Unapo
lala mwili unakuwa umekufa bali roho yako inakuwa hai sasa unachopaswa
kukijua ni kuwa aina za ndoto unazoota
zinaonyesha wewe uko vipi kiroho!.
Kwa
kuwa MUNGU hutumia ndoto kufikisha ujumbe wake kwetu ,Lakini pia shetani naye
hutumia ndoto kufikisha maharibifu yake kwa watu wasio na YESU kupitia ndoto.
Watu
wengi wameshindwa kuelewa ni nini MUNGU anasema katika maisha yao kwa kuwa tuu
hawaelewi pale MUNGU anapoongea na wao kwa njia ya ndoto kwa kuwa hawawezi kutafsiri
kile wanachokiota.
Ndoto
ni moja wapo ya njia ambazo MUNGU
hutumia kuongea na watu wake.Muda mwingine ndoto zinakuwa hazina mafumbo ,Mfano
ni huu
Imeandikwa “Lakini
Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto ya usiku, akamwambia, Umekuwa mfu wewe kwa
sababu ya mwanamke huyu uliyemtwaa, maana ni mkewe mtu.” -Mwanzo 20:3.
Hiyo ndoto ilikuwa haihitaji tafsiri yeyote kwa
kuwa haina mafumbo yoyote na ilikuwa
wazi sana kwa Abimaleki. Lakini kuna ndoto zenye mafumbo tena makubwa sana na
hizo ndizo tunazo jifunza namna ya kutafsiri ndoto hizo!.
Hivyo
basi yatupasa kujua namna ya kutafsiri mafumbo hayo ili tuweze kupata ujumbe
ambao MUNGU ametutakia.
Kama hauoti ndoto unahitaji kuombewa maombi ya
ukombozi na kama unaota ndoto na huelewi maana ya ndoto uliyoota pia unahitaji
maombezi.
Ukisoma
neno la MUNGU(biblia Takatifu) linaonyesha wazi kuwa hakuna aliyemjua MUNGU
ambaye alishindwa kutafsiri ndoto,iwe ni ndoto yake au za wengine.
Mfano: “Akaota tena ndoto nyingine, akawaambia ndugu
zake, akasema, Angalieni, nimeota ndoto nyingine; na tazama, jua na mwezi na
nyota kumi na moja zikaniinamia.”- Mwanzo 37:9
Hiyo
ni ndoto ambayo Yusufu aliiota na hiyo Ndoto ipo katika mafumbo lakini baba
yake aliweza kugundua maana halisi ya ndoto ile “. . . . . . . . . baba yake akamkemea
akamwambia, Ni ndoto gani hii uliyoiota? Je! Mimi na mama yako na ndugu zako
tutakuja tukusujudie hata nchi?” -Mwanzo 37:10.
Hii inamaanisha kuto-ota Ndoto
ni tatizo bali si hivyo tuu bali pia na ukii ota ndoto na kuto kuelewa ni
tatizo zaidi.
Vigezo
pekee vitavyokuwezesha kutafsiri ndoto ya aina yeyote ile navyo ni hivi:-
1.Uwe na ROHO mtakatifu
Imeandikwa “Wakamwambia,
Tumeota ndoto wala hapana awezaye kuifasiri. Yusufu akawaambia, Kufasiri si
kazi ya Mungu? Tafadhalini mniambie” -Mwanzo 10:8.
ROHO mtakatifu
hanunuliwi bali anakuwa ndani ya mtu yeyote aliyemkubali YESUKRISTO kuwa mokozi
wa maisha yake.
Unapomkiri YESU na kukubali kila alichokisema basi yeye YESU
huweka msaidizi ndani yako naye atakuwa akikuongoza na kukusaidia katika mambo
mengi na mengineyo ni kama haya ya kutafsiri ndoto.
Imeandikwa “kwa kuwa roho njema kupita
kiasi, na maarifa, na ufahamu, na uwezo wa kufasiri ndoto, na kufunua maneno ya
fumbo, na kufungua mafundo, zilionekana katika Danieli huyo, ambaye mfalme
alimwita Belteshaza. Basi na aitwe Danieli, naye ataionyesha tafsiri.”- Danieli
5:12
Ndoto
zote ROHO mtakatifu ndio siri pekee mwenye uwezo wa kuzitafsiri ndoto hizo
tokea enzi na enzi.Hatutakiwi kutafsiri ndoto kwa kukariri bali kwa uongozi wa
ROHO wa MUNGU.
2.Uwe na ushirika na MUNGU
Kigezo
cha muhimu unachotakiwa uwe nacho ni kuwa mtu mwenye ushirika wa mara kwa mara
na MUNGU.Kwa kuwa kwa kufanya hivyo MUNGU huongeza nguvu ya udhihirisho wa ROHO
wake mtakatifu.
Angalia
watu wote wenye uwezo mzuri wa katafsiri ndoto huwa wanaushirika mkubwa na
MUNGU. Mfano Danieli yeye alikuwa akiomba MUNGU mara tatu(3) kwa siku,utaona
ni jinsi gani alivyokuwa na ushirika mkubwa na MUNGU.
Na ndio maana alikuwa na uwezo
mkubwa wa kufasiri ndoto.
“Hata Danieli, . .
. . . .. . . . . . . akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru
mbele za Mungu wake, kama
alivyokuwa akifanya tokea hapo.” -Danieli 6:10
Kuna hatua sita (6) zitakazo
kuwezesha kutafsiri ndoto yako.
1.Changanua chanzo cha Ndoto yako
Kipengele
muhimu kuliko vyote ni hiki kwa kuwa ukikijua baasi hakuna ndoto utakayoshinwa
kuifasiri.
Ukitaka
kutafsiri ndoto yako jaribu kuchanganua hiyo ndoto iko kwenye kundi lipi la
vyanzo vyake.
Kwa kuwa kuna makundi matatu ya ndoto na vyanzo vyake ambavyo ni:-
I.Ndoto itokayo kwa MUNGU
Hizi
ni ndoto rasmi ambazo huja na amani kuleta ujumbe kutoka kwa MUNGU juu yako au ya
wengine kwa ajili ya kuwaombea au kuwasaidia
.
Mfano:Unaota rafiki yako anauwa sana . . . . Kama una YESU hii ndoto inakutahadharisha
kuwa umuombee huyo rafiki kwa kuwa anaweza akaumwa siku si nyingi.Na unapo
muombea kweli hawezi tena kuumwa.
II.Ndoto itokanayo na MTU yaani mawazo yake.
Hizi
ni ndoto zinazotokana na mawazo ya mtu
mwenyewe yaani mawazo mengi yanaomsumbua sana hukaa katika ubongo na baadae
hujikuta akiyaota.
.
Mfano:Wewe umeota umepata fedha nyingi
sana,Lakini kabla hujaota hiyo ndoto siku yako nzima uliitumia kuwaza ni namna
gani utaweza kupata pesa nyingi.
Hivyo basi ujue tuu hiyo ndoto ni ndoto iliyotokana na
WEWE mwenyewe kwa kuwa mawazo yako mengi ya kuwaza jinsi ya kupata pesa ndio
yamesababishia kupata ndoto ambayo inahusu fedha.
III.Ndoto itokanayo na shetani.
Ndoto
ambazo chazo chake ni shetani ,mara nyingi ndoto hizi huwatokea watu wengi
ambao hawajaokoka au hawajakaa vizuri na MUNGU wa kweli..
Mfano wa ndoto hizi:kuota unakula nyama
za watu, kuota unauwa, kuota unafanya mapenzi , kuota unapaa,kuota unaongea au
uko karibu na watu waliokwisha kufa zamani, kuota uko uchi ,kuota umewekwa
kwenye jeneza,n.k.
Ndoto za namna hiyo zinakuwa zimetoka moja
kwa moja kutoka kwenye ufalme wa giza(shetani) na zinakuwa na madhara kwetu .
kwa
mfano:mtu anayeota
anakutana au anaongea na mtu aliyekwisha kufa siku nyingi hizi ndoto humsababishia kifo yeye yaani roho
ya mauti inakuwa ilishamuingia ndio
maana anaota watu waliokufa siku nyingi.
Zingine kama kuota unakula nyama za watu hizi humfanya
mtu awe na mikosi yaani balaa ,unapokula vyakula vyao ndotoni wao hupanda bati
mbaya na majanga katika maisha yako.
Kuota uko uchi ni ndoto ambazo husababisha aibu kubwa
kuja kukutokea katika ulimwengu wa mwili.
Kuota unafanya mapenzi ndotoni,ndoto hizi husimamiwa
na majini mahaba na unapoota mara kwa mara hizi ndoto husababisha kukosa mtoto,kutokuwa
na mahusiano yeyote yaani kama upo kwenye ndoa au uchumba basi kutaanza
migogoro isiyoeleweka mpaka mtaachana pia
ndoto hizi husababisha bahati mbaya mara zote katika maisha yako yaani
kuna kuwa na ugumu mkubwa hata kushindwa kufanikiwa.
Kuota
unapaa paa angani au hewani hizo ni
ndoto ambazo wachawi wanatumia sura yako kufanya uchawi wao kwa wengine. –Kuwa makini sana na ndoto kwa kuwa
muda mwingine shetani anaweza kutumia sura ya mtu mwingine unayemjua na kumuona
huyo mtu kwenye ndoto akikujia na kukufanyia jambo baya ili tuu uanze ugombane
naye ukidhani ni mchawi
kumbe sio kwa kuwa naye anatumiwa na wachawi bila yeye mwenyewe kujijua.
Kuota
mara kwa mara unaogelea kwenye ziwa au maji yeyote ujue hizo ndoto ni za
kishetani zinazo sababisha kuto kuolewa,kukosa mtoto na kushindwa kuridhika na
mahusiano ya kimapenzi ulio nayo .Kwa hiyo hupelekea watu kuachana,ndoa
kuvunjika au kukaa pasipo amani siku zote.
Unapoota ndoto kama hizi ni bora tuu ufanye mpango wa
kuombewa na watumishi sahihi ambao wana nguvu ya MUNGU kwa kuwa ndoto hizi ni hatari sana kwa kuwa
kila unapoota ndoto kama hizi shetani anakuwa amepanda mambo mabaya katika
maisha yako.
Na ni YESU pekee ambaye anaweza kukuokoa na
mitego hiyo ya shetani kupitia ndoto.Watu wengi hawafanikiwi si kwa sababu
hawafanyi kazi kwa bidii bali kwa sababu ya ndoto hizi za shetani husababisha
mikosi na bahati mbaya na hasara katika maisha yao.
2.IANDIKE NDOTO YAKO.
Ukisha
ota ndoto na ukawa huielewi hapo hapo iandike na kwa kuwa utakuwa umeshaijua
imetoka katika chanzo gani ?
Kama
chazo cha ndoto yako ni cha WEWE mwenyewe yaani unajijua jana ulikuwa unawaza
sana kuhusu jambo fulani na leo umeliota jambo hilo ujue hiyo ndoto chazo chake
ni mawazo yako mwenyewe kwa hiyo iachilie mbali kwa kuwa haikusaidii.
Kama
imetoka kwa shetani fanya maombi mazito ya kutoa hiyo silaha iliyopandwa katika
maisha yako katika jina la YESU.Au nenda kwa watu wa MUNGU ambao wana nguvu ya
MUNGU nao watakuombea na utakuwa huru na mapando ya shetani.
Kama
hiyo ndoto imetoka kwa MUNGU basi iandike vizuri ukifuatisha hatua kwa hatua.
Imeandikwa “Katika
mwaka wa kwanza wa Belshaza, mfalme wa Babeli, Danieli aliona ndoto, na maono
ya kichwa chake, kitandani mwake; basi akaiandika ndoto, akatoa habari ya jumla
ya mambo hayo.”- Daniel 7:1
Watu
wote wanaoweza kutafsiri ndoto zao na kupokea jumbe zao kutoka kwa MUNGU
walikuwa ni watu wenye kuheshimu maono na ndoto wanazozipata na hata
kuziandika.
Imeandikwa “Kwa malaika wa kanisa lililoko
Efeso andika; Haya ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono
wake wa kuume, yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu.” -Ufunuo
wa Yohana 2:1,
3.ICHUNGUZE NDOTO YAKO NA OMBA
KWA AJILI YA NDOTO YAKO.
Hatua
ya tatu(#3) ichunguze ndoto yako,kwa idadi ya watu au vitu na uombe kwa ajili
ya hiyo ndoto.
Cha
kujiuliza jiulize kwa nini MUNGU ameruhusu nione haya maono au hii ndoto?,
Imeandikwa “Ni
utukufu wa Mungu kuficha jambo; Bali ni utukufu wa mfalme kuchunguza jambo.” -
Mithali25:2
Kumbuka
baadhi ya ndoto ni kukufariji,kukutia moyo ,zingine kukuonyesha njia ya kupita
lakini pia kuna ndoto ambazo ROHO mtakatifu anakuhitaji wewe usimame kwa nafasi
yako kama kuhani.
Wakristo
wengi wamekua wakiwaota watumishi wakubwa na mababa zao wa kiroho wakifanya
mambo maovu huwa wanajiuliza inamaana gani?,
Nataka
nikujuze sasa.Kwa kuwa MUNGU si mmbeya au mpenda udaku mpaka akufunulie siri za
watu wengine .MUNGU hufichulia siri hizo ili uwaombee na niwewe pekee unaeweza
kuwaombea watu haowakawa salama.
Kumbuka
tunategemeana katika KRISTO YESU hivyo unapoonyeshwa mambo mabaya ya watu
wengine unatakiwa uwaombee na sio kwa ajili ya wewe kuwasema sema vibaya.
Uwaombee
tena kwa kufunga na kwa sadaka ili uwakomboe wale wanao pitia matatizo.Kwa kuwa
kwa kuombea wengine kuna thawabu kubwa sana kwako unapata.
4.ITAZAMIE NDOTO YAKO & IISHI
NDOTO NA UFUATISHE UJUMBE WAKO.
Angalia
ndoto yako ambayo imeleta ujumbe kutoka kwa MUNGU na uanze kuifuatisha kwa kuwa
nisauti ya MUNGU.
Imeandikwa
“Paulo akatokewa na maono usiku; alimwona mtu
wa Makedonia amesimama, akimsihi, na kumwambia, Vuka, uje Makedonia utusaidie.
10 Basi alipokwisha kuyaona yale maono, mara
tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa tuliona hakika ya kwamba Mungu
ametuita tuwahubiri Habari Njema.
11 Basi tukang'oa nanga kutoka Troa, tukafika
Samothrake kwa tanga moja, na siku ya pili tukafika Neapoli;
12 na kutoka hapo tukafika Filipi, mji wa
Makedonia, mji ulio mkuu katika jimbo lile, mahali walipohamia Warumi; tukawa
katika mji huu, tukikaa siku kadha wa kadha.”- Matendo ya mitume 16:9-12
Hii
inaonyesha kuwa ukiona ujumbe wa MUNGU unakwambia endelea mbele basi nawe pia
unatakiwa uendelee mbele hata kama unadhani kukaa ni sahihi zaidi.Kwa kuwa
MUNGU hujua mambo mengi tusiyoyajua.
Imeandikwa “Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema,
Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa
uweza wa Roho Mtakatifu”- Mathayo
1:20
Imeandikwa “Naye Yusufu
alipoamka katika usingizi, alifanya kama malaika wa Bwana alivyomwagiza;
akamchukua mkewe;”- Mathayo 1:24
Hii inatuambia kuwa natupasa kutii sauti ya MUNGU kupitia ndoto.Yaani
tuishi na kuenenda sawa sawa na ndoto ya MUNGU inavyotuelekeza.
Haitoshi tuu kutafsiri ndoto tuu bila kuchukulia hatua ya kuitendea kazi
kwa kuwa ndoto ni ujumbe wa MUNGU.
Kumbuka ndoto ni bayana , kwa hiyo usipuuze uyaotayo