa maisha yangu
kwa upendo na huruma, ili wanadamu waendee toba na kuingia katika ufalme wa
Mbinguni.” Yesu kwa huzuni huugua kiasi cha kushindwa kustahimili maumivu,
kadri aonavyo watu pale kuzimu.
Kwa kuwa na Yesu, kulinifanya nijisikie
salama. Niliwaza, “kama nikimwacha Bwana aende, ninge-nasa kuzimu pale” Nikamuuliza,
“Yesu, je nina ndugu yangu mahali hapa?”
Akanitazama kwa jinsi nilivyokuwa nalia na akasema, “Binti, niko nawe,”
Kwasababu nilikuwa mwenye hofu sana.
WASIO SAMEHE ,WENYE MALAAUMU,
MAFUNDO NA CHUKI MIOYONI.
Akanipeleke kwenye sero nyingine. Sikuwahi
kuwaza kumwona ndugu yangu kwenye sero ile. Nilimwona mwanamke akiteswa,
alikuwa na funza wakimla uso wake, na mapepo yakimchoma mikuki mwilini.
Naye hupiga kelele, “Hapana, Bwana, nihurumie,
nisamehe mimi, tafadhari, nitoe mahali hapa kwa dakika moja!” (Luka 16:24)
Kuzimu, watu huteswa na kumbukumbu za waliyoyafanya duniani.
Mapepo hudhihaki watu na kuwaambia, “abudu na kusifu kwasababu huu ndiyo ufalme
wenu!” na watu hupiga kelele 11 wakikumbuka kuwa walimjua Mungu, kwasababu
walijua neno.
Walimjua Bwana waliteswa mara dufu ya wengine.
Bwana akasema, “Hakuna tena nafasi kwa walioko pale[kuzimu]; kungali na nafasi kwa
walio hai.” Nikamuuliza, “Bwana,
kwanini bibi yangu mkubwa yupo pale? Sijui kama alikujua wewe. Kwanini yupo
kuzimu Bwana?” akanijibu, “Binti, yupo hapa kwasababu alishindwa kusamehe….. binti, yeyote asiyesamehe, sitamsamehe huyu.”
Nikamuuliza, “Bwana, lakini wewe husamehe, na
una rehema.” Naye akanijibu,
“Ndiyo, binti, lakini nilazima kusamehe,
kwasababu hawajawasamehe wengi, na ndiyo maana wengi wapo hapa, wameshindwa
kusamehe…… nenda kawaambia wanadamu ni
muda wa kusamehe, hasa hasa watu wangu, kwakuwa wengi miongoni mwa watu
wangu hawajasamehe.
Waambie waache malaaumu, mafundo, chuki mioyoni mwao, kwa kuwa ni muda wa
kusamehe! Kama kifo kikimsitukiza mtu aliyeshindwa kusamehe, huyo mtu atakwenda
kuzimu, kwakuwa hakuna awezaye kununua maisha.”
Tulipoondoka hapo, bibi yangu mkubwa
alifunikwa na moto na akapiga makelele, "Aaaah,"
na akaanza kutukana jina la Mungu, na kumlaani Bwana; kila mtu kuzimu humtukana
Mungu.
Tulipoondoka eneo lile, nikaona kuwa kuzimu
imejaa roho ziteswazo. Watu wengi huinua mikono nje, wakimwomba Yesu msaada wa
kuwatoa nje, Lakini Bwana hakuwa na lolote la kufanya kwao, nao huanza
kumtukana Mungu.
Mara Yesu hulia sana na kusema, “Inaniumiza
sana kuwasikia, inaniumiza mimi sana wanavyofanya, kwasababu siwezi kufanya
lolote kwaajili yao.
Ninacho kueleza ni hiki; nina nafasi kwa hao
walioko duniani, ambao hawajafa, walio hai, wanao muda wa kutubu!” Bwana akaniambia
kuna watu wengi maarufu huku kuzimu, na pia wengi waliomjua Bwana.
SELENA MWUIMBAJI WA MUZIKI WA SALSA;
YESU Akasema,
“Nitakuonesha upande mwingine wa tanuru.” Tukaenda mahali penye mwanamke
aliyezingirwa na miali ya moto. Alikuwa katika maumivu makubwa na kupiga
makelele, akiomba huruma kwa Bwana.
Yesu akanyoosha mkono kwake na akaniambia,
“Binti, Yule mwanamke umwonaye pale, amezingirwa na miali ya moto ni Selena.”
Kadri tulivyokuwa tunamkaribia, akapiga kelele, “Bwana, nihurumie mimi,
nisamehe mimi Bwana, nitoe mahali hapa!” lakini Bwana akamtazama na kusema,
"Umechelewa, umechelewa sana, huwezi kutubu sasa.”
Selena
Aliponiona mimi akasema, “Tafadhari,
nakuomba wewe, waambie watu hivi, tafadhari sema na usinyamaze; nenda waambie
wasije mahali hapa; nenda waambie wasisikilize nyimbo zangu, wala wasiimbe hizo
nyimbo.”(1 Yohana 2:15).
Nikamuuliza, "kwanini unataka mimi niwaambie hivyo?" naye akanijibu,
"Kwasababu kila wakati watu wanaposikiliza nyimbo zangu, nateswa zaidi na
zaidi, na mtu anayeimba na kusikiliza nyimbo zangu, anaelekea mahali hapa.
Tafadhari, nenda uwaambie wasije huku; nenda
waambie kuzimu ni halisi, ipo kweli!”. Akapiga kelele na mapepo humchoma mikuki
na Selena kulia, “Nisaidie mimi, nihurumie mimi Bwana!” lakini kwa huzuni Bwana
alimwambia, “umechelewa sana.”
Nikaangalia pande zote za eneo lile, lilikuwa
limejaa waimbaji na wasanii waliokufa. Walikuwa wakiimba na kuimba, bila
kusimama. Bwana akanifafanulia, “Binti, mtu aliyepo hapa, lazima aendelee
kufanya kile alichokuwa anafanya duniani, kama hajatubu."
Kadri nilivyokuwa naangalia eneo lile, niliona
mapepo mengi yakinyunyiza vitu kama mvua. Nilidhani ni mvua inanyesha. Lakini
niliona watu kwenye miali ya moto wakikimbia mbali na ile mvua na kupiga yowee,
“Hapana, nisaidie, Bwana!.....
Hapana, haiwezekani kuwa hivyo,” na mapepo
yalikuwa yanacheka na kuwaambia watu, “Sifu na kuabudu kwasababu hapa ni ufalme
wenu milele na milele!” Niliona miali ya moto ikiongezeka na funza za
watu zikiongezeka zaidi! Hayakuwa maji yale bali kiberiti cha kuongeza miali ya
moto na kuongea maumivu ya kila mtu.
Nikamuuliza Yesu, “Ni nini kinachotokea?.....
Bwana, ni nini hiki?” Bwana akanijibu, “Huu ni ujira wa yeyote asiyetubu.”
(Zaburi 11:6). Bwana akanipeleka mahali alipo mtu aliyejulikana sana.
Papa John Paul II
Kabla ya maono haya, nilishi maisha kama
msichana wa kikristo wa nia mbili. Nilidhani kila mtu anayekufa anakwenda
Mbinguni; wale walifanyiwa ibada za mazishi watakwenda mbinguni, kumbe sikuwa
sahihi, nilikosa. Alipofariki Papa John Paul II, marafiki zangu na ndugu walisema
amekwenda mbinguni.
Taarifa zote kwenye LUNINGA [TV], na vyombo
mbalimbali vya habari vilisema, "Papa John Paul II amefariki, apumzike kwa
amani. Anafurahia sasa kuwa na Bwana na malaika Mbinguni" na mimi
niliamini yote kuwa ndivyo.
Kumbe nilikuwa najidanganya mwenyewe,
kwasababu nimemwona kuzimu, akiteswa kwa miali ya moto. Nilimtazama uso wake,
alikuwa mwenyewe Papa John Paul II! Bwana akaniambia, “Angalia, Binti, Yule mwanaume
umwonaye pale, ni Papa John Paul II. Yuko hapa; akiteswa kwasababu hakutubu.”
Papa John Paul II Lakini nikamuuliza, “Bwana, kwanini yuko hapa? Alikuwa akihubiri
kanisani.” Yesu akanijibu, “Binti, hakuna mwasherati, wala muabudu
sanamu, hakuna mchoyo na hakuna mwongo atakayerithi ufalme wangu.” (Eph
5:5).
Nikamjibu, “Ndiyo,
najua ni kweli, lakini nataka kujua kwanini yuko hapa, kwasababu alikuwa
akiwahubiria umati wa watu!" Na Yesu akanijibu, “Ndiyo, Binti, alisema mengi,
lakini hakusema kweli kama ilivyo. Hakusema kweli na kweli aliijua na japokuwa
aliijua kweli, alipenda fedha zaidi ya kuhubiri habari za wokovu.
Hakutoa uhalisia; hakusema kuzimu ni halisi na
mbinguni kupo; Binti, sasa yuko mahali hapa." Nilipomwangalia mtu huyu,
alikuwa na joka kubwa lenye sindano nyingi mwilini mwake, limemzingira
shingoni, naye hujaribu kumtoa.
Nalimwomba Yesu, “Bwana, msaidie!” aliko hupiga kelele, “Nisaidie mimi, Bwana nihurumie;
nitoe mahali hapa; nisamehe mimi! Ninatubu Bwana; Nataka nirudi duniani, nataka
nirudi duniani nikatubu.”
Bwana alimtazama na kumwambia, “Ulijua
vizuri yote haya. Ulijua vema kuwa kuzimu ni halisi, ipo…….. umechelewa; hakuna
tena nafasi kwaajili yako.”
WAABUDUO SANAMU
Bwana akasema, “Tazama Binti, nitakonesha maisha
ya mtu huyu.” Yesu akanionesha kioo kikubwa kama LUNINGA [TV]; nikaona
alivyotoa misa mara nyingi kwa umati wa watu. Na watu wale walivyokuwa waabudu
sanamu.
Yesu akasema, “Tazama, Binti, wapo waabudu
sanamu wengi hapa [Kuzimu]. Ibada ya sanamu haiwezi kuokoa
Binti. Ni mimi pekee niwezaye kuokoa, na nje yangu hakuna mwingine aokoaye.
Nawapenda wenye dhambi, lakini nachukia dhambi
Binti. Nenda na uwaambie wanadamu kuwa nawapenda na ninataka waje kwangu.” Kadri Bwana alivyokuwa akisema, nilianza
kuona mtu huyu akipokea makusanyo makubwa ya sarafu na fedha; vyote
alivihifadhi. Alikuwa na fedha nyingi sana.
Naliona sura yake imeketi katika mamlaka yake,
lakini pia naliweza kuona zaidi. Japo ni kweli watu hawa hawaoi,
ninakuhakikishia wewe, sizushi, Bwana alinionesha mimi, wanalala na masista; na wanawake
wengi!.
Bwana akanionesha watu hawa wanaishi kwa
uasherati, na neno linasema hakuna mwasherati atakayerithi ufalme wake. Kadri
nilivyokuwa naona,
Bwana akaniambia, “Tazama, Binti, yote
ninayokuonesha, ndiyo yanayoendelea, ndivyo alivyoishi [Papa] na ndivyo yanayotokea
katikati ya watu wengi, katikati ya mapadre na mapapa waliopo.”
Kisha Bwana akasema, “Binti, nenda na uwaambie
wanadamu ni muda wa kugeukia.” Bwana akanionesha sehemu watu wengi
wanavyoelekea kuzimu. Nikamuuliza, “Bwana, namna gani wanakuja huku?” akanijibu,
“Nitakuonesha.” Akanionesha lango lenye watu wengi wakipita.
Watu
hawa walikuwa wamefungwa toka mikononi hadi miguuni. Walivaa mavazi meusi na
kubeba mizigo mgongoni mwao. Yesu akasema, “Binti, hao watu uwaonao hawanijui
mimi bado.
Mizigo waliyobeba ni dhambi, lakini nenda
waambie walete mizigo kwangu, nami nitawapumzisha; kwa kuwa mie ndiye mwenye
kusamehe dhambi zao zote…. Binti, nenda na uwaambie waje kwangu, kwani
nawasubiri na mikono yangu iko wazi kuwapokea, na uwaambie hapo wanaelekea mahali
hapa [kuzimu].”
Kadri nilivyokuwa nawatazama watu wakitembea,
nikamwambia, “Bwana, Yule mtu pale ni binamu yangu; na Yule kijana pia, Bwana, na
Yule binti pale anayelekea kuzimu; oh familia yangu inakuja huku kuzimu!”
Bwana
akajibu, “Binti, wanakuja huku, lakini nenda uwaeleze wanakoelekea, nenda
waeleze kuwa wanakwenda kuzimu. Nenda waeleze kuwa nimekuchagua wewe uwe mlinzi wangu…… nimekuchagua wewe kama mlinzi, hii inamaanisha kuwa unatakiwa
uwaambie ukweli.
Unatakiwa uende uwaeleze yote niliyokuonesha
wewe. Kama hutawaambia na jambo likampata mtu huyu, damu yake itakuwa juu yako,
lakini ukiende na kufanya nilivyokueleza, hapo mtu huyu nitamdai mwenyewe.
Kama mtu hatatubu, hapo wajibu ulionao
utaondolewa, kwa kuwa atadaiwa mwenyewe na damu yake haitakuwa juu yako.
(Ezekia 3:18)" Yesu akaniambia wengi wa watu maarufu wanaelekea huku
[kuzimu], maarufu na watu muhimu.
MICHAEL JACKSON.
Kwa mfano, Michael Jackson. Huyu alikuwa
maarufu duaniani kote lakini alikuwa mjumbe wa shetani. Japokuwa wengi wanaweza
wasione na kuelewa hivyo, lakini huo ndiyo ukweli.
Huyu alikuwa na mkataba na shetani;
alikubaliana na shetani ili awe na heshima na sifa ilikuwa vutia wapenzi wengi.
Michael_Jackson Hizo hatua na mitindo aliyokuwa anafanya, ndivyo nilivyoona
mimi mapepo yakicheza na kutembea yanapotesa watu kuzimu.
Yalikuwa yanateleza kwa kurudi nyuma na siyo
mbele, huku yakipiga kelele; yakifurahia mateso wanayopata watu. Ngoja
nikuambia wewe kuwa Michael Jackson yuko kuzimu. Bwana alinionesha baada ya
kufa Michael.
Alinionesha Michael Jackson akiteswa kwenye
miali ya moto. Nikalia kwa Yesu, “Kwanini?” haikuwa rahisi kuona mtu
huyu alivyokuwa anateswa na alivyokuwa analia na kupiga mayowe.
Yeyote anayesikiliza nyimbo za Michael Jackson
au kuziimba au ni mpenzi/shabiki wa Michael Jackson, ninakuonya kuwa shetani
anakutega katika mtego wake ili mwisho uishie kuzimu.
Mara hii, jitoe na kumkana shetani kwa jina
Yesu! Yesu anataka kukuweka huru wewe, ili usipotee milele. Bwana akaniambia, “Binti,
kuna watu wanijuao pia wanakuja huku kuzimu.” Nikamuuliza, “Bwana, inakuwa je mtu akujue halafu aje
huku?”
Akanijibu, “Mtu Yule aliyeacha njia zangu na
mtu Yule anayeishi aina mbili za maisha [wokovu na dhambi].” Akaanza
kunionesha watu wanaoelekea kuzimu. Walikuwa wamefungwa kamba toka mikononi
hadi miguuni.
Kila
mmoja alivaa vazi jeupe, lakini limetobokatoboka, lina-mabakamabaka na
limekunjamana. Yesu akaniambia, “Binti, angalia watu walioniacha mimi.
Binti, nataka kukueleza, siji duniani kwaajili ya watu
hawa. Nakuja kwaajili ya watakatifu, waliotayari, wasiolaumiwa, wasio na
makunyanzi na wasio na mawaa…… nenda uwaambie warejee kwenye njia zao za
zamani,” (Efeso 5:26-27).
Nilianza kuwaona wengi miongoni mwa wajomba
zangu na watu wengine wengi waliorudi nyuma na kuziacha njia za Bwana. “Nenda
kawaambie ninawasubiri, walete mizigo yao nami nitawapumzisha."
YESU alikuwa analia baada ya kusema hayo,
“Binti, wanakuja huku [kuzimu]. Nenda kawaambie wajomba zako; nenda kawambie
ndugu zako kuwa wakuja huku! Binti, wengi hawatakuamini, lakini mimi ni shahidi
wako mwaminifu, ni shahidi wako mwaminifu. Sitakuacha wewe.
Hata kama hawataamini, Binti, nenda na
uwaambie ukweli huu, kwa kuwa nipo nawe. Pia Binti nitakuonesha jinsi watu
wanavyofika huku.” Tulikwenda kwenye lango, ambapo tuliona umati wa watu
wakiangukia ndani ya shimo kubwa.
Siyo elfu moja wala elfu mbili, bali wingi
wake kama mchanga wa bahari, hawana idadi! Walikuwa wananguka kwa kila sekunde,
mfano wa mkono uliojaa mchanga umwakikapo chini. Zile roho zilikuwa zinaanguka
kwa kasi.
YESU alikuwa akilia, na kusema, “Binti
hivi ndivyo wanadamu wanavyopotea; hivi ndiyo mwanadamu apoteavyo!!!.....
Binti, inaniumiza sana mimi nionavyo wanadamu wanavyoangamia.”
FAMILIA ZA WACHUNGAJI NA WACHUNGAJI.
YESU akasema, “mapepo pia hufanya mikutano huku
kuzimu” Na nikasema, “mapepo yanafanya mikutano?” Yesu akasema,
"Ndiyo, Binti, wanakutana kupanga, kupanga watavyowafanya wanadamu.
Wanakutana kila siku kwa siri.” Na kwa hilo,
Yesu akanipeleka kwenye sero, ambapo niliona meza ya mbao na viti vikizunguka
meza. Na palikuwa na mapepo, aina zote za mapepo.
Yesu
akaelezea, “Binti, wanapanga kwenda kuharibu nyumba/familia za wachungaji,
wamisionari, wainjilisti na wote wanijuao mimi. Binti wanataka kuwaharibu;
wanamishale mingi.”
Mapepo hucheka na kudhihaki, na kusema, “acha
tuwaharibu wanadamu na kuwaleta huku.” Yesu akasema, “Nenda na uwaambie nipo
pamoja nao watu wangu.
Waambie wasiache milango wazi, wasimpe nafasi
shetani, kwa kuwa shetani anazunguka-zunguka kama simba angurumaye, akimtafuta
wa kummeza. (1 Petro 5:8)"
Lakini neno linasema, "anatembea
kama", kwasababu simba halisi, ni Simba wa Yuda, Yesu Kristo wa Nazareti
(Ufunuo 5:5)! Yesu akasema, "Binti, wanataka kuharibu/kuangamiza
familia za wachungaji.”
Nikamuuliza, “Kwanini wanataka kuharibu
familia za wachungaji?” na Yesu akajibu, “Kwasababu wanawajibu wa maelfu
ya watu ambao ni kondoo wa kundi; kondoo wa kundi Bwana aliowakabidhi wao.”
Wanataka watu hao warudie dunia tena;
waangalie nyuma na kuishia kuzimu…. Nenda kawaambie wachungaji kusema iliyo
kweli tupu. Waeleze wahubiri kweli tupu na kusema kila kitu ninachowaambia na
wasinyamaze nayo haya ninayowaambia!”
Tulipokuwa tunaondoka hapo, akaniambia, “Nataka
nikuoneshe kitu kingine…. Wapo pia watoto huku.” Na nikamjibu, “watoto
huku Bwana?
Kwanini wawepo watoto huku? Neno lako lasema,
'Waacheni watoto wadogo waje kwangu, na msiwazuie: kwa maana Ufalme wa Mbinguni
ni wao." (Mathayo 19:14)
Yesu akajibu, “Binti, ni kweli, ufalme wa
mbinguni ni wao, lakini mtoto lazima aje kwangu, kwa kuwa kila ajaye kwangu
sitamtupa kamwe." (Yohana 6:37)
WAANGALIA KATUNI
(Cartoon).
Ghafla, Bwana akanionesha mvulana wa miaka
nane(8) akiteswa kwenye moto. Mvulana akalia,
“Bwana nihurumie mimi, nitoe mahali hapa, sitaki kuwepo hapa!” aliendelea
kupiga kulia na kelele.
Nikaona mapepo yamemzunguka mtoto huyu,
yaliyofanana na cartoon.Kulikuwa na aina za Dragon, BoyZ, Ben 10, Pokémon, Doral, na
nyingine nyingi.
“Bwana, kwanini mtoto huyu yuko huku?" Yesu akanionesha picha ya mkanda wa maisha mtoto huyu.
Nilimwona anavyotumia muda karibia wote kwenye LUNINGA [TV] akiangalia cartoon.
Cartoon ya Ben 10: Pokemon: Yesu akasema, "Binti,
hayo maigizo ya cartoon, sinema zake, michezo mbalimbali ya kuigiza
inayooneshwa kila siku kwenye LUNINGA [TV] ni vyombo vya shetani atumiavyo
kuwaharibu wanadamu….. tazama, binti ilivyotokea kwa mtoto huyu."
Nilimwona jinsi mtoto huyu alivyokuwa mkaidi
na asiye mtii kwa wazazi wake. Wazazi wake aliposema naye alikimbia na kutupatupa
vitu ovyo na kuto-watii.
Baada ya hapo akagongwa na gari na ukawa
mwisho wa maisha yake. Yesu akasema, “Tangu hapo yupo mahali hapa.” Nilimtazama
mtoto Yule akiteswa.
Yesu akasema, "Binti, nenda na uwaambie
wazazi wawaelekeze watoto wao kama ilivyo katika neno langu.”(Mithali 22:6)
Neno la Mungu ni halisi, linatuambia tumwonye mtoto kwa fimbo, lakini si kila
wakati, pale tu mtoto anapoonyesha ukaidi kwa wazazi. (Mithali 22:15)
Bwana akaniambia kitu cha kuhuzunisha sana na
kuumiza mno. Akasema, “Binti, wapo watoto wengi sana huku kwasababu ya cartoon, kwasababu
ya ukaidi.”
Nikamuuliza, “Bwana,
kwanini lawama ziwe hizi cartoon?” Naye akanieleza, “Kwasababu ni mapepo yanayobeba
ukaidi, kiburi, ukali na chuki kwa watoto, ili wasifanye vitu vizuri;
na mapepo mengine huwaingia watoto ili wasifanye mambo mazuri,
bali wafanye mabaya: vile waonavyo kwenye LUNINGA [TV] watoto hutaka kufanya
vivyo hivyo.”
Kuzimu ipo, kuzimu ni halisi, na watoto lazima
waamue watakwenda na nani. Nikasema, “Bwana,
niambia, kwanini kuna watoto huku?” na Yesu akanijibu, “Mara watoto wapatapo kujua kuna
mbinguni na kuzimu, hapo wanayonafasi ya kuchagua UFALME WA MBINGUNI.”
YESUKRISTO AKANIONYESHA MBINGUNI
Kuna mengi ya kusema juu ya kuzimu, lakini
kwasasa niwashirikishe niliyoyaona Mbinguni. Yesu akasema, "Binti, sasa nitakuonesha
nilichowaandalia watakatifu wangu.”
Tuliondoka kule kuzimu kupitia lango lake.
Tulipokuwa tukisafiri kutoka nje ya kuzimu, ghafla tukatokea mahali penye
mwanga. Sikuona giza tena, mateso wala miale ya moto.
Akasema, “Binti, nitakuonesha utukufu wangu,”
na tukaanza kupanda juu kwenda Ufalme wa Mbinguni! Mara tukafika kwenye mlango
wenye maandishi makubwa yaliyoandikwa kwa dhahabu, yalisema: “Karibu
kwenye Ufalme wa Mbinguni.”
LANGO LA MBINGUNI Yesu akasema, “Binti, ingia,
kwa kuwa mimi ni Mlango na kila aingiaye kupitia kwangu, ataingia na kupata
marisho.”(Yohana 10:9) Baada ya Bwana kusema maneno hayo, mlango ukafunguka na tukaingia.
Niliwaona malaika wakimpa utukufu, heshima na
sifa Baba Yetu wa Mbinguni! (Ufunuo 7:11-12) Kadri tulivyozidi kutembea,
tulikaribia meza niliyoweza kuona mwanzo wake laini siyo mwisho, (Ufunuo 19:9).
Niliona enzi kubwa, na enzi ndogo zimezungukwa
na maelfu ya viti. Katikati ya viti niliona mavazi na mataji. Bwana akaniambia,
“Binti, taji unayoiona pale ni taji ya Uzima."(Ufunuo2:10)
Yesu akasema, “Tazama, Binti, hii ndiyo
niliyowaandalia watu wangu.” Niliona ile meza imefunikwa na vitambaa vyenye
upindo wa dhahabu. Kulikuwa na sahani, glasi za dhahabu, matunda; kila kitu
kimeandaliwa. Ilikuwa nzuri ajabu.
Kulikuwa na chombo kikubwa katikati ya meza,
kilichokuwa na mvinyo tayari kwa mulo. Na Yesu akasema, “Binti, kila kitu kipo tayari
kwa ujio wa kanisa langu.” MEZA YA KARAMU YA MBINGUNI Tulikwenda mahali
pengine, niliwaona watu wengi wakiwa bustanini.
MFALME DAUDI, JOSHUA,
MUSA, IBRAHIMU,SARA NA MARIA.
Kulikuwa na watu wanaofahamika sana kwenye
Biblia, lakini hawakuwa wazee, bali vijana. Palikuwa na kijana akiwa na
kitambaa mkononi, akicheza na kuzungukazunguka na kumsifu Bwana. Yesu akasema,
“Binti, Yule kijana pale ni mtumishi wangu Daudi.” Alikuwa akimpa utukufu Baba
yetu.
Ghafla, kijana mwingine akapita na Yesu
akaniambia, “Binti, huyu ni Joshua; Yule Musa; na Yule pale ni Ibrahimu.” Yesu
huwaita kwa majina yao.
Wote walikuwa na mwonekano mmoja! Ajabu sana
Mbinguni! Yesu akasema, “Mwanamke Yule ni mtumishi wangu, Maria
Magdalena; na Yule mtumishi wangu Sara."
Lakini pia akaniambia, “Binti, huyu ni Maria.
Maria, aliyemzaa Yesu Kristo, ambaye ni mimi. Binti, nikwambie, yeye
hana habari ya yanayotokea duniani.
Nataka kukwambia, nenda kawaambie wanadamu, waambie
waabudu sanamu kuwa kuzimu ni halisi, na waabuduo sanamu hawata urithi
Ufalme wangu, lakini waambie kama wakitubu, wataweza kuingia makao ya mbinguni.
Nenda waambie nawapenda na pia waambie Maria
hajui chochote [kinachotendeka duniani] na pekee wanayeweza kuheshimu ni mimi,
kwasababu si maria wala mtakatifu Gregory wala mtakatifu yeyote awezaye kuokoa.
Mimi ndiye niokoaye na nje yanguhakuna yeyote,
hakuna yeyote, hakuna yeyote – aokoaye!” Alirudia mara tatu-kuwa hakuna yeyote awezaye
kuokoa; isipokuwa yeye.
Wanadamu wamedanganywa na kuamini kuwa kwa
kupitia wadhani wao ni watakatifu, sivyo ilivyo, bali ni mapepo, yafanyayo kazi
kupitia sanamu zilizofanywa kwa mikono ya watu.
Lakini ngoja nikueleze kwamba Bwana anataka
kukupa kilicho bora. Anataka wewe uingie katika Ufalme wa Mbinguni; tubu na
kuacha uabudu sanamu.
Kwasababu ibada ya sanamu haitakuokoa wewe.
Yesu Kristo wa Nazareti ndiye pekee aokoaye, aliyeutoa uhai wake kwaajili yako,
yangu na kwaajili ya wanadamu wote.
Bwana ana ujumbe mzito kwa wanadamu. Huku
akilia aliniambia, “Tafadhari, Binti, usikae kimya; nenda na uwaambie ukweli,
nenda na uwaambie nilichokuonesha wewe.” Sanamu za Maria na Waumini wa
kisujudia Nilimwona Maria akimwabudu Bwana, na niliwaona wanawake wakiwa na
nywele ndefu nzuri.
Nikasema, “Bwana, wanapendeza sana walivyoweka nywele
zao.” Akaniambia, “Binti, kile uonacho ni utaji niliowapa wanawake.”
Akaongeza, “Binti, nenda na uwaambie wanawake watunze utaji niliowapa.”
Kisha akaniambia, “Nina kitu cha muhimu cha
kukuonesha.” Nikatazama mbali kidogo na kuona MJI UNG’AAO, MJI WA DHAHABU!
Nikasema, “Bwana, kile ni nini? Nataka kwenda pale.”
Akanijibu, “Binti, nitakuonesha kilichopo
pale. Ukionacho ni makao ya Mbinguni, majumba ya Mbinguni yaliyotayari kwaajili
ya watu wangu.”
Tulianza kutembea, hadi tukafika kwenye daraja
la dhahabu. Mara tulipovuka daraja, tukafika kwenye mitaa iliyotengenezwa kwa
dhahabu safi! (Ufunuo 21:21)
Kila kitu kilikuwa kizuri sana, kuzuri sana
pale, kunang’aa kama kioo, ni mahali pasipo pakawaida, hakuelezeki! Tuliona
majumba ya ki-mbinguni na pia tuliwaona, maelfu ya malaika wakijenga.
Baadhi ya malaika walikuwa wanajenga kwa
haraka ya ajabu, na wengine pole pole na wengine walikuwa wamesimama kabisa
kujenga.
Nikamuuliza Bwana, “Kwanini malaika wengine
wanajenga haraka haraka, wengine polepole, na wengine wamesimama?" Bwana
akanieleza, “Binti, hivyo ndivyo wafanyavyo watu wangu duniani, na malaika
wanafanya kama wafanyavyo watoto wangu duniani….
Binti, watu wangu hawahubiri neno
langu.
Watu wangu hawafungi tena. Watu
wangu hawaendi mtaani kusambaza ujumbe wa neno langu kwa vipeperushi
vinavyoeleza ukweli. Watu wanaona aibu kuhubiri. Nenda kawaambie watu
wangu warudi kwenye njia za zamani.
Wale malaika uliowaona hawafanyi chochote ni
malaika wa watu wangu waliorudi nyuma na kuacha njia zangu… Binti, nenda
waambie watu wangu warudi njia zao za zamani,” (Yeremia 6:16) na baada ya
kusema haya akaanza kulia Bwana.
Nikasikia watu wengine wakiimba, hivyo
nikamuuliza, “Bwana, nataka unipeleke kule, ambako watu wanaimba.” Yesu alikuwa
akiniangalia, nakwambia jinsi alivyokuwa ananiangalia, sikuweza kuona vema uso
wake bali alikuwa akigeuza uso wake.
Wakati huo machozi yalikuwa yakimtiririkia
kwenye vazi lake, nikamuuliza kwanini analia. Lakini hakuweza kunieleza.
Baadaye tulifika kwenye bustani nzuri sana.
Pale katika majumba ya mbinguni, niliona maua
yalikuwa yakiyumbayumba huku na huku kama yapulizwayo na upepo. Hizi huenda
ndizo sauti za kuimba nilizozisikia.
Bwana akaninyoshea kidole na kusema, “Binti,
tazama, maua yananisifu mimi; yananiabudu mimi! Watu wangu hawafanyi hivi tena
kama walivyokuwa wanafanya mwanzo.
Watu wangu hawanisifu, hawaniiabudu mimi; hawanitafuti mimi kama
mwanzo. Ndiyo maana nalikwambia mwanzo,
Binti, nenda na uwaambie watu wangu wanitafute, kwa kuwa
nitakwenda, nitakwenda, nitakwenda kwa wanaonitafuta kwa roho na kwa kweli, kwa
watu walio tayari, kwa watakatifu!”
na huku
akilia akasema, “Ninakuja, ninakuja!” hapo nikaelewa kwanini alikuwa analia,
kwasababu anakuja, lakini si kwa wasio na nia, watu wa nia mbili [vuguvugu].
Atarudi kwa wale tu wanaomtafuta katika roho na kweli.
Ndipo Bwana akaniambia ninatakiwa kurudi
duniani. Nikasema, “Bwana, Sitaki kurudi duniani! Unamaanisha nini- duniani?
Nataka kubaki na wewe Bwana. Umenileta huku na mimi siendi kokote kwasababu
niko na wewe!”
Yesu
akasema, “Binti, ni muhimu urudi duniani ili ukashuhudie kwamba utukufu wangu ni
halisi, yote niliyokuonesha kuwa ni kweli; ili wanadamu waje kwangu, watubu na
wasiangamie.
Bwana akaanza kulia, nami nikaanguka miguuni
pake; nikaona vidonda kwenye miguu yake. Nikamuuliza, “Bwana, hivi ni vidonda
vya nini?” akajibu, “Binti, ni vidonda ya jana, nilipotoa maisha yangu kwaajili
ya wanadamu.”
MKONO WA YESU Bwana akanionesha vidonda vyake
vya mikononi, nilimuuliza, “Bwana, kwanini ungalinavyo hata sasa?” akaniambia,
“Binti,
ni vidonda vilivyobaki.”
Hivyo nikamuuliza, “je vitapona?” akanijibu,
“Vitapona na kufutika tu baada ya watakatifu wote kuungana hapa….. Binti,
lazima nikurudishe duniani: Familia yako na mataifa yanakusubiri wewe.”
Nilijaribu kukataa lakini akanyosha kidole
chake chini duniani na kusema, “Tazama, wale watu uwaonao chini pale ni
ndugu zako; na mwili ule uuonao pale, ndiyo utakaoingia…… ni muda wa kuondoka
mahali hapa.”
Baada ya hapo akaanipeleka kwenye mto mzuri
mwangavu na akasema, “Binti, ingia katika mto na jizamishe
mwenyewe.”
Kabla sijaingia ndani ya mto wa maji ya uzima,
nilikuwa najisikia furaha ya ajabu, lakini baada ya kujizamisha na kutoka nje,
nilipata furaha kuu. Nilidhani sitarudi tena nyumbani kwetu, lakini Bwana
akaniambia,
“Binti,
unatakiwa kurejea duniani….. Binti, nitakuonesha kitu: jinsi nitakavyorudi mara
ya pili kwaajili ya watu wangu watakatifu.
Nitakuonesha jinsi siku ile ya kutisha
itakavyokuwa.” FURAHA NA MAOMBOLEZO Tulitembea hadi sehemu yenye kioo kikubwa kama
LUNINGA [TV], nikaona watu.
Niliweza kuona dunia yote. Ghafla nikaona
maelfu ya watu wakipotea. Wanawake wenye mimba, mimba zilipotea, na wakawa kama
wamechanganyikiwa na kupiga mayowe. Watoto walitoweka pande zote.
Watu wengi walikuwa akikimbia huko na huku,
wakipiga kelele, “Haiwezekani, haiwezekani, nini hiki kitokeacho?” Niliwaona
wale waliomjua Bwana na kuachwa nyuma. (Mat.24:40-41) Walikuwa wakisema Kristo
amekuja, furaha imetimia.
Walikuwa wakipiga kelele na kutafuta kujiua
wenyewe lakini hakuwezekana. Bwana akaniambia, “Binti, siku hizo kifo
kitawakimbia; Binti, siku hizo Roho Mtakatifu hatakuwepo tena.” (Ufunuo
9:6) kulikuwa na ajali nyingi lakini sikuona hata mtu mmoja aliyekufa: wote
walikuwa wazima japokuwa wameumia [majeruhi].
Niliona mlolongo mrefu wa maelfu ya watu.
Akaniambia, “Binti, tazama, hivi ndivyo kila kitu kitakavyokuwa.” Kisha nikaona
watu wakikimbia kutoka sehemu moja kwenda nyingine, wakipiga kelele, Kristo
kaja, Kristo kaja!” wakisihi, “Bwana nisamehe mimi, nisamehe mimi, nichukue
nawe!”
Baada ya Bwana kuwachukua watu wake [Unyakuo]
Lakini kwa huzuni Bwana akasema, “Watakuwa wamechelewa. Muda wa kutubu ni
sasa…. Binti, nenda kawaambia wanadamu wanitafute mimi, wakati huo hakutakuwa
na nafasi. (Isaya 55:6)
Binti, watakuwa wamechelewa wote watakaobakia
nyuma.” Baada ya Yesu kuona watu wataobaki nyuma akaanza kulia na kusema,
“Binti, nitakwenda duniani kama neno lisemavyo
katika 1 Thes. 4: 16-17: “Kwasababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka
mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu;
nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.
Kisha sisi tulio hai,
tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani;
na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi farijianeni kwa maneno hayo.”
SIKU YA MWISHO Lakini si kila mtu atakwenda na
Bwana, wale tu wafanyao mapenzi yake (Mathayo 7:21) na aishiye maisha
matakatifu.
Kwa kuwa Bwana aliniambia, “Wale tu walio
watakatifu wataoingia Ufalme wa Mbinguni, (Waebrania 12:14) Hakuna ajuaye, siku
wala saa nitakayokuja kwaajili ya watu wangu watakatifu, hata malaika hawajui.”
(Mathayo 24:36)
Kwenye Kioo cha LUNINGA [TV] niliona watu
wakikimbia huko na huku. Magazeti yalisema “KRISTO AMEKUJA.” Kioo kikafungwa,
na Yesu akamalizia kwa kusema, “Ninakuja kwa watakatifu.”
Hivi ndivyo alivyonionesha mimi. Baada ya hapo
akanirudisha duniani hapa. Tukiwa na kusanyiko la malaika wengi wakituzunguka,
tulianza kushuka ngazi nzuri kama nini; ngazi nyeupe na maua yakizunguka.
Nilikuwa nalia njia nzima kushuka chini,
nikimsihi Yesu, “Bwana tafadhari usiniache hapa.
Nichukue niwe nawe!” Alinijibu, “Binti,
mataifa yanakusubiri, familia yako wanakusubiri wewe…….. Binti, lazima urejee
mwili wako. Lazima upokee uhai wako, Binti, ili uweze kwenda kushuhudia yote
uliyoyaona.
Wengi hawatakuamini wewe; wengi watakuamini,
bali mimi ni shahidi wako mwaminifu. Niko pamoja nawe.
KURUDI DUNIANI KWA ANGELICA
Maxima: Binti yangu aliporudi, tulikuwa
tunamsubiri pale, na alikuwa amelazwa pale pale chini sakafuni. Nikasikia
mguno, "uuhmm," bila kitu.
Nikasema, “ahsante Bwana kwasababu Binti yangu
amerudi!” Sote tulimshukuru Bwana. Mara akaanza kupumua polepole,
kidogo kidogo. Baada ya muda wa masaa matano, alikuwa na uwezo wa kufumbua
macho na kusema.
Mwanzo tulipata shida kumuelewa asemacho;
ilikuwa ni vigumu kumuelewa. Hakuwa na nguvu kabisa. Ilibidi tufunge madirisha
kwasababu macho yake hayakuwa na uwezo wa kuhimili mwanga.
Kwakuwa wadadisi, sote tulitaka atueleze
alichoona.
Lakini kwa kuwa alikuwa dhaifu, aliweza kutueleza kidogo tu.
Ilimchukua karibu wiki mbili hadi alipoweza kutushirikisha habari nzima ya
ushuhuda wake.
Mapepo yalikuja kumtesa baada ya hayo yote.
Aliweza kuyaona waziwazi; yalijaribu kujificha kwenye vivuli. Yalikuwepo hapa
karibu siku tatu mfululizo tangu arudi, kabla hajaweza kutueleza.
Aliyauliza yalikuwa yanataka nini, nayo
yakamjibu, “tumekuja kufanya mkataba nawe……. Ni lazima ufunge mdomo, ni lazima
usiseme lolote ya hayo uliyaona kule chini, kwasababu ukisema, tutakuuwa.”
Aliyaelezea yalivyo mapepo, yana sura mbaya,
makubwa na manene yanatisha. Alisema hakuna maneno yakuelezea jinsi yatishavyo
kwa mwonekano. Alijaribu kuyakemea lakini yalikataa kuondoka.
Yakifika yalikuwa yanamrukia na kumchoma. Naye
aliendelea kupambana nayo na kuyakemea, lakini hakuweza kwasababu hakuwa na
nguvu. Siku moja alipokuwa anayakemea, mwanga mkali wa ajabu ulitokea na
yakakimbia yote! Alikuwa ni Bwana.
Alichopitia Binti yangu hakikuwa rahisi.
Alipewa ujumbe wenye maono ya ndani kwaajili ya wanadamu, ili wamtafute Mungu.
Wanadamu wanadhani wafanyayo ni sahihi.
Vijana wamezama kwenye madawa ya kulevya na
pombe, na kuona ni sawa maisha hayo, lakini si sawa. Miongoni mwa alioneshwa
binti yangu ya kutisha ni wasanii wengi walivyojaa kuzimu, wanamuziki/wacheza
dansi na pia Papa John Paul II.
Ni wakati wa kumtafuta Bwana, kutubu, na
kujishusha na kujidhiri mbele za zake. Neno la Mungu ni kweli lisemalo, “Mbingu
na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.”(Marko 13:31) Neno la
Bwana litatimizwa katika muda wake.
Bwana alimwonesha tanuru ambalo watu walikuwa
wanatembea kuelekea kuzimu. Na watu wengi tayari wakiwakuzimu.
Ni kweli haya, lakini hata watu wa Mungu
hawaamini haya, wengi hawaamini. Ujumbe mkuu ni kwamba tumtafute Bwana, siyo
kwa kinywa/mdomoni, bali kutoka ndani ya moyo, kwakuwa kurudi kwa Bwana
ku-karibu.
Yesu alisema, “Siko tena mlangoni; niko zaidi
ya mlangoni. Nakuja muda simrefu; kuja kwangu ku-karibu. Watu wangu wameniacha
na wamerejea mambo ya duaniani……… waambie watu wangu warudie njia zao za
zamani.”
Kanisa leo linatakiwa kurudia njia zake za
zamani; hapa tulipo ni wa motoni, tumtafute Bwana. Pale parapanda ikilia tuwe
tayari kukutana na Bwana, itakuwa ajabu sana! UJUMBE WA MUHIMU WA BWANA kupitia Angelica akiongea mbele ya haraiki:
Bwana akaniambia, “Binti, siku hizo Roho Mtakatifu hatakuwepo tena duaniani. Siku hizo
hatakuwepo duniani.” (2 Thes. 2:7)
Na
nikaona msongamano mkubwa wa magari na ajali nyingi sana.
Watu wengi walijaribu
kujiua, lakini Yesu akasema, “Watatafuta kifo, lakini kifo kitawakimbia
wanadamu.
Kifo hakitakuwepo tena siku hizo.”(Ufunuo 9:6)
Nikawaona watu wakitazama LUNINGA [TV] na kusoma magazeti yakisema, “Maelfu na
maelfu wamepotea.” Wengi watajua kuwa Yesu ameshakuja kwaajili ya watu wake
watakatifu.
Wale waliomjua Bwana lakini wameachwa,
wakakimbia mitaani wakilia, wakijaribu kujiua wenyewe lakini hawakuweza lolote.
Nilipokuwa mbinguni, Yesu alisema, “Nina
kuja duniani kwaajili ya watu wangu watakatifu na ninakuja mapema kwaajili ya
kanisa langu.”
Lakini wiki mbili zilizo pita Bwana
aliniambia, “Binti, ninafurahishwa na unavyotenda, kwa kuwa unatimiza niliyokuagiza
na nakukupa, lakini usiwaambie watu wangu kuwa nitakuja mapema, waambie
ninakuja sasa hivi.”
Tena Bwana akasema, “Waambie watu wangu ninakuja sasa
hivi na ninakuja kwa watu watakatifu. Waambie watu wangu nakuja kwa watakatifu
tu, nao ndio wataoniona mimi!.... tena usinyamaze: endelea kuwashuhudia
ninayokwambia.”
------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
“Sasa umesikia ushuhuda huu, usiipoteze nafasi
hii ukaijutia milele na milele motoni.”
Kwa wale waliotayari kumpokea Bwana,
wafuatiane nami katika maneno haya: Bwana, ninakushukuru kwa Upendo na huruma
yako, ahsante Bwana kwa maneno yako yaliyotufikia mioyoni leo. Baba, ninaomba
msamaha kwako, unisamehe. Unisamehe mimi. Unioshe kwa damu yako ya thamani.
Andika jina langu katika kitabu cha uzima. Nipokee/nikubali mimi niwe mwanao
Bwana. Sasa hivi, ninamsamehe kila mtu niliyeshindwa kumsamehe. Ninakana hali
yangu ya kutosamehe. Ninayakana yote yalinizuia nisikufuate Bwana, ninaomba
unibadilishe Bwana na unijaze uwepo wako ndani yangu kila siku. Katika jina la
YESUKRISTO ameni.
Be blessed by almight God in the name of Jesus Christ
ReplyDeleteAmen🙏Glory to christ.Thank you
Delete