Somo:Sisi
tuu wamoja -part 2
Walengwa:Watumishi
wa MUNGU
Neno: “Kwa maana wako watatu washuhudiao mbinguni,
Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja.” 1 Yohana 5:8
Theme:utukufu wa MUNGU tuliopewa.
Tunajua kuwa ni kweli
YESU ametupa ule utukufu aliopewa na BABA MUNGU kwa kusoma “Nami utukufu ule ulionipa
nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja” Yohana 17:22,
Kuwa na Umoja kama
wakristo ni agizo kuu la kufanya ili
utukufu tuliopewa na YESU uweze kuonekana
katika maisha yetu kama wakristo.
Tunatakiwa tuwe na
umoja katika YESUKRISTO na sio umoja katika udini/dini yetu bali umoja katika
YESUKRISTO.
Umoja katika YESUKRISTO
unapingana kabisa na udini, Ingawa ndani ya udini kunaweza kuwepo umoja lakini
umoja huo sii ule umoja katika YESUKRISTO.
Tusipo kuwa na umoja
katika YESUKRISTO kama watumishi wa MUNGU tunafanya utukufu aliotupa MUNGU
asidhihirike sana katika maisha yetu.
Kama hauna umoja katika
YESUKRISTO utashindwa kumsaidia mkristo mwingine kwa kuwa hajatokea katika kanisa/huduma
yako.
Mahali popote ambapo utukufu wa MUNGU ulishuka
haukuacha pakiwa vile vile bali ulileta mabadiliko ama yawe mabadiliko mazuri
au mabaya kwa panapo uovu .
Utukufu wa MUNGU
unaposhuka tuwapo katika kuabudu au ni sifa basi tunajikuta tunatekwa na
kuhama kuanza kunena kwa lugha na hata
kufurahi sana mpaka kulia na kadhalika
Umoja unaozungumziwa
hapa ni umoja katika YESUKRISTO,Umoja katika kuifanya kazi ya YESUKRISTO pasipo
ubaguzi wa kanisa ,huduma ,au mtumishi gani,au eneo atokalo.
MUNGU anatambua umuhimu
wa umoja katika yeye YESU ,ili utukufu aliotupa upate kuonekana.
Sisi tu wa moja.Na kama
tu wa moja basi tuwe na umoja kama BABA yetu aliye mbinguni alivyo na umoja
yaani MUNGU baba,MWANA na ROHO MTAKATIFU.Ili utukufu wake MUNGU ung`ae maishani
mwetu.
No comments :
Post a Comment
Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!