Mambo yanayofanya kushindwa vita yako
Kuna mambo
ambayo yanaweza kuwa chanzo cha kushindwa katika vita unayopitia.Mtu anapo acha
kutenda sawa sawa na matakwa ya Mungu, mtu huyo anakuwa anajiendea katika njia
ya kushindwa.
i.Kushindwa kungoja kutoka kwa
Bwana.
Wokovu wetu katika vita yoyote
tuipitiayo inategemea msaada kutoka kwa Bwana. Imeandikwa “Naam, wakungojao hawataaibika hata mmoja; Wataaibika watendao uhaini
bila sababu.” Zaburi 25:3.
Tunaposhindwa kungoja mpaka kukata tamaa hata tusimuulizie tena Mungu kwa habari ya vita yetu,
tunapoteza muujiza wetu.
Imeandikwa “Daudi mwenyewe alisema, kwa uweza
wa Roho Mtakatifu, Bwana alimwambia bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume,
Hata niwawekapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako.” Marko 12:36
Ni ahadi ya
Mungu kusaidia pale tunapopitia vita ,misuko suko au mambo magumu
kimaisha.Lakini pia inabidi kuwa na sabira ili kupokea msaada mkuu kutoka kwa
Bwana maana hacheleweshi wala hawaishi.
Bwana huonyesha njia sahii ya kuendea njia ya kushinda kipindi mtu
anapopitia vita katika maisha yake, kipindi anapopitia matatizo makubwa lakini
yaitaji kutokata tamaa kumngoja Bwana kwa maombi bila kuchoka.“Ana
heri mtu yule anisikilizaye, Akisubiri sikuzote malangoni pangu, Akingoja penye
vizingiti vya milango yangu.” Mithali 8:34
ii.Maungamanisho na ushirika mbovu
Kama
mtu anauhusiano mkubwa na watu waovu au makundi mabaya yasio mtii Mungu, Basi
mtu huyo anajiwekea nafasi kubwa ya kushindwa. kwa kuwa watu hao wanauwezo
mkubwa wa ushawishi katika kutenda uovu kitu ambacho ni kinyume na sheria ya
Bwana.
Imeandikwa “Usifanye
urafiki na mtu mwenye hasira nyingi; Wala usiende na mtu wa ghadhabu nyingi;
Usije ukajifunza njia zake; Na kujipatia nafsi yako mtego” mithali 22: 24-25
Jaribu
kujenga urafiki na watu ambao wana hekima ya Mungu, jaribu kuwa karibu kujiunga
na kikundi cha kujifunza neno la Mungu kanisani badala ya kuwa na makundi mengi
ya watu ambao hawamuamini Mungu kwa kuwa siku ya taabu yako hawata weza
kukusaidia chochote.
Mtu
anapokuwa akishirikiana na makundi yasiyo muamini Mungu kwa ukaribu sana, mtu
hyo anaweza kushawishiwa kuiacha njia ya Bwana na hao watu kiraisi sana.
Imeandikwa
“Ndipo
Sauli akamwambia Samweli, Nimefanya dhambi; . . . . . . . . . . .kwa sababu
naliwaogopa wale watu, nikaitii sauti yao” 1 Samweli
15:24.
Sauli alitii sauti ya watu na sio sauti ya Mungu kwa
kuwa watu wengi alio ambatana naye
walikuwa hawamtii Mungu hata wakaweza kumshawishi kumuasi Bwana.
Imeandikwa “Enenda pamoja na
wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; Bali rafiki wa wapumbavu ataumia.” mithali13:20 .Tunapokuwa
na ushirika na wenye hekima nasi tunakuwa na hekima, Bali tunapojiungamanisha
na watu wasio mtii Mungu tunajiwekea kushindwa.
iii.Kusahau matendo makuu ya
Bwana aliyowahi kukutendea
Kusahau
matendo makuu ya Bwana aliyokwisha kutkutendea kunafanya ushindwe katika vita
upitiayo.Mtu anapopitia hali ngumu ya shida halafu akasahau mambo ambayo Mungu
aliwahi kumtendea zamani ,basi mtu huyo hukusa imani na Mungu na kushindwa.
Wana wa israeli
walikuwa wakisahau matendo makuu ya
Mungu katika safari yao kwamba ndiye Mungu
Yeye aliye wawezesha kuvuka bahari ya shamu na akawauwa adui zao.
“ Yale maji yakarudi yakafunikiza magari na
wapanda farasi, hata jeshi lote la Farao lililoingia katika bahari nyuma yao;
hakusalia hata mtu mmoja.
Lakini wana wa Israeli wakaenda katika nchi kavu katikati ya bahari; na
hayo maji yalikuwa ni kuta upande wao wa kuume, na upande wao wa kushoto.
Ndivyo Bwana alivyowaokoa Israeli siku ile
mikononi mwa Wamisri; Waisraeli wakawaona Wamisri ufuoni kwa bahari, wamekufaa” kutoka 14:28-30
Imeandikwa “wana
wa Israeli wakawaambia, Laiti tungalikufa kwa mkono wa Bwana katika nchi ya
Misri, hapo tulipoketi karibu na zile sufuria za nyama, tulipokula vyakula hata
kushiba; kwani mmetutoa huko na kututia katika bara hii, ili kutuua kwa njaa
kusanyiko hili lote.” Kutoka 16:3
Wana wa
israeli walitendewa mambo makuu sana na Mungu katika kutolewa nchi ya utumwa misri,
lakini pamoja na ishara zote ambazo Mungu alizokuwa akiwatendea,
wao walisahau
makuu yote ambayo Mungu aliwatendea, kipindi tuu wakutanapo na vita na kuanza
kumnungunikia musa kwamba ni bora angewaacha misri waendelee kuwa watumwa
kuliko kupambana na vita .
Mungu
hapendi tusahau jambo lolote alilotutendea maishani mwetu, kwa kuwa tunaposahau
inapelekea kutoamini uweza wake Mungu.
Mungu alichukizwa na tabia za wana wa
israeli za kusahau matendo aliyowatendea “Bwana akamwuliza Musa, Je! Watu hawa watanidharau
hata lini? Wasiniamini hata lini? Nijapokuwa nimefanya ishara hizo zote kati
yao.
Nitawapiga kwa tauni, na kuwaondolea
urithi wao, nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, kisha yenye nguvu kuliko
wao.” Hesabu 14:11-12 .
Unaweza kujiuliza ni mambo gani mimi
Mungu aliyonitendea makuu?, ukaona kama hakuna !!.
Ila ukweli ni
mambo mengi makuu sana aliyokutendea Bwana.Kama ukidhani hakuna, kumbuka hata
wewe kuwa hai ni jambo kubwa ambalo Mungu amekutendea kwa kuwa wapo ambao hawajaweza
kufikia umri wako wakiwa hai,
Kwa hiyo katika shida yako mkumbuke Mungu kwa
hilo na uweke imani kuu kwa kukushindia vita yako ulio nayo sasa.
Kama
vita yako ni kupata ada ya wanao, basi kumbuka kuna watu wasio na watoto
lakini Mungu amekuwezesha wewe kuwapata hilo ni jambo kuu .Kwa hiyo katika
shida yako mkumbuke Mungu kwa hilo na uweke imani kuu kwa kukushindia vita yako
uliyo nayo sasa.
Unapopatwa
na vita yeyote ,magumu yoyote yale usisahau hata jambo moja ambalo Bwana
aliwahi kukutendea kwa kuwa kupitia hilo jambo ndilo itakuwa shuhuda yako ya
kukupa nguvu kuona hata vita ambayo unaipitia sasa yeye Mungu anaweza kukuokoa.
upendo wa awali wa Yesu
kushindwa kukumbuka Yesu ndiye aliyekushindia mambo ya nyuma na kusahau ijinsi
alivyokupigania.
No comments :
Post a Comment
Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!