Maono aliyopewa Ndugu Emmanueli Samsonjude na Bwana YESUKRISTO.
4 Kupita sauti ya maji mengi, maji makuu, Kupita mawimbi ya bahari yaumkayo, Bwana Aliye juu ndiye mwenye ukuu.
5 Shuhuda zako ni amini sana; Utakatifu ndio uifaao nyumba yako, Ee Bwana, milele na milele.[ Zaburi 93:4-5].
4 Kupita sauti ya maji mengi, maji makuu, Kupita mawimbi ya bahari yaumkayo, Bwana Aliye juu ndiye mwenye ukuu.
5 Shuhuda zako ni amini sana; Utakatifu ndio uifaao nyumba yako, Ee Bwana, milele na milele.[ Zaburi 93:4-5].
Kila aliyeko chini ya jua yuko na mkakati; na mkakati unaweza kuwa ama MZURI au MBAYA, Inaweza kuwa ni wa MUNGU au SHETANI.MAAMUZI yako ndiyo yanayopelekea HATIMA yako kwa sababu huwezi kumtumikia Mungu na mammoni.
Tangu uko kwa KRISTO, yakale yamepita.Kwa sababu wewe ni kiumbe kipya;Unatakiwa utoke kutoka kwenye vichafu vyote.[ 2 Wakorintho 6:14-18].
Nakumbuka miaka ya nyuma kabla sijaokoka nilikuwa nawaza kuja kuwa muuaji wa kukodiwa !.Namshukuru MUNGU leo kwa sababu Bwana ameharibu kila mipango ya shetani.YESUKRISTO amenigeuza sasa na kunifanya kuwa mleta watu kwake kwa utukufu wa Ufalme Wake.[1 Petro 2:9-10].
YESUKRISTO bado aweza badili maisha yako !Mkubali sasa na atakugeuza kuwa mtoto wa kipekee Kwake.
UTEMBELEO WA YESUKRISTO
Ilikuwa ni mida ya saa 2:50 jioni ,nilikuwa niko kitandani, nilipokuw kitandani.nilimuona Bwana YESUKRISTO;Alikuja kwangu na kusema “NIMEKUJA KUKUONYESHA WEWE KITU FLANI MUHIMU”.Nikasema, ‘Bwana, uliniambia itakuwa mwisho kunitembelea na kunionyesha mambo hayo katika ile mara ya tatu, Kwanini umekuja tena Bwana ?’.Alitabasamu na kusema, “MWANANGU, ULINIJIBU MIMI NILIPOKUULIZA WEWE KITU GANI UNACHOTAKA KUKIONA KATIKA UFALME WANGU,NAWE UKASEMA KUWA MAPENZI YAKO YATIMIZWE !KWA HIYO IMEKUPA NAFASI YA KUONA JINSI WATU WANAVYOTAKIWA KUWA MBALI NA DHAMBI ZAO.”Nikajibu, “Nikweli uliniuliza hivyo uliponijia ile mara ya tatu, lakini najua ni rehema Zako zilizonisaidia kukujibu hivyo.”[ Zaburi 118:1]
NYUMBA YANGU MBINGUNI.
Bwana alinichukua mpaka Mbinguni na kusema, “MWANANGU, ULIOMBA KATIKA MAOMBI YAKO KUONA SEHEMU NYUMBA YAKO ILIPOFIKIA NA LAZIMA NIKUONYESHE.”[ Mathayo 7:7-8]Bwana alinichukua mpaka MBINGUNI na kunionyesha mimi nyumba.Nikaona malaika wengi wakikimbia na dhahabu mikononi mwao, maua, wakiwa wanapamba na kuongeza jengo.Nikamuuliza Bwana aniambie mmiliki wa nyumba hiyo.Bwana akajibu, “MWANANGU, INAMILIKIWA NAWE!” Nikatabasamu na kusema, “Lakini Bwana,niambie sababu kwa nini hao malaika wanakimbia hivyo ? na Bwana akasema, “KWA SABABU YA UFUNUO NILIOKUONYESHA WEWE UNALETA WATU WENGI KUELEKEA KATIKA NJIA NYEMBAMBA, MAOMBI YAO YA WATU WENGI SASA NI KAMA MOTO.WALIORUDI NYUMA WENGI WAMERUDI KWANGU ! WATU WENGI WANAVYO ZIDI KUNIPA MAISHA YAO KUPITIA USHUHUDA WAKO.NDIVYO NYUMBA YAKO NA NDIVYO JINSI NYUMBA YAKO INAVYOKUWA KUBWA !.” [1 Yohana 4:4] [Mathayo 11:28].
LAZIMA URUDI KWENYE UPENDO WAKO WA MWANZO
Baada ya hayo MUNGU alinichukua sehemu mbali mbali Mbinguni kitu ambacho kilinipa huzuni sana katika moyo wangu;Naamini kuwa watu wengi watarekebisha njia zao.[2 Petro 3:9]Niliona baadhi ya nyumba Mbinguni ambako malaika walikuwa wamesimama kuendelea kujenga.Hizo nyumba zilikuwa ndogo sana.Malaika husika walikuwa wenye huzuni kwa sababu, Kwa kuwa walikuwa tayari kufanyia kazi sehemu hiyo na hawakuweza tuu kwa sababu mmiliki alikuwa haendlei kumfanyia kazi YESUKRISTO.Na nilipiga kelele, “Ohh Bwana kwanini ?”, Na Bwana akaniambia, “MWANANGU, ANGALIA KWA MAKINI !HIZI NYUMBA ZINAMILIKIWA NA WALE WALIO ACHA UPENDO WAO WA KWANZA.WAMEACHA KUFANYA MAPENZI YANGU,HAWAFANYI TENA KAZI KWA AJILI YANGU LAKINI WANAFANYA KAZI KWA AJILI YA MIFUKO YAO,WAMEACHA UPENDO WAO WA KWANZA !, WAAMBIE WATUBU NA KURUDI KATIKA NJIA KWA SABABU INAWEZA IKAWA WAMECHELEWA WAKISEMA NGOJA NGOJA” [Ufunuo 2:4-5]
ENDELEA TUU KUPANDA MLIMA
Bwana akanichukua mpaka sehemu na akasema, “MWANANGU, ANGALIA NA KUONA KINACHOTOKEA KWA WATU WANGU, NATAKA WAWE NA UVUMILIVU NA KUWA IMARA”[Marko 13:13].... na tazama, nkaona mlima mkubwa, na watu wasiohesabika wanaupanda.Nikagundua kuna sehemu katika huo mlima ulikuwa umejaa MIBA, na baadhi ya sehemu zilikuwa za MOTO kama moto na sehemu nyingine zilikuwa LAINI.Mwanzo sehemu zote za mlima zilikuwa rahisi sana kuzipanda.
NGUVU YA KWANZA
Katika haya , Bwana aliniagiza na kusema nami, “ANGALIA KWA MAKINI NA ULIZA CHOCHOTE UNACHOPENDA KUKIELEWA”Nikaona baadhi ya watu wanakimbia kupanda ule mlima na wakaanza kuupanda kwa haraka na furaha.Ghafla!, wakafikia kwenye sehemu yenye miba ya ule mlima, wakarudi nyuma na kukimbia kuacha kupanda mlima, na siku waona tena.Nikamuuliza Bwana niambie maana ya hiki Naye akaniambia, “HII INAITWA NGUVU YA KWANZA.HII NI WALE WALIOSIKIA NENO LANGU NA KULIPOKEA KWA FURAHA, NA KUNIKUBALI MIMI KAMA BWANANA MOKOZI WAO BINAFSI, LAKINI MAJARIBU YA DUNIA NA STAREHE ZILIPOWAJIA, WAKAANGUKA NAKUACHA KUNIFUAA MIMI.HAWAKUVUMILIA , KWA SABABU WOKOVU WAO HAUKUWA IMARA”[Luka 8:13-14][Luka 6:49].Je wewe u kati ya watu hao?, Tubu sasa na uokolewe.
SEHEMU YA MOTO YA MLIMA
Bwana alinionyesha mimi wakristo wengi katika sehemu ya moo ya mlima.Baadhi walishindwa kupita kwenye hilo eneo kwa sababu lilikuwa la moto.Nikaona baadhi ya watu hawakujali lilivyo jinsi linavyo waumiza miili yao;Wao walichotaka nikumaliza kupanda ,na kupumzika mwishoni.Nikamuona Mtu aliyesimama kwenye mlima; mara zote anapokea wale wanaomaliza kupanda huo mlima na kuwaingiza katika sehemu nzuri sana.Hiyo sehemu inaitwa “LANGO LA UFALME WA MBINGUNI”[Isaya 35:8-9]Nikamuuliza Bwana aniambie mimi maana yake Naye akasema, “HAYA NI MAJARIBU KWA IMANI ZA WATU WANGU NA KAMA WATAVUMILIA MPAKA MWISHO WATAKUWA WANGU.”[1 Wakorintho 15:58] Kwa hiyo nikamuuliza Bwana, “ina maana sio wako kabla haajamaliza majaribu ?” Naye akanijibu, “MWANANGU,NILIIMALIZA KAZI YANGU KWA KUVUMILIA MAJARIBU....NA NDIO WOKOVU UKADHIHIRIKA.HIVYO WATU WANGU PIA WATAPITA KWENYE MAJARIBU.KAMA ILIVYOSEMA, ‘Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.’”[Yakobo 1:12].
SEHEMU LAINI NA NYEPESI YA MLIMA
Na nikaona wale waliofikia sehemu ya wepesi na ya laini,Ilikuwa iko laini kiasi kwamba wengi waliofika hapo walijipumzisha mpaka wengine kufikia kulala hapo, lakini wapo waliokuwa hawapumziki bali wakizidi kuupanda tuu huo mlima.[Isaya 40:29-31]Tazama, wengi wao waliokuwa wamelala katika eneo lile walianguka na kupotea !.Ghafla nikasikia sauti kubwa ikisema, “WAAMSHE,WAAMSHE KWA KUWA MUDA NI MFUPI KUPUMZIKA HAPA” Na ghafla wengi wao waliokuwa wamelala katika hiyo sehemu laini waliamka na kurudi kuendelea na safari.Wengine walionekana kuidharau sauti na kuendelea kulala.Nika muuliza Bwana nisaidie mimi ili niweze kuelewa.Naye akasema, “MWANANGU,NINAFURAHISHA NA UUMBAJI WANGU JUU YAKO !HAKIKISHA HAYA YATOLEWE KATIKA MAANDISHI ILI WATU WANGU WAJUE NINI KINACHOTOKEA KATIKA UTU WAO WA KIROHO,ULIZA KUJUA CHOCHOTE KIGUMU KWAKO KUKIELEWA !”.
Nikasema, “Tafadhali niambie maana ya sehemu hii laini ya mlima huu.”Bwana alinijibu, “SEHEMU LAINI YA MLIMA NI HALI YA MAISHA AMBAYO WATU WANAFIKIA WANAPOFIKIRI HAKUNA HAJA TENA YA MAOMBI, KUFUNGA NA KUFANYA UINJILISTI !”
[2 Timotheo 2:7], Nikawaza Bwana aniambie maana ya wale walio anguka chini kutoka kwenye sehemu laini na kupotea.Bwana akaanza kulia na kusema, “MWANANGU, WALE WALIOLALA NA KUPOTEA.”[1 Wakorintho 15:18],Nikihitaji kujua na wale waliopumzika na kulala pale.Bwana YESU alisema, “HAWA NI WATU WANGU WALIOFIKA SEHEMU AMBAPO WANAFIKIRI VITA IMEKWISHA NA HAWAHITAJI TENA KUOMBA NA KUFUNGA.WAMESAHAU NILIPOJARIBIWA NA SHETANI NA KUNIACHA MIMI ILIKUWA HIVYO KWA KITAMBO TU NA KURUDI TENA[Luka 4:13].
WAMESHINDWA KUELEWA UTAKATIFU.HAWAKO TAYARI NA HAWAWEZI KUDAKA KUYAPTA MAONYO YANGU !, WAAMBIE WALE WANAO LALA WATAANGAMIA !, HIVYO ,AMSHA WALE WALIO LALA WAAMKE KUTOKA WAFU NA NITAWAPA NURU”[Waefeso 5:14]
Nikamuuliza nini maana ya sauti kubwa inayosema “AMKA”, na Bwana akasema, “HAYO NI MAONYO YANGU KWA WAKRISTO WENGI WANAOJIITA WENYEWE WATUMISHI WANGU; NAWAONYA KUPITIA MAONO, NDOTO NA KUPITIA VITU VINGINE VINGI ILI WAACHE KUANGUKA!” [Zaburi 19:7-11]
Nikamuuliza Bwana aniambie kuhusu wale wanaopuuzia sauti.Naye akasema, “WALE WALIOSIKIA MAONYO YANGU KUPITIA MAONO NI WALE NINAO WAAMSHA KUTOKA USINGIZINI.WALE WANAOPUUZIA MAONYO YA SAUTI YANGU NDIO WALE WANAO NIITA MIMI MUONGO!,WAAMBIE WATUBU NA NITAWAVIKA TAJI YA USHINDI”[Mathayo 11:28-30][Isaya 1:19]
UWEZA NA NGUVU ZAKE AMEZIFANYA KAMILI
Neno la MUNGU katika kitabu cha Isaya 40:29-31, linaleta uhakika na kutokubadilika kwa wale wanaojinyenyekeza wenyewe.
Nilimuona mtu ambaye alikuwa karibu anafika kwenye kilele cha mlima.Ghafla, akaanza kurudi nyuma taratibu.mtu huyu akaanza kulia akisema, “Hapana ! hapana !Nahitaji neema !”na mara nikasikia sauti kubwa; Na sauti hiyo ilikuwa ikisema, “NEEMA YANGU YAKUTOSHA,KWA KUWA KWA UWEZO WANGU NIMEFANYA KATIKA UDHAIFU WAKO !”[2 Wakorintho12:9]
Hivyo mtu yule akapata nguvu na kuendelea kupanda juu.Nikamuuliza Bwana aniambie mimi maana ya haya.Akasema, “HUYU MTU AMEJINYENYEKEZA MWENYEWE NA HAKUTEGEMEA UWEZO AU NGUVU ZAKE MWENYEWE.ALILIA KWANGU KWA UNYENYEKEVU.[LUKA 5:11], SITARUHUSU KUANGAMIA KWA SABABU WALITAKA UONGOZI WANGU KATIKA MAISHA YAO”.[Yakobo 4:10].
Bwana akasema, “SABABU YA WENGI WA WATU WANGU KUANGAMIA NI KWA SABABU HAWATAKI MUONGOZO WANGU KATKA MAISHA YAO, HAWATAKI KUWEKA HATUA ZAO KWA NENO LANGU, BALI WANA LINGANIA (justifying) WAO WENYEWE.NITAWAPA NGUVU WALE WANAOTAKA MUONGOZO WANGU NA SIO MIONGOZO YAO.”[Zaburi 119:129-130].
Bwana alinukuu Zaburi 119:105-112.Bwana YESU alisema, “NENO LANGU, NENO LANGU, NENO LANGU; SITALIPUNGUZA AU KULIFANYIA UTANI.!” Zaburi 119:131-136.Bwana YESU alisema, “WAAMBIE WATU WANGU WAVAE SAWA SAWA NA NENO LANGU, KWA SABABU WENGI WAO WASIO TAYARI KUVAA SAWA SAWA NA NENO LANGU WAO SI WATII NA HAWATAKI MUONGOZO WANGU.MIOYONI MWAO KUMEJAA UOVU WA FIKRA NA KUZIDI KUUPENDEZA MWILI,WAMEKOSEA KUDHANI WANANIPENDEZA MIMI.”
JE UMESHATUBU NA KUTOKA KWENYE DHAMBI ZAKO ?
Kama bado u mdhambi ni vyema utubu sasa ili uokolewe.Bwana alinichukua mimi nakunipeleka sehemu nikatazama niliona hali kiroho ya wadhambi, Niliona watu wasio hesabika wote wakiwa wamefungwa na mapepo; Minyororo na vifungo walivyofungiwa vilivyotumika kuwafunga hao watu ilikuwa kubwa sana.Mapepo yaliokuwa yakiwatesa walikuwa wakubwa ;makadirio ya urefu wa futi 200 hadi futi 1000 !.Hao walikuwa wakitumia mapanga kukata ndimi zao, na kilio cha uchungu kiliwatoka waliokuwa wakiteswa !.Kibaya zaidi wakijikuta kushindwa kutoka ; kwa sababu hawakutubu dhambi zao katika nyanja ya umwili(physical realm)[Yohana 3:18-20].Baadhi wana vichwa 8 katika mwili mmoja, baadhi wana pembe katika pua ,na baadhi yao alikuwa wakitembea kwa kutumia vichwa vyao !, hao ndio mapepo wanaohusika na dhambi.
Wanaitwa “watawala wa giza la dunia”,Nilihitaji maelezo kutoka kwa Bwana ili aniambie mimi maana yake.Bwana akasema, “HAO WATU NI WADHAMBI NI ENDAPO TU WATAPOTOA MAISHA YAO KUNIPA MIMI LASIVYO HAWAWEZI KUKWEPA SEHEMU HII YA ADHABU.” [Yohana 3:3].Tafadhali tubu sasa na utoe maisha yako kwa YESUKRISTO....kama sivyo upo katika mateso na uchungu mkubwa kiroho !.
Kama bado u mdhambi ni vyema utubu sasa ili uokolewe.Bwana alinichukua mimi nakunipeleka sehemu nikatazama niliona hali kiroho ya wadhambi, Niliona watu wasio hesabika wote wakiwa wamefungwa na mapepo; Minyororo na vifungo walivyofungiwa vilivyotumika kuwafunga hao watu ilikuwa kubwa sana.Mapepo yaliokuwa yakiwatesa walikuwa wakubwa ;makadirio ya urefu wa futi 200 hadi futi 1000 !.Hao walikuwa wakitumia mapanga kukata ndimi zao, na kilio cha uchungu kiliwatoka waliokuwa wakiteswa !.Kibaya zaidi wakijikuta kushindwa kutoka ; kwa sababu hawakutubu dhambi zao katika nyanja ya umwili(physical realm)[Yohana 3:18-20].Baadhi wana vichwa 8 katika mwili mmoja, baadhi wana pembe katika pua ,na baadhi yao alikuwa wakitembea kwa kutumia vichwa vyao !, hao ndio mapepo wanaohusika na dhambi.
Wanaitwa “watawala wa giza la dunia”,Nilihitaji maelezo kutoka kwa Bwana ili aniambie mimi maana yake.Bwana akasema, “HAO WATU NI WADHAMBI NI ENDAPO TU WATAPOTOA MAISHA YAO KUNIPA MIMI LASIVYO HAWAWEZI KUKWEPA SEHEMU HII YA ADHABU.” [Yohana 3:3].Tafadhali tubu sasa na utoe maisha yako kwa YESUKRISTO....kama sivyo upo katika mateso na uchungu mkubwa kiroho !.
KITABU CHA ADHABU
Tazama niliona kitabu kikubwa na pepo kubwa lilikuwa limekaa kwenye enzi iliyo onekana mbaya sana ,alikuwa kamanda wa wote watawala wa giza la dunia.Alifungua kitabu na kusema, “acha wanywe asidi” na wale mapepo walitii sauti yake, wakawapa watu wote waliokuwa wamefungwa chini wanywe asidi.Miili ya watu hao ikaanza kuyeyuka na kupasuka vipande vipande, ndipo ikaja tena katika hali ya kawaida.Watu walikuwa wakilia kwa uchungu, lakini Bwana akasema, “NILIWAUMBA HAWA WATU KWA UTUKUFU WANGU, LAKINI WAMENIKATAA MIMI, HATA HIVYO NITAMUOKOA YEYOTE ATAYENIKUBALI MIMI KAMA BWANA NA MWOKOZI !.” [ Matendo ya mitume 17:30-31].Nilijawa na hasira kwasababu wale mapepo walikuwa wakiwatenda ubaya sana, wabaya sana.Waliwakejeli wale walioumbwa na MUNGU kwa utukufu Wake.Katika ulimwengu wa kimwili ni watu waliokataa kweli na walijiruhusu wenyewe kudanganywa.[Wagalatia 5:7-8]
DADA AKINTOLA
Niliona dada, jina lake ni Akintola.Pamoja na kuwa sijawahi mjua kabla, Nilimuona akiwa katika machungu makubwa.Alikuwa akilia kwa uchungu kwa kadri mapepo yalivyokuwa yakimtesa kwa kutumia vifaa kutoa meno yake.Hao mapepo walimwambia, “wewe mpumbavu, hukutaka kuukubali Kweli, hivyo nitaendelea kukuumizaa wewe !” Ndipo nikamuona mwanadada huyo duniani.Niliona dada mmoja mkristo alikuwa akimuhubiria injili, lakini Akintola alisema, “Acha mimi nifurahie maisha yangu , siko tayari kuokoka .”[1 Wakorintho 15:50][1 Wakorintho 15:10].
DADA CHRISTIANNAH
Niliona mwanamke mwingine, jina lake ni Christiannah, na sikuwahi kulijua jina hilo hapo kabla.Alikuwa mwasherati, mapepo yalikuwa yakimtesa yeye kwa hasira kali sana na huku yakisema, “Unadhani una hekima?, wewe ni mwimba kwaya! Unaongea hocus-pocus(unena kwa lugha kwa uongo) ili watu waseme umempokea Mfariji(Roho mtakatifu), na huku ni kichaa na mpumbavu !”.Hao mapepo walikuwa wakitumia moto kumchoma yeye huku bado akiwa hajafa.Walitumia vitu vikubwa kugonga kichwa chakena kichwa chake kilivunjika katika vipande vipande,tuu akawa tena vilevile.Huyu dada alikuwa bado yuko hai duniani anaishi.[1 Wakorintho 6:9]
KIRI DHAMBI ZAKO NA UACHE NAYE YESU ATAKUOKOA.
DHAMBI ZA SIRINI
Niliona makundi ya watu walikuwa wamefungwa chini.Hawa ni wakaka kwa wadada ndani ya kanisa nao wakijichua(masturbation), usagaji(lesbianism),na ushoga.Walikuwa wapo katika uchungu mkubwa kiroho, mapepo waliwamwagia asidi miili yao na walitumia mikuki kuwatesa.Baadhi ya mapepo walitumia mikia yao kuwapiga.[Luka 8:17].Bwana akaniambia mimi, “WAKO KATIKA BONDE LA UHARIBIFU ! WAAMBIE WATUBU KAMA ILIVYO NITAHUKUMU KILA SIRI YA MTU.”[WARUMI 2:16][WAEBRANIA 4:13].
Niliona makundi ya watu walikuwa wamefungwa chini.Hawa ni wakaka kwa wadada ndani ya kanisa nao wakijichua(masturbation), usagaji(lesbianism),na ushoga.Walikuwa wapo katika uchungu mkubwa kiroho, mapepo waliwamwagia asidi miili yao na walitumia mikuki kuwatesa.Baadhi ya mapepo walitumia mikia yao kuwapiga.[Luka 8:17].Bwana akaniambia mimi, “WAKO KATIKA BONDE LA UHARIBIFU ! WAAMBIE WATUBU KAMA ILIVYO NITAHUKUMU KILA SIRI YA MTU.”[WARUMI 2:16][WAEBRANIA 4:13].
WADHAMBI WOTE.
Wadhambi wote wapo katika maumivu makali sana kiroho.Tafadhali tubu na uokolewe.Kumbuka kuwa mapepo yanajua Ukweli.Katika ulimwengu wa kimwili wako vyema katika wanajidhanisha na kudanganya....hawataki wewe ujue Ukweli!, Na huku bado unayo nafasi ya kuujua ukweli, tafadhali mpokee YESUKRISTO katika maisha yako,Atakuokoa wewe ....[2 Petro 3:9]
UTAKUWA HURU KWELI KWELI !
Bwana alisema, “TAZAMA WALE, MWANAGU!, SITABADILI NENO LANGU;YEYE ATAYEKUJA KWANGU ATAOKOLEWA.”[Matthew 9:6-8][Yohana 5:24] na tazama, nilionakitu cha ajabu; Niliona watu katika wale waliofungwa chini wakaanzakutoka na kuwa huru !,Mapepo yalikuwa hayawezi kuja karibu yao.Nao hao watu wakatoweka kutoka kwenye hiyo sehemu!,Nikapaza sauti, “Halleluya !o Bwana, tafadhali niambie maana yake!”.Bwana akasema, “YEYE ANAYEKUJA KWANGU NA KUNIPOKEA MIMI KAMA BWANA NA MWOKOZI ATAKUWA HURU KWELI KWELI!”[Yohana 8:16],Mara wakafunguliwa na mwonekano wao ukabadilika na kuwa mzuri usiokuwa wakuelezeka![Zaburi 90:17][2 Wakorintho 5:17].Kama utampa maisha yako YESUKRISTO sasa, utakuwa huru na utaachiliwa kutoka kwenye vifungo VYOTE na kuwa KIUMBE KIPYA.
NYUMBA YA BOB
Bwana akanichukua mpaka sehemu mbinguni, na nikaona nyumba nyingi kubwa na nzuri sana.Bwana akasema, “HIZI ZINAMILIKIWA NA WALE WANAOVUNA WATU KUWAPELEKA KWENYE UFALME WANGU, WALE WANAOWAONGOZA WATU KWENYE NJIA NYEMBAMBA”.Nilimwambia, “Bwana, Nataka nione nyumba ya BOB” (Ni meneja wa tovoti za kikristo /a Christian website manager).Bwana akasema, “MWANANGU, NJOO UJE UIONE JINSI ILIVYO NZURI MALAIKA WALIVYOIJENGA !” na Tazama, nikaona nyumba kubwa na nzuri , ilikuwaikipambwa kwa maua mazuri yasio elezeka !(Nilikuwa na furaha sana kwa sababu nilitamani kuona kabla sijaonana na YESU mara ya pili.)
NYUMBA YA MCHUNGAJI W.F KUMUYI
Na nilimwambia Bwana, “Bwana hujanionyesha nyumba ya mchungaji w.f Kumuyi.”Bwana akasema “NI MTUMISHI WANGU NA MARA ZOTE ANADAKA MAONYO YANGU !, LAZIMA NIKUONYESHE ILI UJUMBE UMFIKIE YEYE PIA !” Niliona nyumba ya mchungaji W.F Kumuyi; Nyumba yake ilikuwa ndefu lakini bado alaika waliendelea kuijenga.Nyumba ya mchungaji W.F Kumuyi haiko mbali na nyumba ya Mchungaji E.A adeboye.
NYUMBA YA MCHUNGAJI PAULO RIKA.
Hapo ndipo nikamwambia Bwana, “Tafadhali naomba neema ya kuona nyumba ya mchungaji Pauli Rika (Holiness revival movement)” naye Bwana akasema “MWANANGU,ULIZA NA UTAONYESHWA....NJOO UONE”, Bwana akaonyeshankwenye nyumba na akasema, “HII NDIO NYUMBA YA MCHUNGAJI PAULI RIKA !” Niliona nyumba kubwa, ilikuwa nzuri sana na bado malaika walikuwa wakiendelea kujenga; na mmoja wa malaika alipiga kelele “VIZURI KAZI NZURI”, malaika akaanza kupamba ile nyumba kwa maua, na madini na kwa vitu vingine vingi vizuri.
JESHI LA BWANA
Bwana akasema, “MWANANGU, NIMEANDAA JESHI LANGU MWENYEWE, NA NITATUMIA NGUVU ZANGU ZOTE KWALO, NA WATAOKOA WATU WENGI.WATATOA MAPEPO NA KUWEKA HURU WAFUNGWA, WATATANGAZA USHAURI WANGU WOTE!, NITAWATUMIA WATOTO WADOGO VIKUBWA; NITATUMIA VIJANA WENGI KWA UTUKUFU WANGU ! ,KILA MTU ATATANGAZA MIMI NI BWANA WAMABWANA;........NJOO UJIONEE!.
Tazama niliona jeshi kubwa, na wengine wanaonekana kama wa miaka minne(4), walikuwa tayari kwa kazi .Nikasikia sauti kubwa ikisema, “NANI NIMTUME ?” ndipo hilo jeshi lote la Bwana likanyanyuka na panga zao likipiga kelele , “TUTUME SISI, TUTAKWENDA !”(Isaya 6:8-10) ndipo Bwana akaanza kutabasamu, siwezi elezea jinsi tabasamu lake lilivyokuwa vizuri !, Bwana akasema, “WAAMBIE WATU WANGU, NIMEWAPA WAO DAKIKA YA MWISHO YA NEEMA ILI WAWEZE KUTUBU WASIANGAMIE, KIMBILIA SASA CHUMBA CHA NEEMA NA UTAOKOLEWA, NENDA NA UWAAMBIE !” [Ufunuo 3:20-22]
Tazama niliona jeshi kubwa, na wengine wanaonekana kama wa miaka minne(4), walikuwa tayari kwa kazi .Nikasikia sauti kubwa ikisema, “NANI NIMTUME ?” ndipo hilo jeshi lote la Bwana likanyanyuka na panga zao likipiga kelele , “TUTUME SISI, TUTAKWENDA !”(Isaya 6:8-10) ndipo Bwana akaanza kutabasamu, siwezi elezea jinsi tabasamu lake lilivyokuwa vizuri !, Bwana akasema, “WAAMBIE WATU WANGU, NIMEWAPA WAO DAKIKA YA MWISHO YA NEEMA ILI WAWEZE KUTUBU WASIANGAMIE, KIMBILIA SASA CHUMBA CHA NEEMA NA UTAOKOLEWA, NENDA NA UWAAMBIE !” [Ufunuo 3:20-22]
---##-Mwisho-##---
Kama uko tayari kumpa maisha yako YESUKRISTO , tafadhali nenda katika magoti yako na uombe sala hii :Bwana YESU, najijua mwenyewe kama mdhambi, najijua nilikuwa katika giza, lakini sasa niko tayari kufanya kile unachotaka mimi nifanye.Tafadhali nisamehe mimi na dhambi zote, nioshe katika bwawa la damu yako,niponye mimi,nipe nguvu mimi,nipe uwezo mimi,nipe nguvu yako juu ya mwili na acha ufalme wako unijie katika maisha yangu.
Andika jina langu katika kitabu cha uzima na kuwe na furaha mbinguni juu ya wokovu wa roho yangu, na nitumie mimi kwa ukubwa zaidi kwa kazi yako katika jina la YESUKRISTO nimeomba ,Ameni.
Kwa shuhuda nyingi zaidi tembelea; www.jasirimbarikiwa.blogspot.com,tafadhali SHARE ujumbe huu ili nyoyo za wengi ziokolewe.