USHUHUDA WA MTOTO WA MIAKA 12 ALIVYOCHUKULIWA NA YESUKRISTO NA KUPELEKWA KUONYESHWA MBINGUNI NA KUZIMU.

Laura wamna(lala) ni mtoto wa miaka kumi na miwili (12), kutoka nchini indonesia.Tangu akiwa mtoto mdogo sana alikuwa anatamani sana akutane naye YESUKRISTO ana kwa ana.

Laura wamna anafahamika kwa jina lingine ambalo ni LALA sehemu moja akishuhudia alisema “ROHO wa MUNGU alinijia akanichukua mimi katika roho kukutana na YESUKRISTO”.Anaeleza jinsi ilivyokuwa  mpaka alivyochukuliwa na YESUKRISTO, alichokiona ni ukweli hakuna kilichopungua au kuongezwa.Tafadhali unaposoma ushuhuda huu omba ROHO mtakatifu akupe hekima yake na uelewa hata kabla hujasoma ushuhuda huu.

YESUKRISTO  ALIVYONICHUKUA  KUNINIONYESHA  MBINGUNI
·        YESUKRISTO alivyomtembelea LALA siku ya kwanza:Ilikuwa ni kipindi cha kusifu na kuabudu mikono yangu illikuwa imeinuliwa juu yenyewe, na nikamwambia mama yangu: “Mama, siwezi kushusha mikono yangu chini,na ilikuwa imeendelea kuinuliwa juu.Nikawaona malaika wengi ndani ya kile chumba, na ghafla nikaona mwanga mkali sana na unapotoka mwanga ule, kulikuwa na sauti ya BWANA ikisema nami.

Bwana YESUKRISTO aeleza juu ya kifo cha kaka wa LALA:BWANA akasema kutakuwa na kifo cha ndugu yangu wa karibu sana akazidi kusema akaniambia “Nenda kamwambie kaka yako wa karibu, mwambie anatakiwa anirudie MIMI , Kwa kuwa bado nina REHEMA kwa ajili yake, Kwa sababu maisha yake aliyokuwa akiyaishi yalikuwa mbali NAMI.” Kaka yangu alikuwa ana matatizo na alikuwa mzigomkubwa katika familia yetu.

·        YESUKRISTO alivyonitembelea siku ya pili:
Siku ya pili BWANA YESU aliniambia “utafaulu mitihani yako tena kwa daraja zuri”.Kipindi ambacho mimi na mama tulikuwa tunaabudu MUNGU, Ghafla malaika akaja akaitwa roho yangu tukaenda naye juu mpaka juu ya mbwamba naye malaika kanionyesha baadhi ya miji nayo ni Nabire, Serui, Biak, Manokwari.Malaika akaongea nami akisema “MUNGU kakwambia uende usimame katika hiyo miji na uhubiri ujumbe wa BWANA  ,wanatakiwa WATUBU kwa sababu “HAKUNA  MUDA  YESUKRISTO AKUJA HARAKA SANA””.Nilimuuliza yule malaika wewe ni nani ?,Malaika akanijibu “mimi naitwa  Gabriel”, Malaika wa BWANA .Ndipo aliponirudisha roho yangu kwenye mwili wangu.

·        Mauti ilivyozunguka watu:Tarehe 2o machi ,Nilipokuwa katika safari ya kutoka mji wa Abe to Entrop, Nikafikamji wa  Kotaraja nilikuwa kwemye taxi ambapo malaika akanichukua tukaenda juu ya jiji la Jayapura.

Malaika akaniambia “angalia”, Nilipotazama nikaona watu wengi wamesimama, Wamezaa nguo nyeusi zilizo wafunika kutoka kichwani mpaka miguuni na macho yao ni meusi na kuna moto ndani yao.
Niliwaona kila mahali hospitalini ,pembezoni mwa barabara,katikati mwa mitaa, masokoni, majumbani walikuwa kila sehemu.Niliona mikononi wameshika rato kubwa,Nikamuuliza malaika “hawa ni wakina nani?”, Akanijibu hao ni “malaika wa mauti”.

Tulipokuwa tunaruka kiroho juu ya mji wa Entrope, “Niliona makundi ya vijana wadogo wakinywa pombe mitaani, nilijawa na huzuni kwa sababu mauti ilikuwa imewazunguka kila sehemu”.
Malaika akaniambia “Lala, kama kuna kitu kimetokea na hauwi huru nacho., unaweza itia majina mawili nayo ni damu ya YESUKRISTO na kwa jina la YESUKRISTO kwa sababu jina hili lina nguvu sana.”.

Malaika kanichukua tukapaa juu ya mawingu nami nikazidi kuona dunia chini ikiwa ndogo na ndogo sana.Tulivyokuwa tunazidi kwenda  juu kuna sehemu tulipita ilikuwa nyembamba yenye giza na yakutisha.

Niliogopa lakini malaika alinishikilia tukafika nikaona mwanga na ilikuwa mbinguni, Mimi na malaika tulifika getini kulikuwa na malaika walinzi wawili mbele ya geti la mbinguni, Geti la mbinguni limepambwa kwa lulu nzuri za kung`aa ndipo lilipofunguka na wote wawili tukaingia tukawa tunatembea katika bustani.

Kulikuwa kuna mlango uliofunguka na ndani nikaona meza ndefu imepangwa vizuri inaonyesha kwamba si muda kutakuwa na sherehe(Ushirika mtakatifu/Holy communion), Kuna malaika waliosimama nyuma ya kila kiti, kila malaika ana tarumbeta mkononi mwake.Inaonekana kama vile wanaenda kupiga tarumbeta mapema.

Nikaendelea kutembea na katika bustani niliona miti mizuri sana,matunda mbali mbali mazuri, nikaona maua mazuri sana, Malaika Gabriel akaja akaniambaia “muda wako wakukaa hapa umeisha unabidi urudi” nami nikamjibu “ninafuraha na amani kukaa hapa sipendi kurudi”.Ghafla sauti ikatoka kutoka kwenye kiti cha Enzi ambako kulikuwa na mwanga na utukufu ikisikika “Lala ,unatakiwa urudi sasa”.Malaika Gabriel kanisindikiza akanirudisha.

Kutoka juu naliangalia na kuiona ile taxi nyekundu niliyekuwa nimeipanda mwanzo ,ilikuwa ikienda ofisi ya serikali ya mji wa Entrope.Malaika akairudisha roho yangu kwenye mwili wangu nikaamka nikasema “Halleluya!”.

Abiria ambao walikuwa pamoja nami kwenye hiyo taxi walishangaa na kupigwa na butwaa, Wakiniuliza “Dada, je ni mzima ?”.Nilishangazwa sana kwa sababu nilijikuta nikining`inia kwenye bega la abiria mmoja, naye alikinichuwa na mafuta kwenye pua kwa kuwa walidhania nimezimia.Nalisimamisha taxi pale nilipofika nyumbani.

Ilipofika saa11 usiku nilipokuwa nimelala, Malaika akanijia kunipeleka kwa Bwana, Tukaingia katika geti la mbinguni, Na nikaona mtu amesimama naye amevaa kamba ndefu nyeupe.Akanionyesha mikono yake kwangu, Nami nikatembea kufika karibu naye, nikajua kuwa ni YESUKRISTO akanichukua tukatembea wote mbinguni.Mbinguni ni pazuri sana na kuna kila aina ya maua ambayo sijawahi yaona duniani.

Kila kitu kipo pale , moyo wangu ulifarijika sana na kuwa na amani isiyokuwa ya kawaida,kuna miti ya vivuli,itoayo matunda na kwa uwazi kabisa kulikuwa kuna mto.Bwana YESUKRISTO akaniambia “Lala, utajaribu kuweka miguu yako kwenye maji ?,”Nami nikaichovya kwenye maji.YESUKRISTO kaniambia tena “unaweza kunywa maji haya”.

Nilipokunywa yale maji nikajisikia amani katika moyo isiyokuwa ya kawaida.YESUKRISTO aniambia “waweza kuzamisha hata kichwa chako humu kwenye maji na bado ukawa unauwezo wa kuhema ndani mwa maji haya”.
Alichokisema YESUKRISTO  kilikuwa ni kweli kabisa.Kulikuwa na samaki wengi wakiogelea karibu yangu, Nikamwambia YESUKRISTO “Nilipokuwa duniani sikuweza kukamata samaki kwa kuwa kule samaki wanakimbia ukitaka kuwakamata ”.YESUKRISTO akaniambia “Samaki wa huku wanaweza kuongea na wewe, Lala !”.

Baada ya muda nikamuuliza YESUKRISTO “Wawezaje kuona dhambi wanazozitenda  watu dunia nzima na huku dunia ni kubwa sana, waona je?”.YESUKRISTO kaniambia “njoo pamoja nami huku.”nikaenda akanionyesha kuna kioo kikubwa na nikaona dunia kuwa ni ndogo.

Nikaweza kuona watu wanaofanya dhambi nilishangazwa kuomuona mtu ninayemjua nikamwambia YESUKRISTO , “Bwana, naweza kuona yote chini” mama na baba walikuwa wamelala kitandani.Naye YESUKRISTO akanijibu “Ndio, na kuna malaika amesimama katika chumba chako.”
Mimi na Bwana YESUKRISTO tukatembea tena, kulikuwa na chumba ambacho malaika wawili(2) walikuwa wamesimama hapo nje.Kulikuwa na kitabu kikubwa mezani, na nikamuuliza Bwana, “MUNGU, kitabu cha aina gani hiki ?”, YESUKRISTO akanijibu, “Hiki ni kitabu cha uzima”,Nikamuuliza tena “naweza kuona ndani yake ?”, Bwana YESUKRISTO kaniambia “Ndio, unaweza”.

Na hao malaika wawili (2) walikuwa wako tayari kufungua kile kitabu kurasa baada ya kurasa, Kwenye ukurasa wa kwanza nikaona  moja ya majina ya familia ninayoijua, Nikaona tena kuna jina la kaka yangu nikamwambia YESUKRISTO  “Bwana, hili ni jina la kaka yangu” na Bwana akajibu “Ndio, ninayajua maisha yake na sasa yupo humu akimsifu Bwana”.

Malaika akanifungulia ukurasa unaofuata nikaona jina la mtu ninayemjua tena nikamwambia YESUKRISTO “Huyu ni mjomba wangu”.Naye Bwana akanijibu “Ndio , yuko hapa ” .Nikamkumbatia YESUKRISTO huku nikilia.
Tukaendelea kutembea na YESUKRISTO kwenye bustani nikaona watu wawili(2) wakinijia mmoja anaonekana kama anamiaka 18 au 19 hivii,na mwingine kama ana miaka miwili(2) akanikimbilia akanikumbatia nikaona kama amenipita kwa kuwa tulikuwa wote katika roho.

Huyu aliye mkubwa wa kama miaka 18 au 19 alikuwa anafanana na mama yangu yaani walikuwa kama mapacha na mama yangu kwa jinsi alivyofanana naye,  Ndipo nikakumbuka kuwa mama aliwahi niambia ana kaka yake ambaye alikufa nilivyokuwa mdogo sana,Nikwa nimemjua atakua ndiye nao wote wakaenda katika vyumba vyao.

Nikaona maua mazuri nikawa namuuliza Bwana , “Je naweza kuchuma ua hili ?,ningependa kumpa mama yangu kwa kuwa mama yangu anapenda maua” .YESUKRISTO akanijibu “Muda haujafika bado wa wewe kuchukua maua na matunda kutoka sehemu hii mwanangu !”.

Tukawa tunaendelea kutembea na YESUKRISTO nikaona nyumba ambayo mlango wake uko wazi, nikamuuliza YESUKRISTO kama naweza ingia humo,Bwana akanijibu “ndio ,waweza kuingia”.
Nilipofika mbele ya mlango wa nyumba, sikuingia ndani kwa sababu nilikuwa nashangaa sakafu ya dhahabu.Nikamwambia Bwana “MUNGU waooh !!!, ..chini pazuri sana hivi, duniani dhahabu ni ghali sana”. Naye YESUKRISTO alikuwa akibasamu na akasema “Hii ni nyumba yako ,na kuna baadhi ya nyumba zinazofanana na hii.”

Nikamuuliza YESUKRISTO “Bwana ninaweza kwenda nyumba ingine ?”.Bwana akanijibu “ nyumba ambazo milango imefungwa , ni za watu wengine”.YESUKRISTO akaniambia “Nifuate mimi”.

YESUKRISTO ALIVYONIPELEKA KOUNA KUZIMU.
Bwana YESUKRISTO alinishika wote tukaenda njia pana.Nikaanza kuhisi harufu mbaya kwa kadiri tunavyozidi kwenda nikajisikia hewa inakuwa ya moto.Kwa mbali nikaona pepo lenye miguu mitatu amebeba mikuki mitatu iliyoshikana na alipo muona YESUKRISTO akampigia magoti.

Tukaendelea kwenda mimi na Bwana YESUKRISTO huku akiniruhusu niangalie kwa undani zaidi ambako kuna watu walikuwa wakiteswa na shetani.Shetani alikuwa akiwatesa mpaka miili yao inabaki kuwa vipande vipande lakini hawafi.

·        WAZINZI:
Nikaona kitabu juu yake kimeandikwa “uzinzi”.Nikaona watu uchi wakiwa kwenye moto.Walipomuona YESUKRISTO wakaanza kumuita “Baba, Baba” lakini YESUKRISTO hakuwatazama.

·        Watumishi wa MUNGU:
Nilivyozidi  kuangalia nikagundua kuna watumishi wa MUNGU.Ndipo nikamuuliza YESUKRISTO, “Bwana !, Kwa nini kuna mtumishi wa MUNGU hapa kuzimu ?”.YESUKRISTO kanijibu kuniambia “Nilimchagua yeye lakini haku utoa ujumbe wangu”.

Ndipo yule mtumishi alipomuona YESUKRISTO akamwambia “Baba Baba, tafadhali niondoe hapa japo kwa dakika moja, nataka kutubu”.Bwana akamjibu “umechelewa ,akasema sasa namtumia binti huyu akinionyeshea kidole “mimi(lala)” kama mmoja wa watumishi wangu”.

Nikaona watu wengi wakiteswa, YESUKRISTO akaniambia mimi “hawa watu hawakuwa waaminifu kutoa fungu la kumi(zaka)”.
Nikaona kundi kubwa la vijana wadogo ambao walikuwa wanacheza muziki kwenye misumari, Kama muziki huo wa rock ukisikika basi wao wanatakiwa kuruka kwa haraka zaidi na hawakuruhusiwa kusimama hata muda kidogo.Kama wakisimama, shetani anakuja kuwatesa sana.

Ndipo tukarudi tukatoka kwenye njia pana na kuingia mbinguni.Tulivyofika mbinguni , Bwana YESUKRISTO kaniambia, “Lala, Yote uliyoyaona ukawaambie watu wangu”.Bwana YESUKRISTO akanichukua na akasema, “Lala, umesalimisha maisha yako Kwangu, unatakiwa ubatizwe mwezi machi 25 na mtumishi wangu Ronald, naweka amana kwake ili uweze kuandika kitabu chako”.

YESUKRISTO kamuangalia malaika Gabrieli na Gabrieli kapiga magoti kuabdu chini ya miguu ya Bwana YESUKRISTO.YESUKRISTO kamwambia malaika Gabrieli “Mrudishe mnangu.”

Gabrieli akanichukua na akatembea nami nje ya geti nikamwuona malaika mwingine akawa anaongea na Gabrieli kwa lugha ambayo nilikuwa siielewi, lakini Gabrieli alinionyeshea mimi na kuangalia kweye kiti cha enzi cha Baba MUNGU ,alikuwa malaika maiko naye YESUKRISTO akatutazama ,malaika maiko akapiga magoti na kumruhusu Gabrieli na mimi tuendelee na safari yetu.

Tulipokuwa niani tunarudi ,Gabrieli alniuliza “Ulikuwa unaongea nini na Baba?” .Na nikamjibu , “Kuna vitu vingi ambavyo YESUKRISTO ameongea nami”.Nikamuuliza malaika Gabrieli “Unafanya nini mbinguni ?”.Malaika akanijibu “Ni mlinzi wa Bwana YESUKRISTO, Chochote ambacho Bwana YESUKRISTO ananiagiza kukifanya ndipo nakifanya chote”.

Tulipokuwa tumefika karibu na nyumbani takatembea nikaona malaika wa vifo wamesimama pembezoni mwa barabara kushoto na kulia.Nilipofika nikaona mbele ya nyumba kuna malaika wa mlinzi wa BWANA.
Malaika wa kifo alikuwa anatamani sana kuingia nyumbani lakini hakuweza kwa sababu kulikuwa na malaika wawili(2) walinzi wa Bwana walikuwa nyumbani kwetu.Malaika wa mauti alitaka kuingia mara ya pili akatupwa nje ,akaanguka na kupotea kama vumbi.

Gabrieli kanisindikiza mpaka kwenye chumbani kwangu ndipo roho yangu ikarejea na kuingia katika mwili wangu nami nikarejea katika shughuli zangu za kawaida.
Alhamisi ,Machi 22.Tulikuwa na ibada nyumbani na baadhi ya watu wakanisani kwetu, Ndipo malaika Gabrieli alipokuja kunichukua kunipeleka kwa YESUKRISTO.YESUKRISTO alinionyesha mji ninaotakiwa kwenda.Aliniambia nikatoe ujumbe wake kwenye kanisa la Katoliki lililopo Wamena.

Ijumaa.machi 23.Malaika akaja kunichukua kunipeleka kwa Bwana.YESUKRISTO katoa ujumbe maalumu kwa kanisa lililopo kijijini “Harapan” na akasema “Kaliambie kanisa ,wasiwewanachelewa sana ibada.Kwa wale ambao mara zote wanachelewa hao hawatakuwa sehemu ya ufalme wa MUNGU.

Ibada inapoanza hatakiwi yeyote kubakia nje  ya kanisa akazidi kuniambaia waambie wamama wenye watoto ambao bado ni wachanga wanatakiwa kukaa ndani ya kanisa ili kusikiliza NENO la MUNGU.Asiwepo wakukaa nje hata kama kanisa limejaa wanaweza kukaa chini wasikilize NENO LANGU sio shida, kila mtu aheshimu NENO LANGU.

Siku hiyo hiyo tuliomaliza “maombi ya kufunga”,Nikatoa ujumbe wa Bwana YESUKRISTO kwa walimu wa shule ya jumapili(Sunday school) ,nikaanza kurudi nyumbani kutoka kanisani.

Malaika wa Bwana akanijia njiani na kuniambia “asante lala umeutoa ujumbe wa Bwana kwa walimu wa shule ya jumapili”.Akaongea nami “Jumaili utoe ujumbe kwa waumini kanisani.Utatakiwa kutoa ujumbe si kwa kanisa tuu na familia, lakini pia unatakiwa utoe ujumbe kwa dini zingine pia wadudha,uisilam, uhindizim na kadhaliaka.

Wao pia wanatakiwa kupokea wokovu, toa ujumbe mapema kwa kadiri uwezavyo kwa sababu nitakuchukua kukupeleka katika miji mingine.”(yohana 14,6).
Ilivyofika saa moja jioni ,Malaika wa Bwana akaja kunichukua na kunipeleka kwa Bwana, Bwana YESUKRISTO akasema nami “Lala ,haraka, haraka ,haraka kimbia na uwaambie watu wangu ,Muda wangu umekaribia kuisha!” .
Na Bwana YESUKRISTO akanionyesha ,muda wa mbinguni .Nikaona mkono mfupi umeonyeshea kwenye namba na mkono mrefu uko karibu nao sana ingawa sikuweza kuona namba katika saa.
Bwana YESUKRISTO kaniambia, “Lala, kimbia karaka nautume ujumbe kwa watu wangu,Muda wangu umekaribia kuisha”.YESUKRISTO kaniambia tena “Lala, hakuna malaika aliwahi kuona muda mbinguni.Nakuruhusu wewe kuona muda wa mbinguni ili uende kutoa kwa haraka ujumbe wangu”.

Majira ya saa 2:30:-Malaika kanijia na kunichukua kwenda kwa Bwana ,Bwana YESUKRISTO tena akanionyesha jinsi muda wa mbinguni ulivyobaki mfupi sana.Bwana YESUKRISTO kaniambia “Waambie watu wa darasani kwako, walimu wako, majirani zako na yeyote yule unatekutana naye.Waambie watubu na kunirudia mimi.”

Jumamosi, mach 24-saa 7;-Nilikuwa na mama na shangazi yangu.Tulikuwa katika nyumba ya familia ya Wilson Sentani.Kipindi shangazi yangu alipokuwa akiomba kwa ajili ya familia ya Wilson, na nilipolala chumbani nikamuona malaika kaja, Niliweza kumuona malaika kwa sababu roho yangu ilikuwa nje ya mwili na kukaa kwenye kitanda.

Nikamwita malaika kuingia katika chumba lakini malaika alikuwa amesimama nje ya chumba na nikamwita tena ,na malaika akanijibu “siwezi kuingia chumbani, (akamnyooshea kidole shangazi yangu),mtumishi anapoongea na Baba ,hivyo nimi nasubiri mpakaamalize kusoma aseme ameni”.Shangazi yangu alivyo maliza kuomba naye akaja.

Alinichukua na kunipeleka kwa YESUKRISTO naye Bwana akanipa ujumbe wakuja kuwaambia watu, siku ingine mnamo saa 6 usiku ,Nilikuwa nikijiona mwili wangu mzito sana , kwa sababu malaika alitaka kuja kunichukua , lakini mama yangu alizidi kuniambia niandae nguo zangu tayari kwa ajili ya ibada ya kesho.

Nilipokuwa nimelala, malaika akaja na kunichukua kwenda kwa Bwana.Bwana  YESUKRISTO akaniambia “Lala, mwambie mama yako awe anakuruhusu ulale pindi unapojisikia mwili wako mzito sana, kwa sababu kuna jambo muhimu sana ambalo nataka kusema nawe.”

Akanihakikisha mara ya pili,YESUKRISTO akasema “Lala, kwa nini ?umesahau kutoa ujumbe niliokuambia uutoe,Unatakiwa ukumbuke kila nilichokwambia na uwaambie watu”.Nikasema “Bwana, tafadhali nisamehe mimi” naye Bwana YESUKRISTO akajibu “Nitarejesha kila kitu utavyoshuhudia”.

Jumapili, Machi 25, wakati wa asubuhi.-Kwa rehema za Bwana YESUKRISTO, Nilisimama na kutoa ushuhuda wote wa ujumbe wa Bwana YESUKRISTO kwenye kanisa la Barachiel.Baada ya kumaliza kuutoa ushuhuda,Nilijikuta nimebatizwa (kufa na kufufuka na YESKRISTO) na baada ya ibada kulikuwa kuna kikao cha kufanya uamsho.

Nami nilitakiwa kushiriki katika huduma hiyo ya uamsho nikamuona malaika kaja kunichukua kunipelaka kwake YESUKRISTO ,Bwana akaniambia “Waambie watumishi wangu waende katika huduma hiyo ya uamsho nami nitashuka na kuingilia kati kuleta usuluhisho”.

Kipindi bado nipo katika nyumba ya mchungaji ,Bwana alinionyesha shimo kubwa ambalo lilikuwa refu na lenye giza.Nikaona watu wengi wakivutwa kwenda kwenye hilo shimo,Nao walikuwa wakijitahidi kujizuia lakini wakishindwa na kuanguka mpaka kwenye shimo hilo.

Machi 26;Malaika kaja kunichukua tukaenda mpaka kwa Bwana YESUKRISTO naye Bwana kaniambia “Nitakutumia wewe kama mtumishi wangu mpaka nitakapo kuja, Kazi zote na majukumu yote nakupa wewe, hayajaisha bado, lakini nitazidi kukutumia wewe mpaka nitakapo kuja.”

Saa sita malaika kaja kunichukua kunipeleka kwa Bwana,Tena Bwana YESUKRISTO akanionyesha shimo kubwa lenye giza.YESUKRISTO akaongea nami “Shimo unaloliona  ni sehemu kwa ajili ya wasio waaminifu nao wataenda kwa mika mitatu na nusu( mika 3.5) miaka ya dhiki kuu(Ufunuo 13), Na huku kwa walio waamoinifu kwangu nitawachukua mpaka sehemu niliyo waandalia, mbali na macho ya joka.”

YESUKRISTO kaniambia “Lala, usipingane na mama yako, tena usiende kinyume na amri yangu ya 5,unatakiwa uwaheshimu mama yako na baba yako.”
Nilipomsikia akisema hivyo Bwana nilijisikia mwenye hatia na nikalia.Nikamuona YESUKRISTO akilia na akionekana mwenye huzuni. Niliona machozi yakitoka kwenye macho Yake.Bwana YESUKRISTO kaniambia “Lala usilie , ninataka unisikie na utii amri yangu ya tano(5)(uheshimu wazazi wako) hivyo uweze kuishi maisha marefu na yenye baraka.

Nataka nikutumie wewe kiajabu na kwa kushangaza futa miziki ya kidunia kutoka kwenye simu yako” .(yakobo 4:4).Akaniambia unatakiwa uwe mtaratibu na mkimya hata ukiwa shuleni,YESUKRISTO akaniambia “nitawezaje kukupa ujumbe kama wewe haujatulia mwenyewe.”

Nami nikamjibu “Bwana , siwezi kwa kuwa marafiki wanakuja na kunisumbua na hata kutakua nikacheze nao,Vipi kama nisipo enda shule si ndio itakua vyema ?”,Naye akajibu “Hapana, unatakiwa uende shule”.
Machi 27-04:30,Siku niliyokuwa na mtihani shuleni, Malaika alinichukua mpaka kwa Bwana YESUKRISTO naye akaniambia “ HAKUNA MUDA ZAIDI, unatakiwa uwape watu ujumbe wangu haraka sana”.

Katika ibada ya kuabudu jumapili  , kama kawaida malaika alinichukua mpaka kwa Bwana YESUKRISTO. Niliona YESU amesimama mbele ya geti akinisubiri mimi na nilipofika,YESUKRISTO kaniambia “Unatakiwa uende kule ile sehemu ya wamena mara moja na uwape ujumbe wangu, kuwa wanatakiwa WATUBU kwa sababu muda umekwisha.Unatakiwa uende Wamena”.

Bwana alikuwa akiongea huku uso wake ukiwa wenye huzuni na wenye kusinyaa huku akilia, Machozi yake yakidondoka pale kwenye meza ya kioo ambayo anaweza kuona kila kitu ambacho watu wanakifanya.

Nikamuuliza “ Bwana kwanini walia ?” .Hakunijibu swali langu na huku machozi yakizidi kumtoka nakudondoka kwenye meza nami nikayafuta machozi na kamba nyeupe nilioivaa, kila nilivyokuwa mbinguni nilikuwa mara zote navaa kamba nyeupe ambayo sijawi ivaa popote duniani.

Ndipo Bwana akaniambia huku machozi yakimtoka “Lala, waambie watu wangu haraka ,wanatakiwa warudi kwangu haraka, Muda umekwisha kabisa .”Bwana YESUKRISTO kasema tena, “Sitamani mtu yeyote apotee, lakini wote wakae katika ufalme wangu”.

MUNGU unaposoma ujumbe huu pia mshirikishe na mwingine (share),
Badilika na uanze kuishi kama MUNGU atakavyo hapo ndipo utakapo okoa maisha yako.
Ushuhuda wa Laura Wamna(LALA), dada wa miaka kumi na mbili (12) kutuka Indonesia.





Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...