Somo:tuu
wamoja katika YESU KRISTO -part 3
Walengwa:Watumishi/Rafiki
za MUNGU
Neno: “Kwa maana wako watatu washuhudiao mbinguni,
Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja.” 1 Yohana 5:8
Theme:Ulinzi wa jina la
YESU juu yautendaji wa utukufu WAKE.
Jina la YESU
linatulinda sisi kama wakristo ili tuu tuwe na umoja katika yeye
YESU.Imeandikwa“. . . . . . . . . . . . . . . . . Baba mtakatifu, kwa jina lako
ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.” Yohana 17:11
Utukufu huo wa MUNGU
ambao ametupa sisi kama wanawe hauwezi kuonekana katika maisha yako kama hatuko
ndani yake MUNGU.
Kuishi ndani ya MUNGU
ni kuishi kama MUNGU atakavyo,anasema utii amri zake zote “Lakini mjibidiishe sana
kuzifanya amri na sheria, ambazo Musa, mtumishi wa BWANA,
aliwaamuru, kumpenda BWANA, MUNGU wenu, na
kwenenda katika njia zake zote, na kuzishika amri zake, na kushikamana na yeye,
na kumtumikia kwa moyo wenu wote na nafsi yenu yote.” Yoshua 22:5
Mkristo aliye na umoja
hudadisi kwa kujiuliza , “je huyu mtu
anamjua YESU ?,ametoka katika kanisa linalo mjua YESU.
Kama
ni kauli za mkristo aliye na umoja husema ,Sisi kama watu ambao tuna YESU huwa
hatufanyi hivyo!.”
Lakini yule Mkristo
asiyekuwa na umoja hudadisi kwa kuuliza , “Je
mtu huyu ana mjua mchungaji wetu ?,ametokea kanisa gani ?,
ametokea
huduma gani ?. Kama
ni kauli za mkristo asiye na umoja husema “Sisi kwenye kanisa letu huwa
hatufanyi hivyo.”
Kama tukiwa wamoja kama
watumishi wa MUNGU hatutabaguana kwa kusema labda hutachangia hudumaa hii
,nakusema mimi ntakuwa nachangia huduma hii ingine pekee yake.
Tukiwa na umoja
hutaweza kusikia mtumishi mmoja anamsema mtumishi mwenzake kwa lolote lile,Kwa
kuwa akianguka mtumishi mmoja ni sawa na tumeanguka wote kwa kuwa tu
wamoja,hivyo tutakuwa katika hali ya kumsaidia na sii kumsema vibaya au kumuacha
apotee na kuzidi kuaibika.
Tunaposhindwa kuwa na
umoja kama watumishi wa BWANA tunakosa kuiga ule ukamilifu wa MUNGU.
Sisi tu wa moja.Na kama
tu wa moja basi tuwe na umoja kama BABA yetu aliye mbinguni alivyo na umoja
yaani MUNGU baba,MWANA na ROHO MTAKATIFU. Nao ulinzi wa jina la
YESU juu ya utendaji wa utukufu wake MUNGU utadhihirika zaidi katika maisha
yetu.
No comments :
Post a Comment
Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!