KANSA ZINAZOSABABISHWA NA KUSIKILIZA MUZIKI WA BONGO FLEVA


Watu wengi hawafahamu kuwa muziki wa kidunia una nafasi kubwa ya kuwaletea hatari katika maisha yao ya kiroho.




Tambua kuwa mambo ambayo yanatokea katika ulimwengu wa kimwili yanakuwa yameanza katika ulimwengu wa kiroho ,kwa hiyo ukiweza kuudhibiti ulimwengu wa kiroho ndio umeweza kuumeudhibiti ulimwengu wa kimwili.




Kabla ya kuainisha kansa zitokanazo na muziki wa kidunia kwanza pata kujua athari zinazotokea kutokea kutokana na kusikiliza muziki wa kidunia.
HATARI YA MUZIKI WA KIDUNIA KATIKA MAISHA YA KIROHO
Kuna madhara mengi yanayotokea katika maisha ya kiroho pale mtu anaposikiliza muziki wa kidunia.Baadhi ya madhara hayo ni pamoja na:-

1.UKIRI MBOVU  


Nyimbo zinapoimbwa baadaeKinywa kinanguvu sana na maneno mengi katika muziki wa kidunia yanakiri madhaifu, mfano muziki unaimba unasema “sisi tu masikini sana” Sasa unapoimba nyimbo kama hiyo inakufanya ukiri vitu ambavyo sivyema katika ulimwengu wa kiroho na kimwili pia kwa kuwa imeandikwa “Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.”-Mithali 18:21.


Kwa hiyo unapoimba “sisi tu masikini sana” unakuwa unautengeneza umasikini katika ulimwengu wa kiroho na si muda umasikini huo utakuja kujitokeza katika masha ya kimwili.
Mtu yeyote aliye hai kiroho hawezi kukiri au kusema sema hovyo hovyo kwa kuwa kwa kusema sema hovyo huko ndio kunapelekea hayo mambo kutokea katika maisha yake.

Mfano:Ukikiri “kushindwa”nawe utashindwa ,ukikiri “maisha magumu” na kweli kwako wewe yatakuwa maisha magumu hata kama yalitaka kuwa maraisi kwa kuwa shetani atashikilia uthibitisho wa neno lako ulilolisema.
Kwa hiyo kutokana na muziki wa dunia utajikuta kwenye hatari ya kujikuta ukiimba vitu visivyo na maana ukadhani inaishia hapo tuu,kumbe inakwenda kuathiri ulimwengu wako wa kiroho kwa kukiri vibaya baadhi ya mambo katika maisha yako tuu kwa sababu ya kufuatisha na kuziimba nyimbo za kidunia.

2.KUISHI KATIKA ULIMWENGU WA KUFIKIRIKA
Muziki wa kidunia unafanya watu wengi waishi katika ulimwenu wa kufikirika yaani ulimwenu usio halisi kwa kuwa nyimbo nyingi za kidunia huwa haziongelei maisha ya kawaida bali maisha ya kufikirika.
Kuazia anayeimba mpaka anaye kwenda kuusikiliza muziki wa dunia huwa wanajikuta wakiishi katika ulimwengu wa kufikirika yaani kuishi katika ulimwengu ambao si halisi.

3.KUPATANISHWA NA KUZIMU

Mara nyingi wasanii wanaoimba muziki wa kidunia huwa wanafanya mapatano na kuzimu ili wapewe nguvu katika kazi zao za muziki wa kidunia ili pindi zitokapo zifanikiwe sana kwa kusikika ,kupendwa na hata kukubalika. 

Kupitia muundo wa video za miziki ya kidunia kuna baadhi ya vitendo vyao katika mkanda(scene) vinakuunganisha na ushetani .mfano katika picha chini.


Hivyo kwa kusikiliza miziki ya kidunia unaweza jikuta ukipatanishwa na kuzimu kutokana na maagano husika juu ya miziki yao.
Pia mtu anaweza kuzidi kuungana nao hata kupitia style(maisha binafsi) mfano ni :-

        i.            Kupitia tattoo.

Imeandikwa “Msichanje chale yo yote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi Bwana.” Mambo ya Walawi 19:28.


Unapokuta baadhi ya waimbaji wa muziki wa kidunia wana michoro katika miili yao maarufu kama tattoo ni wazi kuwa wana maagano ya moja kwa moja na nguvu za giza juu ya kazi zao za muziki .

Sasa pale mtu mwingine anapoiga ile tattoo aliyekuwa nayo muimbaji flani wa muziki wa kidunia inamfanya naye aingie kwenye maagano ya kishetani pasipo kujijua.

      ii.            Kupitia ishara za vidole.

Kwa kusikiliza  muziki wa kidunia waweza jikuta unakutwa na hatari ya kuunganishwa  na kuzimu kw sababu ya kuiga au kufuatisha wanavyofanya waimbani wa muziki wa kidunia.

Ishara nyingi za vidole zinazotumiwa na waimbaji wengi wa muziki wa kidunia ni za kishetani na baadhi yao waimbaji hao wanajua moja kwa moja wanachokifanya.

 Imeandikwa "Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita (666)."-  --   Ufunuo wa Yohana 13:18

mfano wa chapa hii ya mnyama (damien/shetani) ni alama ya 666 ambyo inatumiwa kama ishara kwa njia ya vidole.

Ishara zingine wanazozionyesha waimbaji wengi wa kidunia ni kama mapozi bali si mapozi kwa kuwa zingine zina maana ya kumtukuza shetani.
Ishara zingine zinakuwa ni za kumsifu shetani kwa kuwapa mashabiki wengi ,kukubalika kwa muziki wa kidunia wanayoimba.

    iii.            Maneno.
“Kwa hiyo nawaarifu, ya kwamba hakuna mtu anenaye katika Roho wa Mungu. . . . . . . . . . . . .. . . ..”1 Wakorintho 12:3
Nataka nikuonyeshe tuu kuwa mtu yeyote anaponena anaweza kunena jambo kutokana na kuhamasika au kuamshwa na roho ,yaweza kuwa ni roho wa MUNGU au ni roho wa shetani.
Kama mtumishi wa MUNGU huwa kuna roho ya MUNGU husema kupitia mumishi huyo.

Je mtu tuu ambaye ni muimbaji wa muziki wa kidunia tuu anaimba baadhi ya nyimbo kupitia roho ya shetani,Yaani kupata awazo ya kishetani juu ya muziki wake naye kuyatimiza ili kuweza kufanikiwa.

4.KUWAKA TAMAA
Imeandikwa “Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu;” -Wakolosai 3:5



Video nyingi za muziki wa kidunia huwa na namna ambayo huamsha watu wanao zitazama hali ya kutamani wanawake,pombe na ngono.
Video hizo ambazo wasanii huvaa nusu uchi na kucheza kwa kuonyesha maungo yao ili tuu kutamanisha.


Mungu hapendi sisi kama wanawe tuwake tamaa zozote bali hupenda tuzishike sheria zae na tuzifuate. “Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.” 2 Timotheo 2:22
Hivyo basi kwa kuziangalia video za muziki wa kidunia mara nyingi unaweza kujikuta ukiwaka tamaa na kwa hiyo tamaa unakuwa umemkosea MUNGU na unapokuwa umemkosea MUNGU hapo ndipo ulinzi wa Mungu unaondoka maishani mwako na shetani kupata nafasi katika maisha yako.

Kwa hiyo ni bora kujiepusha kusikliza na kufuatilia muzki wa kidunia kwa kuwa unakufanya uwake tamaa ambazo mwishowe utaangamia kwa kuwa imeandikwa.Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.- 1 Yohana 2:17

5.KUMSIFU SHETANI PASIPO KUJIJUA
Unaweza kujikuta unamsifu shetani bila ya wewe mwenyewe kujijua kama unasikiliza na kufuatilia sana muziki wa kidunia.

Nyimbo nyingi za kidunia huonyesha majivuno,kusifu wanawake,pombe ,ngono na vinginevyo ambavyo vyote hivyo ni kazi ya shetani.


Nyimbo huhamasisha watu kwenda kinyume na maagizo ya MUNGU hivyo kufanya watu wengi wajikute wakimuabudu shetani pasipo wao wenyewe kujijua na mwishowe kuangamia.

KANSA TATU (3) ZINAZOTOKANA NA KUSIKILIZA SANA MUZIKI WA KIDUNIA
Kuna magonjwa matatu ya kiroho yanayotokana na mtu kusikiliza sana muziki wa kidunia.
kwa kuwa mtu asikilizapo huu muziki wa kidunia hujikuta akishindwa kwenda kanisani mara kwa mara akishindwa kusoma bibilia mara kwa mara ,atajikuta hata akishindwa kufanya maombi yake binafsi mara kwa mara.
Magonjwa makubwa ni :-

1.Kuwa na mahudhurio makubwa ya disco,matamasha na nighty club  kuliko kanisani.
Ugonjwa wa kwanza wa kiroho ni kujikuta una mahudhurio makubwa ya kwenda kwenye matamasha ,kujirusha ya muziki wa kidunia kuliko mikesha kanisani au maombi.

Utajikuta unapenda kwenda kwenye matamasha, kutokana na

 i.Mavazi
Kwa kuwa mtu huyu alikuwa akisikiliza sana muziki wa kidunia ataanza kuiga mavazi yake hivyo basi inapofika muda wa kwenda kanisani anajikuta hana vazi lolote linaloendana na kanisani hivyo kujikuta kuendelea kubakia kwenye utumwa wa kwenda disko na matamasha ya muziki wa kidunia.


ii.Styles
Maisha binafsi na muongozo wake unakuwa umebadilika na kuwa anawaza miziki yenye kuharibu maisha yake.Kwa mfano style ya nywele ya kunyoa kiduku au kama ni mwanaume ajikute amesuka,itamfanya azidi kupata sababu ya kutokwenda kanisani kutokana na style ya nywele zake haziendani na za wengine kanisani.

2.Kuvutiwa kusoma habari za udaku kuliko Bibilia(Neno la MUNGU).
Tatizo lingine linalotokana na kusikiliza sana muziki wa kidunia ni kujikuta ukifuatilia sana habari za wasanii ,yaani udaku kuliko kusoma Neno la MUNGU.

Kwa kuwa umeshazoea kuzisikiliza sana nyimbo za kidunia na majina yao una wajua hivyo itakufanya uwe makini kufuatilia mambo yoyote ya maisha yao yawe mabaya au mazuri lazima uwe unayafuatilia na kukufanya kusahau kabisa kusoma neno la MUNGU.

3.Kuweka hazina sana kwenye ngono,wanaume,wanawake kuliko MUNGU.
Imeandikwa “kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.”- Mathayo 6:21
Badala ya kuweka hazina katika kujitoa katika kazi za MUNGU kwa fedha au hata nguvu basi kwa wanaosikiliza sana muziki wa kidunia hujikuta wakiweka hazina zao kwa wanawake,ngono mdawa ya kulevya.
Hili ni gonjwa la kiroho linalotokana na kusikiliza muziki wa kidunia.

Muziki wa kidunia una athari nyingi nazo hutengenezwa kidogo kidogo kama vile ulikuwa hujui kunywa pombe unaanza kunywa kidogo kidogo,
ulikuwa huna tamaa za wanawake sasa waweza jikuta kutokana na video za muziki wa kidunia unaanza hamasika na kuwa na tamaa na wanawake.

Jiulize wewe mwenyewe kama mkristo unazo nyimbo ngapi za kidunia ,na unazo ngapi za kumsifu MUNGU ?.

Kama una nyimbo  nyingi za kidunia na chache za kumsifu MUNGU basi wewe tambua maisha yako ya kiroho yako kwenye hatari.

MAMBO YA KUFANYA ILI UONDOKANE NA TABIA MBAYA INAYOKUSUMBUA


Kuna vita kubwa kuacha tabia mbaya ambazo  hazimpendezi MUNGU.Tabia mbaya ambazo zimejiwekea mazoea katika maisha yetu mpaka zinakuwa na nguvu kana kwamba ni sehemu ya maisha yetu.

Imeandikwa “ Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohon i ”-1 Wakorintho 2:14

Watu wengi wanaokoka na kuanza maisha ya wokovu huku bado zile tabia zao zamani kabla hawajaokoa zinawafuatilia na kuwasumbua sumbua.

Mfano: labda mtu alikuwa mlevi sana kabla ya kuokoka basi  baada ya kuokoka anaweza kuwa anajikuta mara kwa mara anajaribiwa kurudia ile tabia ya kulewa.

Baadhi ya tabia sugu kwa watu wengi ambazo zinamchukiza MUNGU ni
ü  Ulevi

ü  Kusema uongo
ü  Kutukana matusi
ü  Kuangalia picha za uchi
ü  Kupiga punyeto/kujichua
ü  Uzinzi
ü  Uvivu
ü  Hasira
ü  Na n.k



Hakika kuna dawa ya kuacha tabia mbaya iliyokithiri yaani “addiction” na dawa pekee inayoweza kutatua ni uwepo wa MUNGU ambao huondoa kiu ya mambo machafu na kuweka kiu ya kutafuta mambo ya Rohoni zaidi.









Unapokuta mtu ameacha kwa kujilazimisha na kujizuia kimwili labda ilikuwa ni tabia ya kuvuta sigara na akaamua kuacha kwa kujilazimisha pasipo msaada wa MUNGU huyo anawezekana 

anaonekana kimwili kama ameacha lakini kiroho bado ile tabia anayo na ndio maana  mara nyingi anaweza jikuta akilala huwa anaota anavuta sigara pia watu kama hao hawakai sana wakiwa wameziacha tabia hizo bali si muda utasikia amezirudia tena na akizirudia anakuwa na kiu kubwa zaidi ya awali.

Imeandikwa “Kwa maana watu wa Mataifa wasio na sheria wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati, hao wasio na sheria wamekuwa sheria kwa nafsi zao wenyewe.” -Warumi 2:14

Ukweli ni kwamba uwepo wa MUNGU pekee ndio anaweza kukufutia kiu ya mazoea ya kutenda tabia mbaya.
Je huo udhihirisho wa MUNGU au uwepo wa MUNGU unapatikana vipi  ?.
Uwepo wa MUNGU unapatikana kwa kumuomba MUNGU mara kwa mara kwa kuwa uwepo huo huondoa kiu ya dhambi kabisa.

MAMBO YA KUFANYA ILI UONDOKANE NA TABIA MBAYA INAYOKUSUMBUA
Kila mtu anatabia fulani inayomsumbua ambayo anatamani imtoke ili azidi kuwa safi mbele za MUNGU na kuweza kumwabudu MUNGU katika roho na kweli,Yamkini  tabia ambayo wewe inakusumbua ni madawa ya kulevya,ulevi,uzinzi,pornography,kusengenya,kutukana,au kuhukumu watu.

Haya ni mambo unayotakiwa kuyafanya ili uondokane na tabia hizo :-
1.Kabla hujaitenda lazimisha kutaka uwepo wa MUNGU.
Pindi unapojisikia hamu ya kutenda ile tabia mbaya inayokusumbua labda ni kuvuta sigara,madawa ya kulevya au ni uzinzi ,

Basi wewe  jitahidi kabla ya kufanya hiyo tabia inayokusumbua  jitafutie sehemu ya siri labda ni chumbani na uombe kidogo tuu na ndipo utakapo shangaa kwa kuwa ukitoka utajikuta huna hamu tena ya kutenda ile tabia mbaya.

Mfano: Kunywa pombe, kuvuta sigara, kutumia madawa ya kulevya yaani tabia yoyote ambayo ni mbaya  badala ya kukimbilia kuitenda hiyi tabia ,Jiambie kama utani kuwa ngoja nika Sali kwanza ndipo nitakuja kifanya hiyo tabia mbaya hapo wewe nenda chumbani kwako sirini uombe MUNGU

uwepo huo unakufanya uisikie vizuri sauti ya MUNGU kupitia Roho mtakatifu.

Kila tabia mbaya yaani,uzinzi,uasherati ,tamaa mbaya,kuvuta sigara, madawa, kukasirika, kutukana, kunywa pombe, kusema uongo, 

kujichua au kupiga punyeto . . . . . . . . .tabia zote mbaya huwa zinapewa nguvu na roho za giza yaani mapepo ilizifanye kazi katika maisha yetu kwa hiyo unapokaribia uwepo wa MUNGU kwa njia ya maombi ya mara kwa mara baasi hayo mapepo yanayoleta  kiu ya kuendelea na tabia mbaya yanakimbia.

Na unapokuwa mbali na uwepo wa MUNGU basi mapepo yanaweza kupata nafasi ya kukuharibu kwa kukupa kiu na hamu kubwa ya kurudia ile tabia fulani mbaya uliyoiacha.


2.Mara kwa mara unahitajika kumuomba MUNGU juu ya tabia mbaya uliyo nayo  hata kama ulishamuomba.

Imeandikwa “ombeni bila kukoma;Ukweli” 1 Wathesalonike 5:17 .




Usiogope kuomba hata mara kumi(10) kwa siku juu ya tabia ikusumbuayo kwani ukweli ni kuwa mwanzoni nguvu hiyo inakuwa inafanania na chaji katika simu  ,kwa kuwa uwepo huo wa MUNGUunweza  kupungua na unaweza ungezaka ,

Uwepo huo unapopungua sana ndipo hujikuta unatamani kufanya na kuzirudia zile tabia mbaya za zamani ,hapo  ukurudi kumuomba MUGU tena kuhusu hiyo hiyo tabia na uwepo wa MUNGU unajichaji na kuongezeka kwako kukuondolea ile kiu ya dhambi.

Hatutakiwi kuacha kuomba kwa ajili ya tabia mbaya zitusumbuazo kwa kuwa tunapoomba MUNGU hushusha wingu lake ambao ndio uwepo na kwa huo unafukuza kila pepo wanaoleta kiu za kutenda zile tabia mbaya katika maisha yako.

 “Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.. .” Yakobo 5:16
3.Jitenge na mazingira yaliyo rafiki na tabia unayoikataa

Jitenge na mazingira ambayo yanaurafiki na tabia unayoipinga :Mfano labda unatumia madawa ya kulevya na umeamua  sasa unabidi uachane na kundi la marafiki wa aina hiyo kwa kutokaa karibu na mazingira yao.

Jiondoe kwenye mazungumzo na watu ambao wanakufanya ukumbuke ile tabia ambayo huipendi.Imeandikwa “Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.” 1 Wakorintho 15:33.

Jitahidi kukaa karibu na watu wanaokupa moyo wa kuiacha ile tabia mbaya na sio kukaa karibu na wanaokuchukia na kukucheka kwa uamuzi wako wa kuacha hiyo tabia mbaya.

4.Kiri na sema mara kwa mara kile tuu unachokipenda kitokee na sio unachokitenda.

Siku zote sema mimi nitaacha hii tabia mbaya inayonisumbua labda ya kuvuta sigara,ulevi nitaacha umalaya,nitaacha kuangalia picha za uchi(pornography),nitaacha kupiga punyeto(kujichua/ masturbation), 

kiwe chochote we sema tuu hata kama bado unaendelea na tabia hiyo tabia mbaya wewe endelea kusema tuu hata kama unasema huku ukiwa huna uhakika kama itakuwa rahisi hivyo.

Kuna nguvu kubwa katika vinywa vyetu  ingawa haionekani kwa macho.“Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.”-Mithali 18:21

Kuwa na hali ya kuongea kile unachotaka kitokee na sio kile unachokitenda ,kwa kuwa waweza kuwa unapenda sana uache hiyo tabia mbaya lakini unashindwa kujisemea kuwa nitaiacha kwa kuwa bado kila iitwapo leo unaitenda.

Imeandikwa  “Uuzuie ulimi wako na mabaya, Na midomo yako na kusema hila .”- Zaburi 34:13
Kwa kinywa chako kinaumba kitu katika ulimwengu wa kiroho ambao huja kutokea katika ulimwengu wa kimwili.Kwa hiyo ukiwa mara kwa mara bila kuchoka unajisemea “nitaiacha tuu tabia mbaya niliyo nayo”,au “ kuna siku nitakuja kuacha milele hii tabia mbaya kwa msaada wa MUNGU”,Kweli utashangaa siku utaacha kabisa na itakuwa shuhuda kubwa sana .imeandikwa“. . . . . . . . . . . . . . . .. . . . . . . . ; Ulimi wangu ni kalamu ya mwandishi mstadi.”-  Zaburi 45:1

“Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri; Bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu. “- Mithali 15:2

5.Usikate tamaa kumrudia MUNGU pale unapoanguka mara kwa mara.
Usije kata tamaa  kumuomba msamaha MUNGU mara kwa mara pale unapoanguka katika hiyo tabia mbaya.

MUNGU anapenda watu wote ila anachukia dhambi,kwa hiyo usione aibu kumwendea MUNGU kuomba msamaha kila unapoirudia ile tabia mbaya ambayo huipendi .



Kwa kuto kukata tamaa kwako  juu ya kumuomba msamaha MUNGU kila unapoitenda hiyo tabia yako mbaya,

Yeye MUNGU hutuma uwezo wake kwa neema yake ukusaidie kuacha hiyo tabia kwa kuwa anajua kuwa ukiacha hiyo tabia mbaya utaweza kumtumikia vyema na kwa ujasiri zaidi.

MUNGU hajali kuwa umeirudia ile tabia yako mbaya mara ngapi ,bali anajali umenyanyuka nakumrudia MUNGU kila ulipo itenda hiyo dhambi inayotokana na tabia yako.

Imeandikwa “ Kwa maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena; . . . . . . . . . . .” Mithali 24:16.

Kitu cha muhimu ni kwamba kila unapoanguka nakuirudia tabia yako mbaya hapo hapo rudi kwake MUNGU na kutubu kwa ajili ya hicho ulichotenda naye atakusamehe na kukupa nguvu ya kuacha hiyo tabia mbaya.     




Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...