Somo:Huduma
iliyo katika umoja katika KRISTO YESU -part 4
Walengwa:Watumishi/Rafiki
za MUNGU
Neno: “Kwa maana wako watatu washuhudiao mbinguni,
Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja.” 1 Yohana 5:8
Theme:Tunategemeana
ili utukufu wake MUNGU uonekane maishani
mwetu.
Katika kuitenda kazi ya
BWANA tunategemeana kama watumishi, na kila mtumishi wa BWANA amepewa kazi yake
na BWANA na atapoimaliza atalipwa kwa hiyo.
Hivyo hakuna haja ya kuwa na udini badala ya UKRISTO kwa
kuwa yeye MUNGU huwa katika umoja katika kuzitenda kazi zake.
Imeandikwa“Maana
hapo mtu mmoja asemapo, Mimi ni wa Paulo; na mwingine, Mimi ni wa Apolo, je!
Ninyi si wanadamu?” 1 Wakorintho 3:4
Utaona hapo Apolo na
Paulo hawa wote ni watumishi waliotumiwa
na BWANA lakini tatizo ni kwamba wakristo wanaoongozwa wameshaweka umoja katika kuutetea
udini(u-Apolo na uPaulo) badala kuutetea
u-YESUKRISTO.
“Basi Apolo ni nani? Na
Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu kama BWANA
alivyompa.” 1 Wakorintho 3:5
Kutokuwa na umoja na
ushirikiano na huduma zingine ni kubaya
sana na kuna maanisha kwamba unaweza wewe pekee/ninyi pekee yenu bila msaada wa
mtu yeyote kutoka kanisa lingine au huduma ingine.
Kitu ambacho sii kweli
kabisa ,kwa kuwa ni kweli kabisa tunamtegemea MUNGU kutusaidia yeye pekee
lakini mara nyingine hutusaidia
watumishi wake kupitia watumishi wengine.
Unapopata msaada wa
kuhudumiwa kama mtumishi wa MUNGU kutoka kwenye kanisa lingine au huduma ingine
haimaanishi wao ni wazuri sana kuliko wewe.
Kumbuka YESU alibatizwa
na Yohana kutoka hapo kila mtu akaendelea na huduma yake.Yohana alikuwa huduma
yake na YESU alikuwa na huduma yake lakini ili mbidi Yohana kumbatiza YESU.
je ?kama hatutokuwa na shirikiano na umoja
tutawezaje kufanikiwa vyema katika kuhudumu vyema.
Imeandikwa“Mimi
nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni MUNGU.” 1 Wakorintho 3:6
Sisi tuu wamoja.Na kama
tu wa moja basi tuwe na umoja kama BABA yetu aliye mbinguni alivyo na umoja
yaani MUNGU baba,MWANA na ROHO MTAKATIFU.
No comments :
Post a Comment
Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!