Kumpokea YESU kuna faida kubwa kuliko chochote


Maombi ya kushinda vita yako

Ndugu kabla ya kufanya maombi haya yatakayo kuwezesha kushinda vita yako, yatakayo kutenganisha na wanao onewa, maombi yatakayo rudisha kile ambacho adui(shetani) amekiiba maishani mwako.
Ili kuomba vizuri maombi haya ya kushinda vita yako ni lazima uwe una YESU, kwa kuwa wale waliokuwa na YESU ndiyo pekee waliopewa mamlaka na nguvu za katika kuharibu kazi za ibilisi (shetani).

Ni jambo jema zaidi kuwa na YESUKRISTO ili atawale na aongoze maisha yako katika kusudi la mema yake aliokuwekea katika dunia hii na kukupa kuishi milele hata baada ya kufa kwako. Imeandikwa “YESU akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;” Yohana 11:25
Mpendwa kuna njia moja tuu ya kwenda mbinguni, kuna njia moja tuu ya kuishi milele nayo ni kumkubali Yesukristo katika maisha yako. Imeandikwa  “YESU akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.” Yohana 14:6

Kumkubali YESUKRISTO katika maisha yako ni kukubali kuishi kama yeye apendavyo yaani kutenda yale yoote akuagizayo kupitia neno lake.Imeandikwa “wale ambao kwa saburi katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutokuharibika, watapewa uzima wa milele;” Warumi 2:7.

Mwanzo wa kumpokea YESU
Omba sala hii fupi kwa imani iwe mwanzo kumpokea YESU, Kwa kumpokea YESU atakuongoza kushinda kila gumu unalopitia, kila aina ya vita katika maisha yako atakuwezesha kuishinda.
Mbali na kukushindia katika Vita yako na magumu upitiayo, YESU atakuokoa na hukumu ya moto wa milele na kukuweka katika uzima wa milele. “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” Yohana 3:16.

Omba sala hii fupi kwa imani

“ MUNGU uliyeniumba mimi na vyote vilivyomo humu duniani na mbinguni nakutukuza, pia ninakushukuru kwa upendo wako mkuu katika maisha yangu,
Nimeamua leo nikufuate wewe BWANA MUNGU uliyeniumba katika jina la YESU, nakuomba unisamehe maovu yangu yote katika jina la YESU, nakuomba unipe neema yako ya kuishi katika njia ikupendezayo wewe YESU mpaka siku ya mwisho wa maisha yangu.Asante YESU kwa kuniokoa leo hata milele.”

Wewe sasa umeshakuwa kiumbe kipya kwa kuwa umempokea KRISTO kwa sala fupi hiyo kama neno lake lisemavyo “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.” 2 Wakorintho 5:17.

No comments :

Post a Comment

Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...