Maombi ya ku ufunika mwisho wako hapa duniani kwa damu ya YESU !!


Omba kwa imani "MUNGU uliye hai ,uliyeumba viumbe vyote ,Wewe MUNGU ambaye ni mmiliki wa kila kitu hapa duniani na mbinguni ninakushukuru na kukupa sifa kwa neema yako.Ninakutukuza na kukusifu kwa kuwa wastahili kusifiwa.

Leo hii ninaomba neema yako Mfalme mkuu ,neema ya kumaliza vyema maisha yangu hapa duniani.
imeandikwa " (Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake . . . . . . . . . . . . ." - ufunuo16:15.

Ninaomba rehema zako kwa kuwa wewe MUNGU unajua mwanzo wangu mpaka mwisho wangu,ninakuomba MUNGU wangu uniwezeshe niweze kumaliza vyema kuishi hapa duniani kwa maana ya kumaliza nikiwa na upatanisho wako,

,kumaliza na uchaji wako,kumaliza na utakatifu wako ,kumaliza kuishi hapa duniani nikiwa na kibali chako kuingia mbinguni.

Katika jina la YESU ninahamisha kila vikwazo katika maisha yangu ya kiroho,ninaondoa kila hila za muovu ibilisi katika maisha yangu na katika siku zangu za mwisho hapa duniani,

Imeandikwa " Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; Bali rafiki wa wapumbavu ataumia."-mithali 13:20

Leo hii ninachagua kuenenda pamoja na wenye hekima na nina wakataa kabisa marafiki wapumbavu nisije kuangamia pamoja nao katika jina la YESU.

Nina jitenga na kila aina ya mitego ya marafiki ambao watanisababisha katika siku zangu za mwisho niangamie katika jina la YESU.

Imeandikwa "Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka."-Mathayo 24:13
Mungu wangu naomba uniwezeshe nivumilie mpaka mwisho nami niweze kuokolewa nawe YESU.

Niwe nawe siku zote za maisha yangu kwa msaada wako ee BWANA na unijaze rehema zako na kunitia moyo pale ninapochoka mpaka hata kutaka kukata tamaa !!.
Ni katika jina lako YESU ninakushukuru kwa kunipa zaidi ya nilivyo omba.Ameni

No comments :

Post a Comment

Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...