Kuna vita kubwa kuacha tabia mbaya ambazo hazimpendezi MUNGU.Tabia mbaya ambazo
zimejiwekea mazoea katika maisha yetu mpaka zinakuwa na nguvu kana kwamba ni
sehemu ya maisha yetu.
Imeandikwa “ Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei
mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa
kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohon i ”-1 Wakorintho 2:14
Watu wengi wanaokoka na kuanza maisha ya wokovu huku bado
zile tabia zao zamani kabla hawajaokoa zinawafuatilia na kuwasumbua sumbua.
Mfano: labda mtu alikuwa mlevi sana kabla ya
kuokoka basi baada ya kuokoka anaweza
kuwa anajikuta mara kwa mara anajaribiwa kurudia ile tabia ya kulewa.
Baadhi ya tabia sugu kwa watu wengi ambazo zinamchukiza
MUNGU ni
ü
Ulevi
ü
Kusema uongo
ü
Kutukana matusi
ü
Kuangalia picha za uchi
ü
Kupiga punyeto/kujichua
ü
Uzinzi
ü
Uvivu
ü
Hasira
ü
Na n.k
Hakika kuna dawa ya kuacha tabia mbaya iliyokithiri yaani “addiction” na dawa pekee inayoweza
kutatua ni uwepo wa MUNGU
ambao huondoa kiu ya mambo machafu na kuweka kiu ya kutafuta mambo ya Rohoni
zaidi.
anaonekana kimwili kama ameacha lakini
kiroho bado ile tabia anayo na
ndio maana mara nyingi anaweza jikuta
akilala huwa anaota anavuta sigara pia watu kama hao hawakai sana wakiwa
wameziacha tabia hizo bali si muda utasikia amezirudia tena na akizirudia
anakuwa na kiu kubwa zaidi ya awali.
Imeandikwa “Kwa maana watu wa Mataifa wasio na sheria
wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati, hao wasio na sheria wamekuwa
sheria kwa nafsi zao wenyewe.” -Warumi 2:14
Ukweli
ni kwamba uwepo wa MUNGU pekee ndio anaweza kukufutia kiu ya mazoea ya kutenda tabia
mbaya.
Je huo udhihirisho wa MUNGU au uwepo wa MUNGU unapatikana
vipi ?.
Uwepo wa MUNGU unapatikana kwa
kumuomba MUNGU mara kwa mara kwa kuwa uwepo huo huondoa kiu ya dhambi kabisa.
MAMBO
YA KUFANYA ILI UONDOKANE NA TABIA MBAYA INAYOKUSUMBUA
Kila mtu anatabia fulani inayomsumbua ambayo
anatamani imtoke ili azidi kuwa safi mbele za MUNGU na kuweza kumwabudu MUNGU
katika roho na kweli,Yamkini tabia
ambayo wewe inakusumbua ni madawa ya
kulevya,ulevi,uzinzi,pornography,kusengenya,kutukana,au kuhukumu watu.
Haya ni mambo unayotakiwa kuyafanya ili uondokane na tabia
hizo :-
1.Kabla hujaitenda lazimisha kutaka uwepo wa MUNGU.
Pindi unapojisikia hamu ya kutenda ile tabia mbaya
inayokusumbua labda ni kuvuta sigara,madawa ya kulevya au ni uzinzi ,
Basi
wewe jitahidi kabla ya kufanya hiyo
tabia inayokusumbua jitafutie sehemu ya
siri labda ni chumbani na uombe kidogo tuu na ndipo utakapo shangaa kwa kuwa
ukitoka utajikuta huna hamu tena ya kutenda ile tabia mbaya.
Mfano: Kunywa pombe, kuvuta sigara, kutumia madawa
ya kulevya yaani tabia yoyote ambayo ni mbaya
badala ya kukimbilia kuitenda hiyi tabia ,Jiambie kama utani kuwa ngoja
nika Sali kwanza ndipo nitakuja kifanya hiyo tabia mbaya hapo wewe nenda
chumbani kwako sirini uombe MUNGU
uwepo huo unakufanya
uisikie vizuri sauti ya MUNGU kupitia Roho mtakatifu.
Kila tabia mbaya yaani,uzinzi,uasherati ,tamaa mbaya,kuvuta
sigara, madawa, kukasirika, kutukana, kunywa pombe, kusema uongo,
kujichua au
kupiga punyeto . . . . . . . . .tabia zote mbaya huwa zinapewa nguvu na roho za
giza yaani mapepo ilizifanye kazi katika maisha yetu kwa hiyo unapokaribia
uwepo wa MUNGU kwa njia ya maombi ya mara kwa mara baasi hayo mapepo yanayoleta
kiu ya kuendelea na tabia mbaya
yanakimbia.
Na unapokuwa mbali na uwepo wa MUNGU basi mapepo yanaweza kupata
nafasi ya kukuharibu kwa kukupa kiu na hamu kubwa ya kurudia ile tabia fulani
mbaya uliyoiacha.
2.Mara kwa mara unahitajika kumuomba MUNGU juu ya tabia
mbaya uliyo nayo hata kama ulishamuomba.
Imeandikwa “ombeni bila kukoma;Ukweli”
1
Wathesalonike 5:17 .
Usiogope kuomba hata mara kumi(10) kwa siku juu ya tabia ikusumbuayo
kwani ukweli ni kuwa mwanzoni nguvu hiyo inakuwa inafanania na chaji katika simu
,kwa kuwa uwepo huo wa MUNGUunweza kupungua na unaweza ungezaka ,
Uwepo huo
unapopungua sana ndipo hujikuta unatamani kufanya na kuzirudia zile tabia mbaya
za zamani ,hapo ukurudi kumuomba MUGU
tena kuhusu hiyo hiyo tabia na uwepo wa MUNGU unajichaji na kuongezeka kwako
kukuondolea ile kiu ya dhambi.
Hatutakiwi kuacha kuomba kwa ajili
ya tabia mbaya zitusumbuazo kwa kuwa tunapoomba MUNGU hushusha wingu lake ambao
ndio uwepo na kwa huo unafukuza kila pepo wanaoleta kiu za kutenda zile tabia
mbaya katika maisha yako.
“Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba
kwa bidii.. .” Yakobo 5:16
3.Jitenge na mazingira yaliyo rafiki na tabia unayoikataa
Jitenge na mazingira ambayo yanaurafiki
na tabia unayoipinga :Mfano labda unatumia madawa ya kulevya na umeamua sasa unabidi uachane na kundi la marafiki wa
aina hiyo kwa kutokaa karibu na mazingira yao.
Jiondoe kwenye mazungumzo na watu
ambao wanakufanya ukumbuke ile tabia ambayo huipendi.Imeandikwa “Msidanganyike;
Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.” 1 Wakorintho 15:33.
Jitahidi kukaa karibu na watu
wanaokupa moyo wa kuiacha ile tabia mbaya na sio kukaa karibu na wanaokuchukia
na kukucheka kwa uamuzi wako wa kuacha hiyo tabia mbaya.
4.Kiri na
sema mara kwa mara kile tuu unachokipenda kitokee na sio unachokitenda.
Siku zote sema mimi nitaacha hii tabia mbaya inayonisumbua
labda ya kuvuta sigara,ulevi nitaacha umalaya,nitaacha kuangalia picha za
uchi(pornography),nitaacha kupiga punyeto(kujichua/ masturbation),
kiwe
chochote we sema tuu hata kama bado unaendelea na tabia hiyo tabia mbaya wewe
endelea kusema tuu hata kama unasema huku ukiwa huna uhakika kama itakuwa
rahisi hivyo.
Kuna nguvu kubwa katika vinywa vyetu ingawa haionekani kwa macho.“Mauti
na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.”-Mithali
18:21
Kuwa na hali ya kuongea kile unachotaka kitokee na sio kile
unachokitenda ,kwa kuwa waweza kuwa unapenda sana uache hiyo tabia mbaya lakini
unashindwa kujisemea kuwa nitaiacha kwa kuwa bado kila iitwapo leo
unaitenda.
Imeandikwa “Uuzuie
ulimi wako na mabaya, Na midomo yako na kusema hila .”- Zaburi 34:13
Kwa kinywa chako kinaumba kitu katika ulimwengu wa kiroho
ambao huja kutokea katika ulimwengu wa kimwili.Kwa hiyo ukiwa mara kwa mara
bila kuchoka unajisemea “nitaiacha tuu tabia mbaya niliyo nayo”,au
“ kuna siku nitakuja kuacha milele hii tabia mbaya kwa msaada wa MUNGU”,Kweli
utashangaa siku utaacha kabisa na itakuwa shuhuda kubwa sana .imeandikwa“. .
. . . . . . . . . . . . . .. . . . . . . . ; Ulimi wangu ni kalamu ya mwandishi
mstadi.”- Zaburi 45:1
“Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri; Bali vinywa vya
wapumbavu humwaga upumbavu. “- Mithali 15:2
5.Usikate tamaa kumrudia MUNGU pale unapoanguka mara kwa
mara.
Usije kata tamaa kumuomba msamaha MUNGU mara kwa mara pale
unapoanguka katika hiyo tabia mbaya.
MUNGU anapenda watu wote ila
anachukia dhambi,kwa hiyo usione aibu kumwendea MUNGU kuomba msamaha
kila unapoirudia ile tabia mbaya ambayo huipendi .
Kwa kuto kukata tamaa kwako juu ya kumuomba msamaha MUNGU kila unapoitenda
hiyo tabia yako mbaya,
Yeye MUNGU hutuma uwezo wake kwa neema yake ukusaidie
kuacha hiyo tabia kwa kuwa anajua kuwa ukiacha hiyo tabia mbaya utaweza
kumtumikia vyema na kwa ujasiri zaidi.
MUNGU hajali kuwa umeirudia ile
tabia yako mbaya mara ngapi ,bali anajali umenyanyuka nakumrudia MUNGU kila
ulipo itenda hiyo dhambi inayotokana na tabia yako.
Imeandikwa “ Kwa
maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena; . . . . . . . . . . .” Mithali
24:16.
Kitu cha muhimu ni kwamba kila
unapoanguka nakuirudia tabia yako mbaya hapo hapo rudi kwake MUNGU na kutubu
kwa ajili ya hicho ulichotenda naye atakusamehe na kukupa nguvu ya kuacha hiyo
tabia mbaya.