Imeandikwa “ . . . . . . . . . . . . . .
Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu .Hata
sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe
timilifu.”- Yohana 16:23-24.
MUNGU anatuambia tumuombe YEYE kwa kuwa
anao uwezo wakutupa yale tumuombayo.Lakini wengi wetu ,yawezekana hata wewe
waweza kuwa unajiuliza “mbona
nimemuomba MUNGU lakini hakunipa nilichomuomba wala kunijibu chochote !?,”.
Imeandikwa “. . . . . . . . . . . . . . . .
. .; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni”.-Yohana 15:16.MUNGU
anatupa ruhusa yakuomba lolote ili YEYE ayatimiz juu yetu nasi tuweze furahia.
Swali linakuja hapo kwa nini sasa wewe haupati unachokiomba
kwa MUNGU ?. Hapa leo utajua kwa nini hukupata au kupokea kitu
ulichomuomba MUNGU, ama kwa nini HAKUKUJIBU maombi yako.
Sababu tano(5) zinazofanya usipokee unachomuomba MUNGU !
Utagundua kuwa MUNGU ametupa
uwanja mkubwa wakuongea naye na kumuelezea matatizo yetu ili atutatulie ,lakini
kuna sababu ambazo zinafanya MUNGU asitupe yale tunayomuomba.Sababu zenyewe ni
:-
1.KUTOSAMEHE
Maombi ya wengi hayajibiwi kwa
sababu hawaja wasamehe baadhi ya watu katika maisha yao.Imeandikwa“Bali
msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.”-Mathayo
6:15.
Kaa chini jifikirie na uanze kusamehe wote,
waliokutenda vibaya waliokuumiza,waliokusaliti ,waliokuonea,wasamehe hata
waliokukataa kabla ya kuzaliwa kwako,waliokataa kukusomesha samehe wote .Usiseme
nimesamehe ila sitakaa wasahau bali wasamehe toka moyoni mwako na kuwasahau kwa
yale waliyokutendea.
Watu wengi ukimuuliza kama huwa
anasamehe atakujibu “mimi ninasamehe sana na nimeshasamehe wengi lakini kuna
yule kaka aliyenisaliti sitakaa nimsamehe,au anasema nimemsamehe lakini
sitamsahau”. MUNGU
anatusamehe dhambi zetu nakuzisahau,nasi pia twatakiwa kuwasamehe na kusahau mabaya
waliotutenda watu.
Ukweli hiyo si sahihi kwa kuwa MUNGU
husamehe tuu wale wanao “wasamehe sio baadhi ya watu” bali
ni “wale wanaowasamehe watu wote katika maisha yao”.
Waweza kukuta mtu anazunguka huku
na kule kuombewa na watumishi wakubwa na wadogo hata ajiombea sana yeye
mwenyewe lakini hapokei kitu anachomuomba MUNGU kwa sababu kuna baadhi
ya watu hajawasamehe kiukweli.
Imeandikwa“Kwa maana mkiwasamehe watu
makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.” Mathayo 6:14.
Jipime
kama kweli umemsamehe kiukweli kwa kujiiuliza hivi,yule unayedai umemsamehe je ?,unaongea nae
vizuri?,Je?, unaweza kumplekea zawadi!,Je haumkimbii au kujisikia vibaya
unaposikia amefanikiwa zaidi?,au ana habari fulani njema amefanya ?,
Mpaka utapoondoa kipangamizi
chochote kinacho onyesha kutosamehe ndipoi maombi yako yatajibiwa na MUNGU.
2.KUTOONGOZWA
NA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUOMBA
Imeandikwa“Kadhalika Roho naye hutusaidia
udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe
hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.“- Warumi 8:26
Wakristo wanaomba vyovyote na
hata wengine wanafuta tu mkumbo ,bila hata kujua anaomba nini .Tambua kuwa
pasipo kuongozwa na ROHO mtakatifu kuomba, maombi yako yanakuwa hayana nguvu
mbele za MUNGU.
Jiweke huru na uruhusu Roho wa
MUNGU akuongoze katika kuomba. Roho mtakatifu atakukumbusha kuwa unaomba katika
jina la YESU,Roho mtakatifu atakuelekeza kumshukuru MUNGU hata kama wewe huoni jambo
la kumshukuru MUNGU.
Imeandikwa “Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga
juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu,”- Yuda
1:20.
3.KUTOKUMUHESHIMU
MWENZI(mke/mume) WAKO.
Imeandikwa “Kadhalika ninyi waume, kaeni na
wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na
kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe. “-1
Petro 3:7
Unapokwenda kumuomba MUNGU
jichunguze kama mkeo au mumeo ana amani na wewe.Kama hana amani na wewe yaani
kuna ugomvi au hali ya kutokuelewa ilitokea baasi rudi ukarekebishe na
kusameheana naye.
Bila ya kutengeneza na mkeo au mumeo kabla ya kuomba,na
ukaamua kwenda kumuomba MUNGU utakuwa unapoteza muda wako tu.
Kwa kuwa hutaweza pata majibu na
kuomba kwako ukiwa una migogoro/kutokuelewana/mtafaruku na mkeo au mumeo ni
bure tena ni kupoteza muda na nguvu yako.
4.KUTOKUWA NA IMANI.
Imeandikwa “6 Ila na aombe kwa imani, pasipo
shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na
upepo, na kupeperushwa huku na huku. 7 Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa
atapokea kitu kwa Bwana.”-Yakobo 1:6-7
Maana halisi ya imani ni ile hali yakuwa na hakika kuwa
umepata huku katika ulimwengu huu wa mwili haulioni. Uliomba MUNGU gari lakini
hulioni na hujapata kwa kuwa hujaweka imani katika maombi yako.
Kuwa na hakika na vyote
unavyomuomba MUNGU acha mazoea na jiondoe kwenye ile hali ya wasi wasi juu ya
kile unachomuomba MUNGU kwa kujihoji wenyewe kama atafanya au hatafanya.
Tunaweza sema mtu ana imani
kupitia vitu vitatu(3):-
1.Unatenda je ?
2.Unasema je ?
3.Unamtazamo upi ?
1.Unatenda je ?
Imani ina uthibitisho katika
matendo yaani “unatenda je?” kama umemuomba
MUNGU gari basi tengeneza uzio ambao gari uliloliomba kutoka kwa MUNGU litakuja
kaa.
Kama unamuomba mke au mume basi ukishamaliza
kumuomba MUNGU ,nenda dukani kanunue pete yake ya uchumba na ndoa na uitunze kwa
kuwa si muda utampata ili umvishe !.
2.Unasema je ?
Imani ina uthibitisho katika
kusema kwetu kwa kawaida kila siku.Kama umemuomba MUNGU gari basi hutaacha
kusema unapoona gari ingine lolote mtaani hata kuwaambia watu neno lolotelinaloonyesha
una matarajio ya kupokea gari si muda mrefu. mfano:“gari yangu itakuwa
inafanana na hii” au ukiwaambia
watu “gari yangu itakayopewa na MUNGU
itakuwa nzuri kama hii”.
Kama uliomba akoponye ugonjwa
fulani utaanza watu wakikuuliza hata kama hali ni mbaya waambie “naona MUNGU ndio anaifanyia operesheni saivi
kwa hiyo si muda ninapona”
3.Unamtazamo upi ?.
Imani inathibitika pia katika
mtazamo tulio nao.Kama umemuomba MUNGU akupe mke au mume ,je una mtazamo upi
?.Ondoa mtazamo wa dunia kwamba haiwezekani bali weka mtazamo wa ki MUNGU “kwa kuona katika akili yako hii harusi yangu itatia foira kwa uzuri”
ingawa kweli kwa hali halisi kidunia jambo hilo linaonekana haiwezekani.Wewe endelea
kuwa na mtazamo huo na MUNGU atakushangaza kwa kukuinua na kukupa jibu lako
haraka sana.
Kama umemuomba MUNGU akupe afya
njema basi kuwa na mtazamo utapopata afya utakuwa unafuraha kiasi gani na
utamshanga vipi MUNGU.ondoa ule mtazamo wa kishetani unaokwambia wee utakaa
hivi hivi maisha yako yote.
Kiukweli hatupewi kwa kuwa tumemuomba MUNGU, Bali
tunapewa na MUNGU kwa kuwa tuna amini tukimuomba MUNGU anatupa yale tunayo
muomba.Hivyo yatupasa tuwe na imani thabiti katika yote tunayomuomba
MUNGU.
5.TAMAA ZETU
WENYEWE.
Imeandikwa “Hata mwaomba, wala hampati kwa
sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.” -Yakobo 4:3
Unapo ongozwa natamaa zako mbaya
kuomba kaa ukijua hutapata unachokiomba, Mfano: unaomba MUNGU uwe na gari lakini moyoni unajua kuwa
unaomba gari ili uwaringishie/wakukome hapo mtaani jinsi ulivyo juu.
Unatakiwa
uibadilishe hiyo hali kutoka moyoni na kusema nikiipata gari itakuwa ni vyema
kwa kuwa ninavyoenda nayo kazini nikakuwa nawapa lift hawa watu njiani.
Unaomba MUNGU akupe afya njema lakini moyoni unajijua unaomba
afya njema ili uufanye uzinzi vizuri., Badili nia mbaya na kuiweka hii kwa moyoni mwako kuwa ninapopata afya njema
nitaweza kumsifu na kutukuza MUNGU vyema.
Unaomba MUNGU akupe kazi nzuri lakini moyoni unajijua kuwa
unaomba hivyo ili tuu uwaonee watakao kaa chini yako na utakuwa ukipokea rushwa
si mchezo, Badili hiyo nia yako kwa kuwa hutakaa upate toka kwa MUNGU
unachomuomba na nia hiyo ,sasa weka nia kwamba ukiipata hiyo kazi utakuwa mtu
wa haki.
Kwa kuzingatia haya mambo hutakaa uone ombi lako lolote kwa MUNGU kutojibiwa.