Katika hizi siku za mwisho ,Wakristo
ambao wataitikisa dunia kwa injili sii tu kwa kuwa ni wanamaombi bali pia wenye
hekima ya MUNGU katika kuitenda kazi yake.Kwa kuwa hekima ni chachu ya
kuukomboa wakati , Imeandikwa katika Wakolosai 4:5- Enendeni kwa hekima mbele yao
walio nje, mkiukomboa wakati.Kitu ambacho ungekifanya (labda nikujenga
) kwa kutumia hekima ya MUNGU kwa muda
wa miaka miwili.Kitu hicho hicho kinaweza kugharimu miaka kumi na tano(15)
kikifanyika pasipo hekima ya MUNGU. Mhubiri 2:13-Ndipo nilipoona ya kuwa kweli
hekima hupita upumbavu, kwa kadiri nuru ipitavyo giza;
Maombi ya kumuomba MUNGU hekima yake
katika maisha yako hasa katika siku hizi za mwisho.
Anza Maombi “MUNGU wewe uliye NIKO ambaye NIKO wewe uliyeniumba mimi na vyote
vilivyomo duniani ninakushukuru kwa wakati huu ,nakutukuza MFALME wa wafalme
nakusifu kwa ukuu wako,nakujia leo nikiomba unisamehe dhambi zangu zote
nilizozifanya kwa siri na kwa uwazi uniokoe na kunifanya mpenzi WAKO BABA
MUNGU.
Nakuomba unipe hekima yako MUNGU katika siku hizi za mwisho
,kama ilivyoandikwa katika Ayubu 12:13-Hekima
na amri zina yeye Mungu; Yeye anayo mashauri na fahamu.
Naomba unipe hekima ya kufanya maamuzi mazuri ninapo pitia
magumu ,unipe hekima ninapo ongea,uniunganishe na watu wako wenye hekima kutoka kwako kama
ilivyoandikwa katika Mithali 13:20 Enenda pamoja na
wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; Bali rafiki wa wapumbavu ataumia .Katika
jina la YESU ninajiungamanisha na watu wenye hekima ya MUNGU katika maisha yangu.Imeandikwa
1 Wakorintho 2:5 ili imani yenu isiwe katika
hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu.Ninaikataa hekima
ya dunia hii hekima ya kujivuna ninaikataa katika jina la YESU ,ile hekima
ambayo inaonekana kama yatoka kwako lakini kumbe haitoki kwako ninaikataa
katika jina la YESU.Imeandikwa katika Isaya 5:21-Ole wao walio wenye hekima katika
macho yao wenyewe, na wenye busara katika fikira zao wenyewe!.BABA MUNGU ninakataa hekima kama hiyo
itayonipelekea kuangamia bali ninajiunganisha na hekima yako kuu kutoka juu
mbinguni itakayonifanya niishi vyema katika uhai siku zote za maisha yangu
katika jina la YESU ,amen.Nakushukuru MUNGU kwa kunipa zaidi ya niombavyo jina
lako lihimidiwe siku zote kwa hekima uliyoiweka katika maisha yangu siku hii ya
leo.
No comments :
Post a Comment
Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!