Jiulize unawatendea nini ?, watu mbalimbali unaowajua au usio wajua hicho ndicho unamtendea MUNGU!.
Haipingiki kuwa kuna kwenda mbinguni kama umemkubali YESU au kwenda kwenye moto wa milele kama umemkataa baada ya kifo.
Haipingiki kuwa kuna kwenda mbinguni kama umemkubali YESU au kwenda kwenye moto wa milele kama umemkataa baada ya kifo.
Imeandikwa “32 na mataifa yote watakusanyika mbele
zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi;
33 atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na
mbuzi mkono wake wa kushoto.
34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono
wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa
tayari tangu kuumbwa ulimwengu;
35 kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa
chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha;
36 nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa,
mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia.
37 Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema,
Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha?
38 Tena ni lini tulipokuona u mgeni,
tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika?
39 Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au
kifungoni, tukakujia?
40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin,
nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo,
mlinitendea mimi.
41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake
wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele,
aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;
42 kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe
chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe;
43 nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa
uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama.
44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni
lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u
mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie?
45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia,
Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.
46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu
ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.”-mathayo 25:33-46.
Anaposema nilikuwa uchi
mkanivisha nilikuwa na njaa mkanilisha
na kadhalika,Hayo yote ni
matendo ya upendo na Hii inamaanisha
kuwa Upendo wa kweli ndio
utamfanya mtu aweze kwenda mbinguni,
Jiulize unamtendea nini jirani yako,nduguyo,rafiki yako,hata adui wako
?,Chochote unachomtendea mtu yeyote hata uwe humfahamu ndicho hicho unamtendea
YESUKRISTO.
Imeandikwa “40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin,
nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo,
mlinitendea mimi.”-Mathayo 25:40
Je kuna baadhi ya watu
unawadharau ?, Jua unamdharau YESUKRISTO au kunabaadhi ya watu unawaona sii
kitu yaani wewe uko juu yao jua unamshusha YESU.
Imeandikwa “akasema, Amin, nawaambia,
Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.”-
Mathayo 18:3
Waweza jiuliza inamaanisha nini ?
Watoto hawatunzi chuki,hawa hesabu mabaya ya mtu, watoto ni wepesi wa kusahau mabaya waliotendewa ,hawahesabu hata mazuri waliowatendea watu . . . .hizi ni baadhi tuu ya tabia ambazo wanazo watoto ambazo MUNGU pia anataka tuwe nazo ilituu kuweza kumpenza YEYE.
Tunatakiwa tuwe na upendo wa kweli ,upendo wa vitendo kutoka moyoni.Imeandikwa "Zaidi ya hayo yote jivikeni
upendo, ndio kifungo cha ukamilifu" Wakolosai 3:14
No comments :
Post a Comment
Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!