Watu wengi
wanamwabudu MUNGU lakini hawawezi kumsikia MUNGU na pengine hawajui anachokisema
kwao kuhusu mambo mbalimbali ya maisha yao. Sasa utajifunza au jinsi gani ya
kumsikiliza MUNGU anapo nena nawe.
Watu
wengi hujiuliza kwanini MUNGU asiongee nasi kwa wazi wazi na kama sisi nasi tunavyowasiliana na
wanadamu wenzetu na kuelewana ?.
Yawezekana nawe pia huwa unajiuliza swali
hilo hilo ,Jibu ni hili: Imeandikwa hivi “Mungu ni Roho, ………………….” -Yohana 4:24,Jibu ni kwamba MUNGU wetu ni
ROHO kama unavyojua ROHO haionekani kwa
macho ya nyama bali ni macho ya KIROHO ,na ROHO haiongei ukasikia kwa
masikio haya ya mwilini bali yale masikio ya KIROHO.Hivyo ndiyo maana inakuwa
si kawaida kumsikiliza MUNGU wazi wazi kama unavyo ongea na mwanadamu mwenzio.
Ukweli ni huu kuhusu
kumsikiliza MUNGU kuwa kuna siri.Siri ni hii ya kuwa
Kama ilivyo katika maisha ya kawaida ilivyo ngumu kuongea na mtoto mchanga naye
mpaka akakuelewa nawe ukamuelewa ndivyo ilivyo katika habari ya kumsikiliza
MUNGU.
Hii inamaanisha jinsi
unavyokuwa kiroho zaidi ndiyo una nafasi kubwa na nzuri zaidi ya kumsikiliza
MUNGU kuliko wale ambao bado ni wachanga wa kiroho.
Kumbuka tena siri
kubwa ni hii kuwa “Kama wewe unavyopata shida
kumsikiliza na kumuelewa mtoto mdogo au jinsi ilivyoshida
kumuelezea/kumuelewesha kitu fulani
mtoto mchanga ndivyo ilivyo katika mambo ya kumskiliza na kumuelewa MUNGU”.
Hii
inamaanisha katika kumsikiliza MUNGU kuna viwango tofauti tofati kulingana na
jinsi ambavyo umekua KIROHO kiasi gani.
Mtu ambaye ni mchanga
kiroho hivyo hivyo naye MUNGU huongea naye kichanga changa .
Kama ilivyo ki
kawaida kuwa huwezi kutaka kujadiliana na mtoto mchanga ili akushauri kuhusu
jambo lolote bali utacheza cheza naye tuu kwa kuwa ni mchanga na hawezi kuelewa
mambo makubwa.
Kwa
mtu ambaye ni mkubwa kiroho yaani amekomaa kiroho huyo MUNGU huongea naye
ki-utu uzima tena hujadiliana naye kwa kuwa ana kiwango kikubwa.
Watu wengi hudhani
kuokoka na kukaa muda mrefu katika wokovu ndio ukomavu au ndio kukuwa kwenyewe
KIROHO,Lakini Hasha ! si hivyo hata
kidogo bali ukuaji wa mtu kiroho hupimwa na MUNGU mwenyewe naye huangalia vitu
vingi sana ambayo waweza kujumisha yote kwa kusema tuu kuwa hupima uaminifu
wako katika mambo yake.
Hivyo
basi ukitaka kusikia sauti ya MUNGU kwa undani sana na kwa uwazi sana unatakiwa
ujitahidi ukuwe KIROHO naye MUNGU atasema nawe kwa uwazi zaidi.
MUNGU huongea na watu kupitia njia mbalimbali kutegemeana
na kiwango cha kiroho ambacho mtu huyo amefikia.
Baadhi ya njia ambazo MUNGU hutumia kusema
na watu
Kuna njia mbali mbali
ambazo MUNGU hutumia kuongea na watu naye MUNGU hutumia njia hizo kwa
watukutokana na viwango vyao vya KIROHO.Njia hizo baadhi zao ni :-
1.MUNGU huongea kupitia (Bibilia)NENO LA MUNGU.
Hii ni njia KUU , ya MSINGI na ya PEKEE
ambayo watu wengi ambao hawajakuwa kiroho na wengine ambao wamekuwa kiroho
,MUNGU hutumia kusema nao kwa njia ya neno lake.
Imeandikwa “Hapo mwanzo kulikuwako Neno,
naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.”- Yohana 1:1-2.
Unaposoma neno la MUNGU huku ukiongozwa na ROHO
mtakatifu ujue kabisa hapo unamsikiliza MUNGU mwenyewe !.Tunapaswa kujua kuwa
kwa njia ya ROHO mtakatifu BIBILIA ina kila sauti ya kutusaidia katika maisha
yetu !.
Imeandikwa-“Yesu akajibu, akawaambia, Mwapotea, kwa
kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu.”- Mathayo 22:29. Hii inamaanisha kwenye maandiko kuna sauti ya kila
jambo yaani jambo la sasa na la yajayo ambayo itakufanya usipotee hata kidogo.
NAMNA YA KUENENDA :Soma BIBILIA yako kwa makini sana
huku ukiwa umekwisha mualika ROHO mtakatifu ili akuongoze na unapoisoma
tafakari ukifananisha neno la BIBILIA ulilolisoma na kitu unachotaka ndipo
utapata namna ya kuenenda katika kitu ulichokuwa ukikitakia sauti kutoka kwa
BWANA.
Ifuatishe sauti hiyo kwa kuwa katika hiyo kuna wokovu.
2.MUNGU huongea kupitia watu wanaokuzunguka.
Njia hii hutumiwa
sana na MUNGU, yaani njia ya kuachilia sauti YAKE kwa watu wake.
Mara nyingi njia hii
MUNGU huitumia kwa wale ambao wameanza kukuwa kidogo kiroho. Imeandikwa “Na shauri lake Ahithofeli, alilokuwa akilitoa siku
zile, lilikuwa kama mtu aulizapo kwa neno la Mungu; ndivyo yalivyokuwa mashauri yote ya Ahithofeli, kwa Daudi, na kwa
Absalomu.”- 2 Samweli 16:23
Umesoma huo mstari
kwamba mtu alipokuwa akishauriwa na Ahithofeli ilikuwa ni kama vile MUNGU
mwenyewe anamshauri mtu.
Kuna
watu ambao MUNGU amewajaza hekima na maneno yake kiasi kwamba kwa kila jambo
ambalo unapitia katika maisha yako wao wanakuwa wana jua kabisa sauti ya MUNGU
kwa ajili yako.
Wewe unapomuomba
MUNGU jambo fulani mfano unamuomba MUNGU
akupe kazi na baada ya kuomba MUNGU ukashangaa tuu ukakutana na mtu ambae
hujawahi kumwambia kuwa unatafuta kazi na anakwambia namna ya kupata kazi, wewe
hapo tambua ni MUNGU mwenyewe anamtumia huyo mtu kuongea nawe kwa habari ya
kupata kazi ambako ulikuwa ukimuomba.
Unapomuomba MUNGU
jambo fulani au unataka kusikia sauti ya MUNGU kwa habari ya jambo fulani na
sii muda ukakutana na mtu ambaye hajui shida yako akawa anayazungumzia yale
ambayo ulikuwa ukimuomba au akitaka kuyajua hapo ujue ni MUNGU mwenyewe
anaongea nawe kupitia mtu huyo!.
3. MUNGU huongea kupitia matukio ya
HALI mbalimbali YENYE ishara.
Hii ni ngazi kubwa
zaidi ya kumsikiliza MUNGU ambayo ukitaka kusikia sauti ya MUNGU kwa viwango
hivyo unabidi uwe umekua zaidi KIROHO.
Ngazi hii inayohitaji uwe na uhusiano
yaani ukaribu mkubwa na MUNGU ukisaidiwa na ROHO wake mtakatifu.
MUNGU anaweza kuzungumza kwa kutumia tukio
lolote au kutumia mnyama wa aina yeyote na pasipo kujali hali au mali.
ROHO mtakatifu anahisia ambazo zinaelezea
hali ya mambo ya kiroho nayo huathiri mtu kama mtu huyo akiwa na uhusiano
mkubwa naye huyo ROHO.
Imeandikwa “Saa ile ile alishangilia kwa Roho Mtakatifu, akasema, Nakushukuru, …………………………………..” -Luka 10:21.
Umeona
kwa ROHO mtakatifu waweza kukaa na
furaha zaidi na furaha hii isiyo ya kawaida.
Imeandikwa “Na wanafunzi walijaa furaha na Roho Mtakatifu.”- Matendo ya Mitume 13:52
Inahitaji umakini kwa
kuwa watu wengi huwa MUNGU huongea nao kupitia ROHO mtakatifu lakini wao huwa
hawasikii neno lolote kutoka kwao,
Imeandikwa “Na Roho Mtakatifu naye amshuhudia; kwa maana, baada ya
kusema,”- Waebrania 10:15
Mfano: Unaomba MUNGU
labda kuhusu safari yako na unataka kujua kama kweli MUNGU amekuruhusu kwenda itakuwa
salama au usubiri kidogo !.
Sasa baada ya
kumuomba MUNGU ukajikuta una Amani moyoni mwako yaani AMANI ISIYO YA KAWAIDA
ambayo hukuwa nayo kabla ya kuomba ,ujue MUNGU anakutaarifu kupitia ROHO wake
mtakatifu kuwa hakuna shida katika safari yako.
Na pengine baada ya
kuomba ukajikuta unahuzuni au hofu kubwa iliyokujia baada ya kuomba yaani hujawa
nayo kabla ya kuomba lakini baada ya kuomba ndiyo huzuni hiyo ikakujia ujue
MUNGU anakutaarifu jambo sio zuri katika safari yako hivyo ROHO mtakatifu
hupasha hisia kwa nguvu ya MUNGU ambayo inasauti kabisa na hutoa maelekezo
namna ya kufanya ,inaweza kukwambia usubiri kidogo au usiende kabisa ya
tegemeana.
Angalizo kuu ni kwamba njia hii MUNGU hitumia kwa watu
waliokwisha kukomaa kiroho yaani sio watu ambao ni wachanga bali ni wale ambao wanauelewa
mkubwa wa mambo ya MUNGU.
Hisia zinaweza kuwa
kusisimka nywele kupita kiasi ambayo mara nyingi humaanisha kuna hatari hiyo
sehemu au kuna mvutano kati ya nguvu za MUNGU na za shetani,
Yaweza kuwa
amani isiyokuwa ya kawaida,furaha,huzuni
isiyokuwa ya kwaida …. Na n.k
Kikubwa ni hiki njia hii MUNGU huitumia kwa wale watu
waliokuwa wamekomaa kiroho ambao wana uwezo mkubwa wa kupambanua jema na baya.
4.MUNGU huongea kupitia NDOTO .
Imeandikwa “Lakini Mungu akamjia Abimeleki
katika ndoto ya usiku, akamwambia, Umekuwa mfu wewe kwa sababu ya mwanamke huyu
uliyemtwaa, maana ni mkewe mtu.”- Mwanzo 20:3
MUNGU ni Yule Yule jana ,leo na hata
milele hivyo kama alitumia ndoto kuzungumza na watu wa zamani hivyo hivyo hta
sasa hataacha kuzungumza na watu kupitia ndoto.
Kama unataka kumsikia sana MUNGU kupitia NDOTO basi
una bidi uwe muombaji sana hasa wakati wa
kwenda kulala, Mwuombe MUNGU karibia hata masaa mawili(2) kwa kuwa unapomuomba
MUNGU uwepo wake huwa una shuka na katika uwepo wake huwa kuna sauti ya MUNGU
ambapo kama ukiwa umelala unapata sauti ya MUNGU kwa ufasaha zaidi kwa sababu
ya uwepo wake.
Mungu hatakaa aache kuongea na watu wake
kupitia ndoto na katika ndoto MUNGU hutuonya,hutufundisha na kutuelekeza pia
inategemeana na jinsi apendavyo
Imeandikwa “Nao wakiisha kuonywa na Mungu
katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine.”- Mathayo 2:12
Kwa mafundisho mengi
zaidi ya jinsi ya kufsiri ndoto bonyeza hapo.... . ..http://jasirimbarikiwa.blogspot.com/2015/09/jinsi-ya-kutafsiri-ndotomaono-yako.htmll
5.MUNGU huongea kupitia MAONO /
UNABII.
Imeandikwa “Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi
ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.”- 2 Petro
1:21.
Hii ni namna ya MUNGU ambayo huitumia kuwasiliana nasi na njia hii MUNGU
huitumia kwa watu ambao wamekuwa kweli kweli kiroho yaani watu ambao ni well
advanced Spiritual.
Namna pekee ya kufikia kiwango cha kumsikia MUNGU kupitia njia hii ni kupitia
maombi yaani mtu anayeomba muda mwingi
na kisahihi huku akijua neno la MUNGU.
Mara nyingi imekuwa
ni karama MUNGU kuongea na watu kupitia njia hii kwa kuwa kwa kipawa hicho MUNGU
huweza kufungua watu kwa kuwajulisha sauti ya MUNGU kwao.
Watu waliopewa karama
na vipawa hivyo ndiyo tunawaita manabii Imeandikwa
“Kisha
akawaambia,Sikizeni basi maneno yangu;Akiwapo nabii kati yenu,Mimi,Bwana,nitajifunua
kwake katika maono,Nitasema naye katika ndoto.”- Hesabu 12:6
Ni ahadi ya MUNGU kwamba ataongea nasi kwa
njia hii kwa kuwa ataachilia ROHO yake kwetu na kwa ROHO hiyo tutapata kuona na
kusikia sauti yake . Imeandikwa “Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu,
nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na
vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto.”- Matendo ya Mitume 2:17
6.MUNGU huongea kupitia sauti KABISA
masikioni mwako yaani WAZI WAZI BILA mafumbo.
Njia hii mara nyingi ni kwa neema kubwa na pia ni karama
kwa ajili ya kanisa katika kulikosoa
,kulirekebisha na kulitia moyo ili kulijenga imara.
Imeandikwa “Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana,
waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la Bwana yeye ataliona. Mbona basi ninyi
hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?”- Hesabu 12:8
Watu wote ambao MUNGU alikuwa akiongea nao waziwazi walikuwa hajafanya
jambo lolote lilo wafanya wawe qualified kusikia sauti hiyo yaani watu wote
waliosikia sauti ya MUNGU wazi wazi bila ya mafumbo hawajafanya jambo ambalo
liliwafanya wastahili kusikia sauti hiyo bali ni neema tuu ya MUNGU.
Soma mfano wa sauli alikuwa ni mtu aliyelitesa kanisa
lakini neema ya MUNGU ilimuangikia na akasikia sauti waziwazi ikimkemea kuhusu
kitendo kibaya anachokifanya kuhusu kanisa Imeandikwa
“Akaanguka
chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi” -Matendo
ya Mitume 9:4
Ngazi hii haina kanuni kama sauti zingine za MUNGU kwa
kuwa MUNGU kwa neema yake tuu anaweza kunena nawe kwa sauti juu ya jambo lolote
lile kwa sauti yake pasipo mafumbo.
ANGALIZO KUU :Kama Ilivyo kwamba MUNGU anaweza kuzungumza na watu wake pia vivyo
hivyo shetani aweza kuongea na watu wake.
Namna pekee ya kutambua hiyo ni sauti ya
MUNGU au ni ya shetani ni namna moja tuu kuwa kama sauti unayoisikia inapingana
na neno la MUNGU(BIBILIA ) ujue hiyo ni sauti ya shetani na kama hiyo sauti
haipingani na neno la MUNGU ujue hiyo ni ya MUNGU.
Mfano:Umekaa
sehemu nawe ukasikia sauti ikikwambia “nyanyuka
nenda kaibe sehemu fulani......” na
haujaona mtu yeyote akisema , hata kama
akisema anayenena sauti hiyo ni YESU wewe ikatae na kuikemea katika jina la
YESU, kwa kuwa YESU hawezi hata siku moja kujipinga na NENO lake kwa kuwa neno lake (BIBILIA ) linakataa
kuiba hivyo kataa kwa kuwa sauti hiyo ina pingana na NENO la MUNGU hivyo sii
sauti ya MUNGU bali ni ya shetani.
________