Ufunuo wa kiMungu kuhusu kuzimu ya moto na Emmanuel Agyarko.

 Emmanuel Agyarko ni kijana kutoka Kumasi nchini Ghana.Alianza kuona maono ya kiMungu toka alivyokuwa mtoto.Akieleza ‘Hata hivyo ilivyofika mwaka 2009 ilizidi sana, na Bwana alinionyesha maono mengi ,lakini ilipofika tarehe 24 mwezi wa 11 mwaka 2011,mchana nilipokuwa natoka shule.

Nilijiona nimechukuliwa na Bwana mchana,mchana nilipokuwa narudi kutoka shule na Bwana akanipeleka kuzimu kunionyesha mambo mbali mbali ambayo kwa hayo wanadamu walioko duniani wataonywa ili wasiiendee njia ya kuzimuni.

WACHUNGAJI WASIOTOA FUNGU LA KUMI.
Bwana alinionyesha wachungaji wanne(4) kuzimu, ambao walikuwa hawatoi fungu la kumi hapa duniani.Mmoja aliitwa Albert na mwingine alikuwa Daniel, Mchungaji wa Kanisa la YESU na katika kanisa lake walikuwa hawaamini katika kutoa fungu la kumi.Daniel aliniambia kuwa alikuwa akiwaambia waumini wake wasitoe zaka na sio muhimu tena.Danieli alikuwa kuzimu kwa makosa mawili(2) ,kwanza kwa kutokutoa fungu la kumi na kosa la pili ni kuzuia wengine kutoa fungu la kumi.
Albert, kanisa lake lilikuwa likiamini katika kutoa fungu la kumi ,lakini yeye alijua ni kwa ajili ya waumini pekee ndio wanaotakiwa kutoa fungu la kumi na sio wachungaji.Alikuwa akitamani japo arudi duniani ili aanze upya na atoe zaka kama inavyotakiwa.
Wachungaji wengine wawili(2) hawakuwa wakitoa zaka,mmoja wao alijua na alidhani hatakiwi kutoa zaka hata kama alijua,mwingine aliona kuhudumu kama vile hakuelekei vizuri hivyo hahitaji kutoa fungu la kumi.

WATU WANAOTUMIA HIRIZI ILI KUPATA WAUME.
Niliona wanawake wengi waliotumia hirizi ili kupata waume ili waolewe.Wengine walitumia lipstiki za kiganga,make-up za kiganga ili kuweza kutongoza wanaume.Nilimuona mwanamke mmoja aliyeandikwa jina lake Ama Gyamfua aliyekuwa akihudhuria kanisa la Pentekoste, naye alipewa hirizi kutoka kwa mnganga wa kienyeji iliamuendeshe mume wake kama mbwa; Hiyo ndiyo sababu alikuwa kuzimu akiungua moto kutokana na kutumia hirizi.Mwanamke mwingine niliye muona aliitwa Mavis ambaye yeye alikuwa akipaka midomo yake kwa lipstiki, na alipewa lipstiki hiyo na mganga wa kienyeji na kila alipokuwa akiitumia ilikuwa inafanya wanaume wamtamani kulala naye alikuwa akijipatia fedha kutoka kwa wanaume hao.

Niliona mwanamke mdogo anayeitwa Vivian ambaye alionekana kama vile alikuwa ana miaka 24,akiwa ana nguo za aibu sana ziko fupi sana, alikuwa na kucha ndefu zilizoandikwa,amejidobeka lipstiki na skafu kichwani mwake.Yupo kuzimu kwa sababu alikwenda kutafuta hirizi kutoka kwenye miungu, Hivyo alipo lala mwanaume yeyote alikuwa akichokua mbegu za wanaume(semen/manii/shahawa) na kuzipeleka kwenda kufanyia dawa.Kutokana na vitendo vyake hivyo wanaume watano(5) walishafariki, Na alikuwa akifanya hivyo ili aweze kupata fedha, Aliniambia alikuwa akivaa kiaibu sana alipokuwa duniani ili awatongoze wanaume na alikuwa akiishi Kwashieman,Accra,Ghana.

Niliona mwanamke ambaye alikuwa ni mke wamchungaji duniani naye ni Alice.Alikwenda kwa kutafuta hirizi kwa ajili ya mumewe,Aliniambia alikuwa ni mchawi na alikwenda kutafuta dawa/hirizi.Aliweka damu za siku zake(hedhi kwenye maji ya dafu akachanganya na vitu vingine ili mume wake anywe.Na muda huo huo mumewe alipokula vitu hivyo akawa kama mtoto wake yani anaweza kumdhibiti n kumendesha vyovyote atakavyo.Kiroho alimfungia mumewe kwenye chupa.
Pia aliweza kuua baadhi ya washirika na alipokufa alitupwa mara moja kuzimu kwa vile vyote alivyovitenda duniani.

WANAOTUMIA HIRIZI ILI KUFANYA MAPENZI NA WANAWAKE WENGI
Bwana alinionyesha mwanaume aitwaye Kwame, ambaye alikuwa ni mwanachama wamambo ya kishetani.Alikuwa ana pete katika uume wake ambayo ilifanya iwezekane kuwaingiza makahaba kwenye chama hicho cha kishetani.kwa hiyo baada ya kulala na makahaba, huwaua kishirikina na kutumia sehemu za miili yao kama sadaka za kiuchawi kwa ajili ya watu wengine.

Nikaonyeshwa mwanaume mrefu, aliyekuwa na hirizi inayomuwezesha kutongoza wasichana kwa ajili ya kufanya nao ngono.Aliweza kufanya ngono na wasichana 1000 na alikuwa katika chuo kikuu cha Ghana,Legion,Accra.Alikwenda kuongeza ukubwa uume wake kwa kutumia uganga wa kienyeji na akapewa vitu avipande.Hayo mambo yamemsababisha awe kuzimu na aliwahi kuwa kiongozi wa vijana kanisani, na akafanya mapenzi na wasichana wengi kanisani hapo.

Baadaye nikaonyeshwa mchungaji/mwinjilisti aliyeitwa Francis ambaye alikuwa kanisa la Methodist.Alikwenda kwa waganga kujipatia hirizi itayomuwezesha kutokupingwa/kutokukataliwa jambo lolote atalolisema.Alikuwa akitongoza wasichana na hakuweza kumkatalia na  alikuwa pia shoga.

WANAOTUMIA HIRIZI KUPATA ILI WAPATE UMAARUFU NA FEDHA.
Nikamuona mwanadada ambaye alikuwa ni mtangazaji wa habari kutoka hapa Ghana kabla hajafa alikuwa akitumia make up alizopewa na mganga wa kienyeji kutoka India(Indian occultist).Na lengo lake ilikuwa ni kupata umaarufu,kibali na kupendwa na watu.Na alikuja kufa kwa ugonjwa wa kisukari na kujikuta yupo kuzimu kutokana na yale aliyoyatenda duniani.
WATUMISHI WANAOTUMIA NGUVU ZA GIZA.
Nikaonyeshwa wachungaji saba(7), ambao walikufa hapa Ghana, na wote walikuwa katika vyama vya siri vya Kishetani na walikuwa wakivaa kama hivyo,Waalikuwa wote manabii na walikuwa na pete za ajabu, ambazo walikuwa wakizitumia kufanya miujiza na kutabiri katika makanisa yao. 

Wote walikuwa wakilia kwa uchungu wako kuzimuni.Nikaonyeshwa muimbaji wa injili ambaye alishafariki Ghana, Naye alikuwa akisema ni mchungaji naye kumbe alienda kwa mpiga ramli wa kihindi(indian man) kwa ajili ya kupata msaada kwa ajili ya uimbaji wake.Alisema huyu mganga alimpa mafuta na uvumba wa kichawi ambao alitakiwa awe anauchoma pia alikuwa na pete ya kichawi yenye kumpa mamlaka ya kutoa kanda(album)nyingi za muziki.

Naye alikuwa akitakiwa kulala na wanawake, hivyo katika makanisa amelala na wanawake wengi sana.Kuzimu kulikuwa na funza wakali waliokuwa wakitoboa mwili wake kutoka kichwani hadi miguuni  yaani kila sehemu ya mwili wake na wakati huo huo moto mkali ulikuwa ukimuwakia na kumuunguza sana.Naye aliandikwa kwenye paji la uso wake namba 666.Nikamuona mtu aitwaye Abednego ambaye alifungwa nyororo shingoni mwote.Alipokuwa duniani alikuwa akitumia hirizi ambayo inamuwezesha kupotea sehemu yeyote yenye hatari/vifo.
Alikufa na sasa yupo kwenye moto wa kuzimu akiteseka.Niliona baadhi ya wa ghana wakivaa pete,dhahabu,siliva,chuma za tofauti tofauti na wote walikuwa wana chama wa vyama vya kishetani(wajenzi huru).
Nilionyeshwa waziri aliopita wa uchumi wa Ghana, ambaye alikuwa kuzimu kwa sababu ya kuwa mwanachama wa vyama vya siri vya kishetani(secret society), naye alipewa nguvu za giza zenye kumpa akili nzuri.
Nikamuona mchungaji kutoka ghana aliyeitwa Alfred ambaye alimtafuta malikia wa kishetani wa pwani(queen of the coast) kwa ajili ya kupata nguvu.Naye alikuwa na pete na kitambaa cheupe.Kitambaa kilikuwa ni kwa ajili ya uponyaji, na pete ilikuwa kwa ajili ya kutoa mapepo.Moto wa mateso yake ulikuwa mara saba zaidi ya wengine wote pale waliokuwa wakitumia hirizi.
Nikaonyeshwa mwanamke kutoka Naijeria aliyekuwa akitumia limbwata(charm) ili mume wake atapokufa yeye azirithi mali bahati mbaya huyu mwanamke alikufa na kujikuta ndani ya moto mkali wa kuzimu.
Bwana alinionyesha wanafunzi mbali mbali wakiwa na mabegi migongoni mwao.Kuanzia shule ya msingi, sekondari hadi chuo.Nao wanafunzi hao walienda kutafuta dawa(hirizi) kutoka kwa waganga wa kienyeji ili wafanye vizuri masomoni.Bahati mbaya hawakuweza kumaliza elimu zao na wakapatwa na mauti wote wakafa na kujikuta kuzimu.

Niliwaona pia baadhi ya wanafunzi kutoka katika shule marufu sana hapa Kumasi,Ghana.
Niliwaona madaktari(medical doctor) wengi wakiwa kuzimu, na mmoja wao anaitwa Dr.Frimpong ambaye aliponiona mimi alieleza kuwa yupo kuzimu  kwa sababu alipokuwa duniani alikuwa amejiunga na vyama vya siri vya kishetani na huko walipewa pete ili iweze kumlinda yeye.Naye alikufa kwa ajali na akajikuta yupo kuzimu iwakayo moto.
Niliwaona wanasheria wengi,mahakimu na majaji wote wakiungua motoni.Nao wote walikuwa sehemu ya vyama vya kishetani(secret societies) na wote walitafuta mashetani ili wapate ulinzi.Walikuwa na pete za kishetani zilizokuwa zinawalinda walipokuwa hai.
Nilionyeshwa binti ambaye mimi binafsi nilikuwa namfahamu kwani alikuwa akiishi Kwadaso, hapa Ghana.Naye alienda kwa waganga wa kienyeji ili aweze kupata wanaume wazuri.Naye alikufa kifo cha aibu baada ya hapo yupo kuzimu sasa anaungua moto kutokana na makosa yake aliyoyafanya.
Nikamuona mtu ambaye alikuwa anaitwa Budo ambaye alikuwaga Buokrom,Ghana.Alipokuwa duniani huyu mtu alikuwa ana nguvu sana mpaka polisi walikuwa wanamuogopa,alikuwa ana ulinzi wa kishetani na hizo nguvu zimefanya mwili wake kuwa kama chuma.Hivyo hata akipigwa risasi ilikuwa haingii mwilini mwake ila tuu inaweka alama, Alimuuzia shetani roho yake ili aweze kupata nguvu hizo.Huyu mtu pia yupo kuzimu motoni akiteseka na mapepo wanatumia mikuki ya moto(myekundu) kutoboa mwili wake na kuuchana chana.

Niliona makahaba ambao walikuwa wakikimbizwa na mapepo ndani ya moto na hao mapepo walikuwa wanawabaka hao mabinti ndani ya moto.Hao mabinti walienda kutafuta hirizi ili waweze kufanya biashara za kujiuza bila ya kudhurika au kuuwawa.Mmoja wao anaitwa Joana naye alisema “nilikuwa na nguvu ya kuyeyuka sehemu kama hiyo sehemu ina hatari”.Wanawake wote hawa walikuwa kuzimu kwenye moto wakiteseka kweli kweli.

Nilimuona mwanamke toka Ghana ambaye alikuwa anaitwa “Anti Afua”.Naye alikwenda kupata maji mtakatifu kwenye galoni kubwa kutoka kwa nabii ambaye alikuwa Ghana.Mwanamke huyo aliyafanya maji hayo kama mungu.Hayo maji yalikuwa ni ya kipepo na huyo dada alipokufa aliishia kuzimu.Nilimuona Frank ambaye alitokea Ghana.Naye alienda kupata kitambaa cha mkononi(handkerchief) kutoka kwa nabii, ili kwamba muda wote akijifutia usoni apate kibali.Alijipatia kibali kila alipokwenda ,na hiki kitambaa kilikuwa ni cha kipepo, alikufa akiwa na dambi hii na kuwa kuzimu akiungua moto.
Nikaona kwa mbali korongo na kulikuwa kama vile watu elfu kumi(10,000) wakiungua kwenye mlipuko wa moto mkali mfano wa uji uji.Mapepo yalikuwa yakiwacheka na kuwa kejeli wakisema “wote ninyi mmetumia pete zetu za maajabu”.Niliposogea karibu nikajua jina la mtu mmoja katika kundi hilo naye alikuwa akiitwa mchungaji Afriyie kutoka Ghana.Alisema alienda kupata pete ya uponyaji”.Kulikuwa na karibu wachungaji elfu mbili katika hilo eneo kwa wale waliokuwa wanatumia pete za maajabu kutoka kwa shetani.
Nao walikuwa ni kutoka nchi  mbali mbali duniani kote.Nikamuona kijana mmoja niliyekuwa namjua awali hapa Ghana na alifariki.Huyu kijana alikuwa mzuri wa sura na alipokuwa mzima alikuwa na marafiki wakike aliokuwa anatembea nao naye yupo kuzimu kwa sababu ya uzinzi.Niliona mkanda wa moto kiunoni mwake ambao mkanda huo ulikuwa unamuunguza yeye na kumkatakata.

Naye alijuta kwa nini alilkuwa duniani.
Niliona mapepo watano wakiwa na mabegi makubwa yaliyojaa kila aina ya fedha kutoka nchi mbali mbali na zilikuwa zimetolewa kwa wale walioingia mikataba na shetani ili wapate utajiri kwa masharti ya kuuza roho zao kwa shetani na watakufa baada ya muda.Kwa wale waliojiunga katika huu mfumo na mara tu utapojiunga unakuwa umeifungia roho yako kwenda kuzimu na mara utapokufa utajikuta kuzimu ndani ya moto.
Nalimuona mjumbe wa shetani akimwambia mtu kuwa ataishi miaka saba(7), lakini kiukweli  hiyo yaweza kugawanya kwa mbili na mtu afe baada tuu ya miaka mitatu na nusu na kujiunga kuzimu motoni.
Nilimuona mwanamke wa kinaijeria mwenye umri kama miaka 43 alikuwa motoni kwa sababu ya kutoa kafara damu zisizo na hatia.Alikuwa akiiba watoto hata wa umri wa mwezi kutoka mahospitalini ili kuwatumia katika makafara ya kishetani.Alikuwa akiweka watoto kwenye vinu na kuwatwanga mpaka kuwaua.

Ndipo huongeza mchanganiko wa manjano na kijani wa mafuta ya kichawi na anapochanganya tuu na hizo maiti za watoto wachanga ,Ghafla hugeuka mara  na kuwa fedha za kimarekani(US dollars) katika roho.Naye hufurahia na kusema hela hela!!!.
Kuzimu huyu mwanamke alikuwa akiteswa na mapepo watatu na wakimwambia “wewe,mwanamke mbaya,msifu shetani kwa kuwa hicho ndicho ulichokitenda duniani”.
Nikaona mwanamke ambaye duniani alilala na wanaume wengi na kila akilala na mwanaume hukusanya kondom walizotumia na kuchukua shahawa na kuziweka kwenye chombo na kupeleka kwa waganga ili kutoa kafara kwa ajili ya kupata fedha.

Huyu mwanamke alivyokufa alipelekwa kuzimu akiteswa ndani kwenye moto.
Kila roho iliyotenda hayo iko kwenye shimo kuzimu.Watu wa namna hiyo walikuwa kutoka nchi nyingi sana lakini mimi nilifanikiwa kuwaona kwa ukaribu  hawa wawili ambao walitokea Ghana.Mtu mmoja kutoka Naijeria alisema “MUNGU niokoe mimi”. Na sauti ikasema “ Si kukujua wewe”.Lusifa/Shetani akaja kwenye ile sehemu ya kuzimu na kucheka kwa kejeli na bila ya kujizuia.

MTOTO WA MALIKIA DIANA NA MICHAEL JACKSON
Nikaonyeshwa mtoto wa kike wa malikia Diana naalikuwa kuzimu kwa sababu ya uchawi,alipokuwa kuzimu alionekana kidogo kama ameharibika.Alikuwa na pete ya kishetani ya kujilinda aliyoipata India lakini cha ajabu pete hiyo ilishindwa kumuokoa usiku ule alipofariki.

Moja ya mtu niliyemuona kutoka kwenye makundi ya muziki alikuwa ni Maiko jackson.Alikuwa na pete la kishetani kutoka India kwenye mkononi mwake inayoweza kuita nguvu kubwa za shetani.Naye alisema “Nilikwenda kwa shetani kupata pete, inayonipa umaarufu na utajiri na sauti yangu kuwa kama ya malaika, Sasa nipo kuzimu nateseka milele bila KRISTO”.Na ni hii pete kutoka India iliyonipa umaarufu mkubwa na nilipata nguvu ya kuimba vyema.Alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wanatumia hirizi hapa duniani.

MUAMMAR GADDAFI NA MKUU SANI ABACHA WAKIWA KUZIMU
Nilionyeshwa aliyekuwa raisi wa zamani wa Naijeria aliyeitwa Sani Abacha katika sehemu huko kuzimu,ambako wengi wa viongozi wa dunia yote huenda huko.

Naye aliyesema “Nilisababisha vifo vya maelfu kwa maelfu kwa ajili ya kutoa kafara”.Na pia nilimuona Muammar Gaddafi aliyeuwawa na waasi nchini Libya.Muammar Gaddafi alisema “niko hapa kuzimu kwa sababu sikuamini katika YESU”.

Nilionyeshwa jinsi alivyoishi duniani, Alikuwa na mkufu wa maajabu uliokuwa unamsaidia kupotea popote hata kuwa kama upepo. Siku ambayo nguvu ya NATO na waasi walipomvamia hiyosiku alikuwa amesahau mkufu wake wa maajabu alioutoa kwa wakuu wa vyama vya kishetani kutoka India(occult grand master in India).Aliniambia niwaambie wa Libya,watoto wake na mkewe kugeukia Ukristo.Alisema yeye anateseka sana na wao kama hawatabadilika wote wataishia sehemu hii ya moto.Alizidi kusema kuwa hata wote walioniua mimi wasije mahali hapa.Akaniomba tone la maji.
WATU AMBAO WAKO NJIANI KUELEKEA KUZIMU.
Bwana alinionyesha watu ambao wanafanya manunuzi vitu mbali mbali na kuelekea kuzimu.Duka lilikuwepo Ghana,lakini maduka kama hayo yapo nchi mbalimbali duniani kote.Maduka hayo yanauza vitu mbalimbali vya kishetani vinavyotumiwa na waganga wa kienyeji na manabii wa uongo katika makinisa yao.Hivi vitu ni jumla ya nyekundu,nyeusi,majenta,dhambarau na mishushumaa ya kijani,mafuta mbali mbali ya kishetani,poda,maji, makofuli na vitu vingine vinavyotumiwa makanisani.Wanaonunua vitu hivyo vya kishetani wanatembea moja kwa moja kuelekea kuzimu.

Bwana YESU alinieleza kuwa muda wowote mtu anapopata hirizikwa ajili ya kufanyia chochote, huyo anakuwa amejiingiza kuzimu.Nikaona pepo kuzimu amebeba chombo kimejaa pete nyingi.Pepo akasema pete zote hizi wanapewa watu wanaojitafutia hirizi kwa ajili ya ulinzi,uponyaji,uroho,nguvu za giza, marifa na mengineyo.

Nilionyeshwa chupa nyingi na zingine walikuwa wanazichukua na kuleta duniani ili zitumiwe na watu wenye kutoa kwa wengine na hufunga roho zao kwenye chupa katika ulimwengu wa kiroho.Mtu yeyote anaye mloga mwenziye anakuwa mmoja na shetani naye ataishia kuzimu kwenye adhabu.Niliweza kuonyeshwa baadhi ya watu maarufu,watu wa mahakamani na hata wanasiasa wakiwa kwenye njia ya kuelekea kuzimu kwa sababu ya kutumia kwao kwa hirizi mbali mbali ili waweze kufanya vyema, kupata nafasi kubwa na kuwa maarufu.

Nilimuona muigizaji maarufu wa kike nchini Ghana ambaye aliweka hirizi katikati ya matiti yake ili aweze kuwavuta watu.Yeye na wengine wengi wanaotumia hirizi za namna hiyo wako njiani kuelekea kuzimu.Niliwaona waimbaji wengi wa injili na wamiziki ya kidunia waliokuwa wakielekea kuzimu kwa sababu ya kutumia hirizi ili kuimba na kutengeneza kanda(albums) zao.Nilimuona mtunisha misuli naye alikuwa akitumia kisehemu ya vitu vya kishetani fulani fulani katika mwili wake ili awe mwenye nguvu na ashinde medali nyingi zaidi.Wote hawa walikuwa njiani kuelekea kuzimu.

WACHEZA MPIRA
Nikaona mvulana wa miaka 12 ambaye alikuwa ni mcheza mpira.Nikauliza Bwana YESU kwa nini huyu yuko hapa kuzimu ,Naye Bwana akanijibu ni kwa ajili ya kushiriki katika nguvu za kishirikina.Mwalimu wake wa mpira alimuongoza kufanya matendo hayo ya kishirikina ili awe mcheza mpira mkubwa.Huyo kijana alipewa mafuta ya kishirikina ili ayapake mwilini kabla ya mchezo.
Nilimuona mchezaji kutoka Brazil naye alikwenda kwa wachawi ili asaidiwe kucheza ligi vizuri.Naye hakwenda kushukuru kwa hao wachawi baada ya ligi ndipo alipokufa siku akiwa na mechi nyingine.
Nilionyeshwa Marc-Vivien Foé, mcheza mpira mkamerooni ambaye alikufa katika mechi huko ufaransa mwaka 2003.Yeye alienda kwa Malikia wa kishetani wa nyika(Queen of the coast) kwa ajili ya kucheza vizuri kombe la Afrika(African Cup of Nations).Na baada ya kucheza kombe hilo alitakiwa kumtoa mama yake kama kafara naye alikataa.Ndipo hiyo siku roho za giza kutoka ufalme wa majini zikaja kumpiga  moyo wake pale pale na kumuua pale pale.Naye akajikuta kuzimu kwa kosa la kushiriki mambo ya ushirikina.Kuzimu nilimuona akibeba fuvu la mtu ndani ya moto.
WACHEZAJI NA WASHABIKI NJIANI KUELEKEA KUZIMU.
Nikaonyeshwa timu nyingi na mashabiki zake wakielekea kuzimu kupitia kwenye handaki.Timu ya kwanza niliyoiona ni Chelsea,nao walikuwa wakiongozwa na Ivanovic, na wakifuatiwa na wachezaji wengine katika mstari ulionyooka.Wote walikuwa na uvumba wa kishetani,mafuta ,pete za ajabu na vitu vingine vya kishetani.Nilionyeshwa jinsi gani wale wanaoshabikia hizi timu kutoka miyoni mwao wanavyoelekea kwenye tanuru la moto kuzimu.

Nilionyeshwa Ronaldino na watoto ambao umri wao ni kati ya 8 ha 13.Hawa watoto walikuwa wakijifuna kucheza kama yeye.Nikaona pepo la ajabu likatokea kwa umbao la ajabu ajabu mara linakuwa kama mwanamke, mara kama ngedere, na alikuwa ana mabawa kama popo.Huyo pepo alikuwa anamsaidia kucheza vyema.Kwa hiyo hao watoto walipokuwa wakijifunza kucheza kama Ronaldino, ndipo pepo hilo likajidhihirisha na kuwaingia wale watoto.Niliona yeye na wote mashabiki wake,wasaidizi na hao watoto wanaojaribu kumuiga kucheza kama yeye wanatembea kenye tanuru kuelekea kuzimu.

Mcheza mpira mwingine maarufu niliye muona naye alikuwa Kaka.Alikuwa na Bibilia mkono wa kulia na mpira kwenye mkono wa kushoto.Nikaona pepo limemfuata na kumwambia “nifuate na ntakuonyesha njia ya udanganyifu na uongo”.Huyo pepo alimbadilishia bibilia na kuiweka mkono wake wa kushoto na kumpa mpira mkono wa kulia kwake.

Kwa huzuni huyu pepoalikuwa akimuongoza kuzimu pia.Nikamuona mtu akimwambia ki Potugo(Portuguese) kuwa unaweza kuwa Mkristo lakini kila kitu unachokitaka kukifanya kwenye mpira nitafanya kwa ajili yako.Huyu mtu alikuwa akifanya kafara na mapepo yalikuwa yakitokea ,ndipo huweka mafuta kidogo kichwani na pepo kumuingia yeye.Ndipo anaanza kucheza vizuri.Nikaona wachezaji vijana wa kibrazili wote wanamfuata kelekea kuzimu.

Nikaonyeshwa baadhi ya watu waliokuwa wakitembea kimya kimya kuelekea kuzimu, na walikuwa ni timu ya Brazili.Nikamuuliza Bwana YESU, Nini walichokifanya naye YESU akanijibu ni kwa sababu ya kuabudu sanamu.Hii ni kwa sababu Mpira ni mungu na wale wanao wasaidia wanaishia kuzimu.

Nikamuona Pele amekwenda kwenye sehemu wanapozikia watu wengi(makaburini) usiku naye huita mapepo, Nayo mapepo huja kwa wachezaji na mafuta ya ajabu na kuwapaka na walitakiwa wasiguse mwanamke.Nikaona pepo la ajabu  na alikuwa na kichwa kama cha mtu lakini kiwili wili kama cha kondoo.Huyu pepo alikuwa akiongoza timu ukijumuisha na wachezaji wa zamani kama vile Pele na wengine.Nikaona wengi wa brazili wakimfuata kimya kimya kuelekea kuelekea kuzimu kwa sababu ya mapenzi makubwa na mpira.

Nikaona wachezaji wengi wanaotumia pete,mafuta maalumu ya kishetani,na vitu vingine vingi vya kishetani vilivyozoeleka kiasi kwamba kuonekana kuwa kama vile ni vifaa madhuti  kwa ajili ya kuchezea.Kitu cha kuhuzunisha ni hiki wachezaji wote na mashabiki wao wote wanaelekea moja kwa moja kuzimu.
Nikaona timu ya Ufaransa ikiongozwa na Zidane na wachezaji wengine wa zamani.Mashabiki wao na wapenzi wao wote walikuwa wanaelekea kuzimu baada ya hiyo nikaona timu ya taifa ya Misri ikiongozwa na Abutreka na wote walikuwa njiani kuelekea kuzimu.Timu ilikuwa inaongozwa na mapepo mawili yenye umbo kama ng`ombe.
Pepo mkubwa aliowasaidia kushinda kombe la Afrika (African cup of nations) mara saba alikuwa Osiris.
Nilionyeshwa  timu zote duniani ikiwemo na timu ya taifa ya Ghana,Maarufu kama Black stars ikifuatiwa na washabiki wake.Ndipo nikamuuliza Bwana YESU kwa nini iko hivyo, na Bwana YESU akaniambia ni kwasababu wote wanamilikiwa na adui na wamehusika katika matendo ya kishirikina.Bwana akaniambia Anawaonya hakuna ashirikiye matendo ya kishirikina atakaye ingia kwenye ufalme wangu.
Nikaonyeshwa klabu zote za mpira zipo katika viwango tofauti tofauti njiani kuelekea kuzimu kimya kimya ,wakifuatiwa na mashabiki wao kwa ukaribu sana.Vijana wote wadogo waliokuwa wakiwafuta wacheza mpira hawa wakubwa wote walikuwa wakiwafuata kwenda kuzimu.Baadhi ya hao vijana hawakwenda kwa hao waganga  wa kienyeji wenyewe bali walimu wao wa mpira na makocha wao ndio huwapa masharti yote ya kiganganga ya kufanya na ndio wanaowapeleka kwa ajili ya nguvu za giza ili kupata ushindi.

WAKRISTO NA MPIRA WA MIGUU
Nilionyeshwa timu mbili za kiKristo zikicheza mechi,na mapepo yakaja pale kwa muundo wa wanyama mkubwa na wakakaa na kuangalia mechi.Walikuwa na furaha na wakipunga.mapepo wengine pia walijitokeza kutokea chini ya kiwanja cha mpira na wakaanza kupindua matokeo kishetani kama vile wao ni makocha na hata wakristo walivyokuwa wakicheza hiyo mechi, mapepo walikuwa wanahaki ya kuwa pale kwa sababu mpira wa miguu ni mchezo ulioundwa na shetani ili kudanganya wengi waende kuzimu.
Nikaonyeshwa mechi mbali mbali za mpira za makanisani na nikaona mtu mmoja akaenda kumuona mganga wa kienyeji ili washinde mechi.Alipewa saa na muda wa kwenda makaburini  na kulala kutokea saa 6 usiku mpaka saa 12 asubuhi. Akaweka saa karibu na pembezoni mwa kanisa lililo kinyume nao ili waweze kushinda hiyo mechi.
Na timu ingine pia ikaenda kwa mganga wa kienyeji aliye wapa kimiminika cha ajabu alicho kinyunyiza kwenye jezi zao.Ndipo mapepo yalipokuwa yakiwatawala wachezaji hao.
WATU WENYE TATUU(TATTOOS)
Nikaona mvulana wa miaka 17 wa kimarekani aitwae Phillip.Huyu mvulana alikuwa na tatuu ya buibui(spider) kwenye mgongo wake.naye alisema rafiki yake alimwambia  yeye kuwa yaweza kumlinda kutopata magonjwa.Nikamuona shetani akimpita na kumkejeli.Huyu kijana alikuwa kanisani na alidhani ataenda mbinguni.Bahati mbaya huyu kijana yupo kuzimu sasa kwa sababu ya tatuu(tattoo).Shetani alisema “Wote wanaotumia tatuu(tattoos) wananitumikia mimi”.Nimeona wengi kwenye hiyo sehemu wapo kuzimu kwa sababu ya tattoo katika miili yao.
Nilimuona shetani akijigeuza yeye binafsi na kuwa mtu mdogo mwenye tatuu nyingi sana mwilini mwake,Alikuwa akiwatoboa ,akiwachana chana ndani ya moto na huku akiwakejeli kwa kunukuu Mambo ya walawi 19:28 “Msichanje chale yo yote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi Bwana”.
Kuzimu kuna vyuma vyekundu vinavyoshikizwa  kila sehemu ambapo mchoro wa tatuu umepita, na kunakuwa na maumivu makali sana.Nikamuona kijana mmoja aliyesema hakujua shida itayompata, yeye aliiga tuu kuchora tatuu kutoka kwa rafiki yake naye akafanya hivyo hivyo.Hata hivyo huyo kijana yupo kuzimu  na maumivu mengi kwa ajili ya kuchora tatuu.
WANAUME WANAOVAA HERENI
Nikasogea sehemu ile kidogo na nikaona kijana mdogo kwenye moto akiungua akiwa amevaa hereni masikioni.Alisema alikwenda kutafuta nguvu ya giza kwa ajili ya kutongoza wasichana.Alikuwa na pete aliyokuwa akiitumia kutongoza wanaume na wanawake ili afanye nao mapenzi.Wavulana na wanaume wengi  wanatumia hivyo vitu kutongoza wasichana ili kufanya nao mapenzi.Hiyo ni njia ingine ya kufanya ushirikina kwa sababu nguvu za giza huingia kwa wavulana na wanaume wanaofanya hivi maisha yao huongozwa kuhamasika tofauti na ilivyo kawaida.
VITABU VYA KISHETANI NA KIKRISTO.
Nilionyeshwa maktaba kuzimu na ilikuwa nyeusi na kulikuwa na mishushumaa myekundu,bluu na myeusi lakini ilikuwa ikiyeyuka ilivyokuwa ikiungua.Nikaona kitabu cha Momoni(Mormon), Vitabu vya utabiri wa nyota (astrology), Uchawi mweupe, bibilia ya kishetani, vitabu vya uumbwaji(books of evolution), Kitabu cha sita na cha saba cha Musa, bibilia ya Hip-hop, Kitabu cha mabadiliko na vitabu vingine ,baadhi vvilikuwa vikitumiwa na dini mbali mbali.Wote wanaotumia vitabu hivi huishia kuzimu.Nikaona pia vitabu vingi vya kikristo na shetani akisema roho yangu na nguvu yangu inaishi kwenye hivyo vitabu na kwa kitabu chochote ambacho hakina ROHO wa MUNGU.Shetani alisema pia kitabu chochote kinachopeleka watu kuzimu huwekwa kwenye hiyo maktaba ya kuzimu.Watu wanabidi wawe makini sana na vitabu wanavyosoma hata kama vikiwa na kichwa cha habari kinachoonyesha ni kitabu cha kikristo.
MAASKARI
Baada ya hayo nikatoka kwenye hicho chumba,nilipelekwa kwenye sehemu kuzimu ambako kuna maaskari.Hawa ni maaskari kutoka nchi mbalimbali duniani kote.Walikuwa katika dimbwi la moto.Hao walikwenda kwa waganga kutafuta nguvu za giza ili kujilinda na kupigwa risasi,na silaha zingine.Baadhi yao walikwenda kwa waganga wa kienyeji ili kupata nguvu za giza za kuyeyuka,wengine walikuwa na mavazi ambayo yametoka kwa shetani ili kuzuia risasi zisiwapate.
Walifanya kila aina ya maendo ya ushirikina walipokuwa duniani.kila mmoja wao alikuwa na namba 666 kwenye mapaji ya nyuso zao.
Kulikuwa na mapepo wakubwa aliokuwa akiwa garagaza na kuwapa mateso.Mapepo  yaliokuwa yanahusika kutoa mateso yalikuwa yana urfu wa futi 19naye alikuwa akionekana kama chura na macho matatu.nilimuona askari wa Ghana aliyekuwa na habari ya kusikitisha yeye alikuwa kwenye michezo ya ngumi(martial arts) na alipokufa mapepo yakamvuta mpaka kwenye hiyo sehemu kuzimu.Watu wengi hawajui kuwa michezo hiyo ina husisha na imani za kishetani,wale wanaocheza michezo hiyo ya martial arts hushia kuzimu.
WAVUTAJI
Na baadaye nikaomnyeshwa watu wawili(2) ambao wako kuzimu kwa sababu walikuwa ni wavutaji.Hivyo watu wanabidi waache kuvuta kwa kuwa kuvta kwa weza kukupeleka kuzimu.
WATU WANAO OMBA KWA WATAKATIFU
Nikaona mtu ambaye anaomba kwa majina ya watakatifu alipokuwa duniani.na vitendo hivi viwekwa kama ushirikina na mtu huyo alikuwa akipata mateso makubwa sana motoni .Baada ya hapo nilichukuliwa na kutolewa kuzimu kuja duniani.
SALA YA TOBA
Mpendwa Baba MUNGU uliye mbinguni, ninakuja kwako katika jina la YESUKRISTO.Nina kiri na kutambua kuwa ni mwenye dhambi zote, nisamehe dhambi zangu na maisha niliyoishi;Nahitaji msamaha wako.Naamini wewe YESUKRISTO ulimwaga damu yako pale msalabani kalivari na kufa kwa ajili ya dhambi zangu.Sasa niko tayari kugeuka kutoka kwenye dhambi.Umesema katika neno lako takatifu Warumi10:9 “Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.”
Sasa nakiri kuwa YESUKRISTO ni Bwana wa roho yangu,Kwa moyo wangu wote.Naamini kuwa MUNGU alimfufuaYESUKRISTO kutoka katika wafu.Wakati huu nakupokea YESUKRISTO kama mokozi wangu binafsi na kutokana na Neno lako hivi sasa nimeokolewa.Asante YESU kwa neema isiyopelekea lesni bali mar azote hupelekea kutubu.Bwana YESU badilisha maisha yangu ili nilete utukufu na heshima kwako pekee na sio kwangu.Asante YESU kwa kufa kwa ajili yangu na kunipa uzima wa milele.Amen

Shuhuda nyingine nyingi za ufunuo wa mbinguni na kuzimu waweza kuzipata kupitia mtandao ambao ni:WWW.JASIRIMBARIKIWA.BLOGSPOT.COM 




No comments :

Post a Comment

Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...