Emmanuel
Agyarko ni kijana kutoka Kumasi nchini Ghana.Alianza kuona maono ya kiMungu
toka alivyokuwa mtoto.Akieleza ‘Hata
hivyo ilivyofika mwaka 2009 ilizidi sana, na Bwana alinionyesha maono mengi
,lakini ilipofika tarehe 24 mwezi wa 11 mwaka 2011,mchana nilipokuwa natoka
shule.
Nilijiona nimechukuliwa na Bwana mchana,mchana nilipokuwa narudi kutoka
shule na Bwana akanipeleka kuzimu kunionyesha mambo mbali mbali ambayo kwa hayo
wanadamu walioko duniani wataonywa ili wasiiendee njia ya kuzimuni.
WACHUNGAJI WASIOTOA FUNGU LA KUMI.
Bwana
alinionyesha wachungaji wanne(4) kuzimu, ambao walikuwa hawatoi fungu la kumi
hapa duniani.Mmoja aliitwa Albert na mwingine alikuwa Daniel, Mchungaji wa Kanisa
la YESU na katika kanisa lake walikuwa hawaamini katika kutoa fungu la
kumi.Daniel aliniambia kuwa alikuwa akiwaambia waumini wake wasitoe zaka na sio
muhimu tena.Danieli alikuwa kuzimu kwa makosa mawili(2) ,kwanza kwa kutokutoa
fungu la kumi na kosa la pili ni kuzuia wengine kutoa fungu la kumi.
Albert, kanisa lake lilikuwa likiamini katika kutoa fungu la kumi
,lakini yeye alijua ni kwa ajili ya waumini pekee ndio wanaotakiwa kutoa fungu
la kumi na sio wachungaji.Alikuwa akitamani japo arudi duniani ili aanze upya
na atoe zaka kama inavyotakiwa.
Wachungaji
wengine wawili(2) hawakuwa wakitoa zaka,mmoja wao alijua na alidhani hatakiwi
kutoa zaka hata kama alijua,mwingine aliona kuhudumu kama vile hakuelekei
vizuri hivyo hahitaji kutoa fungu la kumi.
WATU WANAOTUMIA HIRIZI ILI KUPATA WAUME.
Niliona
wanawake wengi waliotumia hirizi ili kupata waume ili waolewe.Wengine walitumia
lipstiki za kiganga,make-up za kiganga ili kuweza kutongoza wanaume.Nilimuona
mwanamke mmoja aliyeandikwa jina lake Ama Gyamfua aliyekuwa akihudhuria kanisa
la Pentekoste, naye alipewa hirizi kutoka kwa mnganga wa kienyeji iliamuendeshe
mume wake kama mbwa; Hiyo ndiyo sababu alikuwa kuzimu akiungua moto kutokana na
kutumia hirizi.Mwanamke mwingine niliye muona aliitwa Mavis ambaye yeye alikuwa
akipaka midomo yake kwa lipstiki, na alipewa lipstiki hiyo na mganga wa
kienyeji na kila alipokuwa akiitumia ilikuwa inafanya wanaume wamtamani kulala
naye alikuwa akijipatia fedha kutoka kwa wanaume hao.
Niliona
mwanamke mdogo anayeitwa Vivian ambaye alionekana kama vile alikuwa ana miaka
24,akiwa ana nguo za aibu sana ziko fupi sana, alikuwa na kucha ndefu
zilizoandikwa,amejidobeka lipstiki na skafu kichwani mwake.Yupo kuzimu kwa
sababu alikwenda kutafuta hirizi kutoka kwenye miungu, Hivyo alipo lala
mwanaume yeyote alikuwa akichokua mbegu za wanaume(semen/manii/shahawa) na
kuzipeleka kwenda kufanyia dawa.Kutokana na vitendo vyake hivyo wanaume
watano(5) walishafariki, Na alikuwa akifanya hivyo ili aweze kupata fedha,
Aliniambia alikuwa akivaa kiaibu sana alipokuwa duniani ili awatongoze wanaume
na alikuwa akiishi Kwashieman,Accra,Ghana.
Niliona
mwanamke ambaye alikuwa ni mke wamchungaji duniani naye ni Alice.Alikwenda kwa
kutafuta hirizi kwa ajili ya mumewe,Aliniambia alikuwa ni mchawi na alikwenda
kutafuta dawa/hirizi.Aliweka damu za siku zake(hedhi kwenye maji ya dafu
akachanganya na vitu vingine ili mume wake anywe.Na muda huo huo mumewe
alipokula vitu hivyo akawa kama mtoto wake yani anaweza kumdhibiti n kumendesha
vyovyote atakavyo.Kiroho alimfungia mumewe kwenye chupa.
Pia
aliweza kuua baadhi ya washirika na alipokufa alitupwa mara moja kuzimu kwa
vile vyote alivyovitenda duniani.
WANAOTUMIA HIRIZI ILI
KUFANYA MAPENZI NA WANAWAKE WENGI
Bwana alinionyesha mwanaume aitwaye Kwame, ambaye alikuwa ni
mwanachama wamambo ya kishetani.Alikuwa ana pete katika uume wake ambayo
ilifanya iwezekane kuwaingiza makahaba kwenye chama hicho cha kishetani.kwa
hiyo baada ya kulala na makahaba, huwaua kishirikina na kutumia sehemu za miili
yao kama sadaka za kiuchawi kwa ajili ya watu wengine.
Nikaonyeshwa mwanaume mrefu, aliyekuwa na hirizi inayomuwezesha
kutongoza wasichana kwa ajili ya kufanya nao ngono.Aliweza kufanya ngono na
wasichana 1000 na alikuwa katika chuo kikuu cha Ghana,Legion,Accra.Alikwenda kuongeza
ukubwa uume wake kwa kutumia uganga wa kienyeji na akapewa vitu avipande.Hayo
mambo yamemsababisha awe kuzimu na aliwahi kuwa kiongozi wa vijana kanisani, na
akafanya mapenzi na wasichana wengi kanisani hapo.
Baadaye nikaonyeshwa mchungaji/mwinjilisti aliyeitwa Francis
ambaye alikuwa kanisa la Methodist.Alikwenda kwa waganga kujipatia hirizi
itayomuwezesha kutokupingwa/kutokukataliwa jambo lolote atalolisema.Alikuwa
akitongoza wasichana na hakuweza kumkatalia na
alikuwa pia shoga.
WANAOTUMIA HIRIZI KUPATA ILI WAPATE UMAARUFU NA
FEDHA.
Nikamuona
mwanadada ambaye alikuwa ni mtangazaji wa habari kutoka hapa Ghana kabla hajafa
alikuwa akitumia make up alizopewa na mganga wa kienyeji kutoka India(Indian
occultist).Na lengo lake ilikuwa ni kupata umaarufu,kibali na kupendwa na
watu.Na alikuja kufa kwa ugonjwa wa kisukari na kujikuta yupo kuzimu kutokana
na yale aliyoyatenda duniani.
WATUMISHI WANAOTUMIA NGUVU
ZA GIZA.
Nikaonyeshwa wachungaji saba(7), ambao walikufa hapa Ghana, na
wote walikuwa katika vyama vya siri vya Kishetani na walikuwa wakivaa kama
hivyo,Waalikuwa wote manabii na walikuwa na pete za ajabu, ambazo walikuwa
wakizitumia kufanya miujiza na kutabiri katika makanisa yao.
Wote walikuwa
wakilia kwa uchungu wako kuzimuni.Nikaonyeshwa muimbaji wa injili ambaye alishafariki Ghana, Naye
alikuwa akisema ni mchungaji naye kumbe alienda kwa mpiga ramli wa
kihindi(indian man) kwa ajili ya kupata msaada kwa ajili ya uimbaji
wake.Alisema huyu mganga alimpa mafuta na uvumba wa kichawi ambao alitakiwa awe
anauchoma pia alikuwa na pete ya kichawi yenye kumpa mamlaka ya kutoa
kanda(album)nyingi za muziki.
Naye alikuwa akitakiwa kulala na wanawake, hivyo
katika makanisa amelala na wanawake wengi sana.Kuzimu kulikuwa na funza wakali
waliokuwa wakitoboa mwili wake kutoka kichwani hadi miguuni yaani kila sehemu ya mwili wake na wakati huo
huo moto mkali ulikuwa ukimuwakia na kumuunguza sana.Naye aliandikwa kwenye
paji la uso wake namba 666.Nikamuona mtu aitwaye Abednego ambaye alifungwa
nyororo shingoni mwote.Alipokuwa duniani alikuwa akitumia hirizi ambayo
inamuwezesha kupotea sehemu yeyote yenye hatari/vifo.
Alikufa na sasa yupo
kwenye moto wa kuzimu akiteseka.Niliona baadhi ya wa ghana wakivaa
pete,dhahabu,siliva,chuma za tofauti tofauti na wote walikuwa wana chama wa
vyama vya kishetani(wajenzi huru).
Nilionyeshwa waziri aliopita wa uchumi wa Ghana, ambaye alikuwa
kuzimu kwa sababu ya kuwa mwanachama wa vyama vya siri vya kishetani(secret
society), naye alipewa nguvu za giza zenye kumpa akili nzuri.
Nikamuona mchungaji kutoka ghana aliyeitwa Alfred ambaye
alimtafuta malikia wa kishetani wa pwani(queen of the coast) kwa ajili ya
kupata nguvu.Naye alikuwa na pete na kitambaa cheupe.Kitambaa kilikuwa ni kwa
ajili ya uponyaji, na pete ilikuwa kwa ajili ya kutoa mapepo.Moto wa mateso
yake ulikuwa mara saba zaidi ya wengine wote pale waliokuwa wakitumia hirizi.
Nikaonyeshwa mwanamke kutoka Naijeria aliyekuwa akitumia
limbwata(charm) ili mume wake atapokufa yeye azirithi mali bahati mbaya huyu
mwanamke alikufa na kujikuta ndani ya moto mkali wa kuzimu.
Bwana alinionyesha wanafunzi mbali mbali wakiwa na mabegi
migongoni mwao.Kuanzia shule ya msingi, sekondari hadi chuo.Nao wanafunzi hao
walienda kutafuta dawa(hirizi) kutoka kwa waganga wa kienyeji ili wafanye
vizuri masomoni.Bahati mbaya hawakuweza kumaliza elimu zao na wakapatwa na
mauti wote wakafa na kujikuta kuzimu.
Niliwaona pia baadhi ya wanafunzi kutoka
katika shule marufu sana hapa Kumasi,Ghana.
Niliwaona madaktari(medical doctor) wengi wakiwa kuzimu, na mmoja
wao anaitwa Dr.Frimpong ambaye aliponiona mimi alieleza kuwa yupo kuzimu kwa sababu alipokuwa duniani alikuwa
amejiunga na vyama vya siri vya kishetani na huko walipewa pete ili iweze
kumlinda yeye.Naye alikufa kwa ajali na akajikuta yupo kuzimu iwakayo moto.
Niliwaona wanasheria wengi,mahakimu na majaji wote wakiungua
motoni.Nao wote walikuwa sehemu ya vyama vya kishetani(secret societies) na
wote walitafuta mashetani ili wapate ulinzi.Walikuwa na pete za kishetani
zilizokuwa zinawalinda walipokuwa hai.
Nilionyeshwa binti ambaye mimi binafsi nilikuwa namfahamu kwani
alikuwa akiishi Kwadaso, hapa Ghana.Naye alienda kwa waganga wa kienyeji ili
aweze kupata wanaume wazuri.Naye alikufa kifo cha aibu baada ya hapo yupo
kuzimu sasa anaungua moto kutokana na makosa yake aliyoyafanya.
Nikamuona mtu ambaye alikuwa anaitwa Budo ambaye alikuwaga
Buokrom,Ghana.Alipokuwa duniani huyu mtu alikuwa ana nguvu sana mpaka polisi
walikuwa wanamuogopa,alikuwa ana ulinzi wa kishetani na hizo nguvu zimefanya
mwili wake kuwa kama chuma.Hivyo hata akipigwa risasi ilikuwa haingii mwilini
mwake ila tuu inaweka alama, Alimuuzia shetani roho yake ili aweze kupata nguvu
hizo.Huyu mtu pia yupo kuzimu motoni akiteseka na mapepo wanatumia mikuki ya
moto(myekundu) kutoboa mwili wake na kuuchana chana.
Niliona makahaba ambao walikuwa wakikimbizwa na mapepo ndani ya
moto na hao mapepo walikuwa wanawabaka hao mabinti ndani ya moto.Hao mabinti
walienda kutafuta hirizi ili waweze kufanya biashara za kujiuza bila ya
kudhurika au kuuwawa.Mmoja wao anaitwa Joana naye alisema “nilikuwa na nguvu ya
kuyeyuka sehemu kama hiyo sehemu ina hatari”.Wanawake wote hawa walikuwa kuzimu
kwenye moto wakiteseka kweli kweli.
Nilimuona mwanamke toka Ghana ambaye alikuwa anaitwa “Anti
Afua”.Naye alikwenda kupata maji mtakatifu kwenye galoni kubwa kutoka kwa nabii
ambaye alikuwa Ghana.Mwanamke huyo aliyafanya maji hayo kama mungu.Hayo maji
yalikuwa ni ya kipepo na huyo dada alipokufa aliishia kuzimu.Nilimuona Frank
ambaye alitokea Ghana.Naye alienda kupata kitambaa cha mkononi(handkerchief)
kutoka kwa nabii, ili kwamba muda wote akijifutia usoni apate kibali.Alijipatia
kibali kila alipokwenda ,na hiki kitambaa kilikuwa ni cha kipepo, alikufa akiwa
na dambi hii na kuwa kuzimu akiungua moto.
Nikaona kwa mbali korongo na kulikuwa kama vile watu elfu
kumi(10,000) wakiungua kwenye mlipuko wa moto mkali mfano wa uji uji.Mapepo
yalikuwa yakiwacheka na kuwa kejeli wakisema “wote ninyi mmetumia pete zetu za
maajabu”.Niliposogea karibu nikajua jina la mtu mmoja katika kundi hilo naye
alikuwa akiitwa mchungaji Afriyie kutoka Ghana.Alisema alienda kupata pete ya
uponyaji”.Kulikuwa na karibu wachungaji elfu mbili katika hilo eneo kwa wale
waliokuwa wanatumia pete za maajabu kutoka kwa shetani.
Nao walikuwa ni kutoka
nchi mbali mbali duniani kote.Nikamuona
kijana mmoja niliyekuwa namjua awali hapa Ghana na alifariki.Huyu kijana
alikuwa mzuri wa sura na alipokuwa mzima alikuwa na marafiki wakike aliokuwa
anatembea nao naye yupo kuzimu kwa sababu ya uzinzi.Niliona mkanda wa moto
kiunoni mwake ambao mkanda huo ulikuwa unamuunguza yeye na kumkatakata.
Naye
alijuta kwa nini alilkuwa duniani.
Niliona mapepo watano wakiwa na mabegi makubwa yaliyojaa kila aina
ya fedha kutoka nchi mbali mbali na zilikuwa zimetolewa kwa wale walioingia
mikataba na shetani ili wapate utajiri kwa masharti ya kuuza roho zao kwa
shetani na watakufa baada ya muda.Kwa wale waliojiunga katika huu mfumo na mara
tu utapojiunga unakuwa umeifungia roho yako kwenda kuzimu na mara utapokufa
utajikuta kuzimu ndani ya moto.
Nalimuona mjumbe wa shetani akimwambia mtu kuwa ataishi miaka
saba(7), lakini kiukweli hiyo yaweza
kugawanya kwa mbili na mtu afe baada tuu ya miaka mitatu na nusu na kujiunga
kuzimu motoni.
Nilimuona mwanamke wa kinaijeria mwenye umri kama miaka 43 alikuwa
motoni kwa sababu ya kutoa kafara damu zisizo na hatia.Alikuwa akiiba watoto
hata wa umri wa mwezi kutoka mahospitalini ili kuwatumia katika makafara ya
kishetani.Alikuwa akiweka watoto kwenye vinu na kuwatwanga mpaka kuwaua.
Ndipo
huongeza mchanganiko wa manjano na kijani wa mafuta ya kichawi na
anapochanganya tuu na hizo maiti za watoto wachanga ,Ghafla hugeuka mara na kuwa fedha za kimarekani(US dollars)
katika roho.Naye hufurahia na kusema hela hela!!!.
Kuzimu huyu mwanamke alikuwa akiteswa na mapepo watatu na
wakimwambia “wewe,mwanamke mbaya,msifu shetani kwa kuwa hicho ndicho
ulichokitenda duniani”.
Nikaona mwanamke ambaye duniani alilala na wanaume wengi na kila
akilala na mwanaume hukusanya kondom walizotumia na kuchukua shahawa na
kuziweka kwenye chombo na kupeleka kwa waganga ili kutoa kafara kwa ajili ya
kupata fedha.
Huyu mwanamke alivyokufa alipelekwa kuzimu akiteswa ndani kwenye
moto.
Kila
roho iliyotenda hayo iko kwenye shimo kuzimu.Watu wa namna hiyo walikuwa kutoka
nchi nyingi sana lakini mimi nilifanikiwa kuwaona kwa ukaribu hawa wawili ambao walitokea Ghana.Mtu mmoja
kutoka Naijeria alisema “MUNGU niokoe mimi”. Na sauti ikasema “ Si kukujua
wewe”.Lusifa/Shetani akaja kwenye ile sehemu ya kuzimu na kucheka kwa kejeli na
bila ya kujizuia.
MTOTO WA
MALIKIA DIANA NA MICHAEL JACKSON
Nikaonyeshwa mtoto wa kike wa malikia Diana naalikuwa kuzimu kwa
sababu ya uchawi,alipokuwa kuzimu alionekana kidogo kama ameharibika.Alikuwa na
pete ya kishetani ya kujilinda aliyoipata India lakini cha ajabu pete hiyo ilishindwa
kumuokoa usiku ule alipofariki.
Moja ya mtu niliyemuona kutoka kwenye makundi ya muziki alikuwa ni
Maiko jackson.Alikuwa na pete la kishetani kutoka India kwenye mkononi mwake
inayoweza kuita nguvu kubwa za shetani.Naye alisema “Nilikwenda kwa shetani
kupata pete, inayonipa umaarufu na utajiri na sauti yangu kuwa kama ya malaika,
Sasa nipo kuzimu nateseka milele bila KRISTO”.Na ni hii pete kutoka India
iliyonipa umaarufu mkubwa na nilipata nguvu ya kuimba vyema.Alikuwa mmoja wa
watu waliokuwa wanatumia hirizi hapa duniani.
MUAMMAR GADDAFI NA MKUU SANI ABACHA WAKIWA KUZIMU
Nilionyeshwa aliyekuwa raisi wa zamani wa Naijeria aliyeitwa Sani
Abacha katika sehemu huko kuzimu,ambako wengi wa viongozi wa dunia yote huenda
huko.
Naye aliyesema “Nilisababisha vifo vya maelfu kwa maelfu kwa ajili ya
kutoa kafara”.Na pia nilimuona Muammar Gaddafi aliyeuwawa na waasi nchini
Libya.Muammar Gaddafi alisema “niko hapa kuzimu kwa sababu sikuamini katika
YESU”.
Nilionyeshwa jinsi alivyoishi duniani, Alikuwa na mkufu wa maajabu
uliokuwa unamsaidia kupotea popote hata kuwa kama upepo. Siku ambayo nguvu ya
NATO na waasi walipomvamia hiyosiku alikuwa amesahau mkufu wake wa maajabu
alioutoa kwa wakuu wa vyama vya kishetani kutoka India(occult grand master in
India).Aliniambia niwaambie wa Libya,watoto wake na mkewe kugeukia
Ukristo.Alisema yeye anateseka sana na wao kama hawatabadilika wote wataishia
sehemu hii ya moto.Alizidi kusema kuwa hata wote walioniua mimi wasije mahali
hapa.Akaniomba tone la maji.
WATU
AMBAO WAKO NJIANI KUELEKEA KUZIMU.
Bwana alinionyesha watu ambao wanafanya manunuzi vitu mbali mbali
na kuelekea kuzimu.Duka lilikuwepo Ghana,lakini maduka kama hayo yapo nchi
mbalimbali duniani kote.Maduka hayo yanauza vitu mbalimbali vya kishetani
vinavyotumiwa na waganga wa kienyeji na manabii wa uongo katika makinisa
yao.Hivi vitu ni jumla ya nyekundu,nyeusi,majenta,dhambarau na mishushumaa ya
kijani,mafuta mbali mbali ya kishetani,poda,maji, makofuli na vitu vingine
vinavyotumiwa makanisani.Wanaonunua vitu hivyo vya kishetani wanatembea moja
kwa moja kuelekea kuzimu.
Bwana YESU alinieleza kuwa muda wowote mtu anapopata hirizikwa
ajili ya kufanyia chochote, huyo anakuwa amejiingiza kuzimu.Nikaona pepo kuzimu
amebeba chombo kimejaa pete nyingi.Pepo akasema pete zote hizi wanapewa watu
wanaojitafutia hirizi kwa ajili ya ulinzi,uponyaji,uroho,nguvu za giza, marifa
na mengineyo.
Nilionyeshwa chupa nyingi na zingine walikuwa wanazichukua na
kuleta duniani ili zitumiwe na watu wenye kutoa kwa wengine na hufunga roho zao
kwenye chupa katika ulimwengu wa kiroho.Mtu yeyote anaye mloga mwenziye anakuwa
mmoja na shetani naye ataishia kuzimu kwenye adhabu.Niliweza kuonyeshwa baadhi
ya watu maarufu,watu wa mahakamani na hata wanasiasa wakiwa kwenye njia ya
kuelekea kuzimu kwa sababu ya kutumia kwao kwa hirizi mbali mbali ili waweze
kufanya vyema, kupata nafasi kubwa na kuwa maarufu.
Nilimuona
muigizaji maarufu wa kike nchini Ghana ambaye aliweka hirizi katikati ya matiti
yake ili aweze kuwavuta watu.Yeye na wengine wengi wanaotumia hirizi za namna
hiyo wako njiani kuelekea kuzimu.Niliwaona waimbaji wengi wa injili na wamiziki
ya kidunia waliokuwa wakielekea kuzimu kwa sababu ya kutumia hirizi ili kuimba
na kutengeneza kanda(albums) zao.Nilimuona mtunisha misuli naye alikuwa akitumia
kisehemu ya vitu vya kishetani fulani fulani katika mwili wake ili awe mwenye
nguvu na ashinde medali nyingi zaidi.Wote hawa walikuwa njiani kuelekea kuzimu.
WACHEZA
MPIRA
Nikaona mvulana wa miaka 12 ambaye alikuwa ni mcheza
mpira.Nikauliza Bwana YESU kwa nini huyu yuko hapa kuzimu ,Naye Bwana akanijibu
ni kwa ajili ya kushiriki katika nguvu za kishirikina.Mwalimu wake wa mpira
alimuongoza kufanya matendo hayo ya kishirikina ili awe mcheza mpira
mkubwa.Huyo kijana alipewa mafuta ya kishirikina ili ayapake mwilini kabla ya
mchezo.
Nilimuona mchezaji kutoka Brazil naye alikwenda kwa wachawi ili
asaidiwe kucheza ligi vizuri.Naye hakwenda kushukuru kwa hao wachawi baada ya
ligi ndipo alipokufa siku akiwa na mechi nyingine.
Nilionyeshwa
Marc-Vivien Foé, mcheza mpira mkamerooni ambaye alikufa katika mechi huko
ufaransa mwaka 2003.Yeye alienda kwa Malikia wa kishetani wa nyika(Queen of the
coast) kwa ajili ya kucheza vizuri kombe la Afrika(African Cup of Nations).Na
baada ya kucheza kombe hilo alitakiwa kumtoa mama yake kama kafara naye
alikataa.Ndipo hiyo siku roho za giza kutoka ufalme wa majini zikaja
kumpiga moyo wake pale pale na kumuua
pale pale.Naye akajikuta kuzimu kwa kosa la kushiriki mambo ya
ushirikina.Kuzimu nilimuona akibeba fuvu la mtu ndani ya moto.
WACHEZAJI NA
WASHABIKI NJIANI KUELEKEA KUZIMU.
Nikaonyeshwa timu nyingi na mashabiki zake wakielekea kuzimu
kupitia kwenye handaki.Timu ya kwanza niliyoiona ni Chelsea,nao walikuwa
wakiongozwa na Ivanovic, na wakifuatiwa na wachezaji wengine katika mstari
ulionyooka.Wote walikuwa na uvumba wa kishetani,mafuta ,pete za ajabu na vitu
vingine vya kishetani.Nilionyeshwa jinsi gani wale wanaoshabikia hizi timu
kutoka miyoni mwao wanavyoelekea kwenye tanuru la moto kuzimu.
Nilionyeshwa Ronaldino na watoto ambao umri wao ni kati ya 8 ha
13.Hawa watoto walikuwa wakijifuna kucheza kama yeye.Nikaona pepo la ajabu
likatokea kwa umbao la ajabu ajabu mara linakuwa kama mwanamke, mara kama
ngedere, na alikuwa ana mabawa kama popo.Huyo pepo alikuwa anamsaidia kucheza vyema.Kwa
hiyo hao watoto walipokuwa wakijifunza kucheza kama Ronaldino, ndipo pepo hilo
likajidhihirisha na kuwaingia wale watoto.Niliona yeye na wote mashabiki
wake,wasaidizi na hao watoto wanaojaribu kumuiga kucheza kama yeye wanatembea
kenye tanuru kuelekea kuzimu.
Mcheza mpira mwingine maarufu niliye muona naye alikuwa
Kaka.Alikuwa na Bibilia mkono wa kulia na mpira kwenye mkono wa kushoto.Nikaona
pepo limemfuata na kumwambia “nifuate na ntakuonyesha njia ya udanganyifu na
uongo”.Huyo pepo alimbadilishia bibilia na kuiweka mkono wake wa kushoto na
kumpa mpira mkono wa kulia kwake.
Kwa huzuni huyu pepoalikuwa akimuongoza kuzimu
pia.Nikamuona mtu akimwambia ki Potugo(Portuguese) kuwa unaweza kuwa Mkristo
lakini kila kitu unachokitaka kukifanya kwenye mpira nitafanya kwa ajili
yako.Huyu mtu alikuwa akifanya kafara na mapepo yalikuwa yakitokea ,ndipo
huweka mafuta kidogo kichwani na pepo kumuingia yeye.Ndipo anaanza kucheza
vizuri.Nikaona wachezaji vijana wa kibrazili wote wanamfuata kelekea kuzimu.
Nikaonyeshwa baadhi ya watu waliokuwa wakitembea kimya kimya
kuelekea kuzimu, na walikuwa ni timu ya Brazili.Nikamuuliza Bwana YESU, Nini
walichokifanya naye YESU akanijibu ni kwa sababu ya kuabudu sanamu.Hii ni kwa
sababu Mpira ni mungu na wale wanao wasaidia wanaishia kuzimu.
Nikamuona Pele
amekwenda kwenye sehemu wanapozikia watu wengi(makaburini) usiku naye huita
mapepo, Nayo mapepo huja kwa wachezaji na mafuta ya ajabu na kuwapaka na
walitakiwa wasiguse mwanamke.Nikaona pepo la ajabu na alikuwa na kichwa kama cha mtu lakini
kiwili wili kama cha kondoo.Huyu pepo alikuwa akiongoza timu ukijumuisha na
wachezaji wa zamani kama vile Pele na wengine.Nikaona wengi wa brazili
wakimfuata kimya kimya kuelekea kuelekea kuzimu kwa sababu ya mapenzi makubwa
na mpira.
Nikaona wachezaji wengi wanaotumia pete,mafuta maalumu ya
kishetani,na vitu vingine vingi vya kishetani vilivyozoeleka kiasi kwamba
kuonekana kuwa kama vile ni vifaa madhuti
kwa ajili ya kuchezea.Kitu cha kuhuzunisha ni hiki wachezaji wote na
mashabiki wao wote wanaelekea moja kwa moja kuzimu.
Nikaona timu ya Ufaransa ikiongozwa na Zidane na wachezaji wengine
wa zamani.Mashabiki wao na wapenzi wao wote walikuwa wanaelekea kuzimu baada ya
hiyo nikaona timu ya taifa ya Misri ikiongozwa na Abutreka na wote walikuwa
njiani kuelekea kuzimu.Timu ilikuwa inaongozwa na mapepo mawili yenye umbo kama
ng`ombe.
Pepo mkubwa aliowasaidia kushinda kombe la Afrika (African cup of
nations) mara saba alikuwa Osiris.
Nilionyeshwa timu zote
duniani ikiwemo na timu ya taifa ya Ghana,Maarufu kama Black stars ikifuatiwa
na washabiki wake.Ndipo nikamuuliza Bwana YESU kwa nini iko hivyo, na Bwana
YESU akaniambia ni kwasababu wote wanamilikiwa na adui na wamehusika katika
matendo ya kishirikina.Bwana akaniambia Anawaonya hakuna ashirikiye matendo ya
kishirikina atakaye ingia kwenye ufalme wangu.
Nikaonyeshwa klabu zote za mpira zipo katika viwango tofauti
tofauti njiani kuelekea kuzimu kimya kimya ,wakifuatiwa na mashabiki wao kwa
ukaribu sana.Vijana wote wadogo waliokuwa wakiwafuta wacheza mpira hawa wakubwa
wote walikuwa wakiwafuata kwenda kuzimu.Baadhi ya hao vijana hawakwenda kwa hao
waganga wa kienyeji wenyewe bali walimu
wao wa mpira na makocha wao ndio huwapa masharti yote ya kiganganga ya kufanya na
ndio wanaowapeleka kwa ajili ya nguvu za giza ili kupata ushindi.
WAKRISTO
NA MPIRA WA MIGUU
Nilionyeshwa timu mbili za kiKristo zikicheza mechi,na mapepo
yakaja pale kwa muundo wa wanyama mkubwa na wakakaa na kuangalia mechi.Walikuwa
na furaha na wakipunga.mapepo wengine pia walijitokeza kutokea chini ya kiwanja
cha mpira na wakaanza kupindua matokeo kishetani kama vile wao ni makocha na
hata wakristo walivyokuwa wakicheza hiyo mechi, mapepo walikuwa wanahaki ya
kuwa pale kwa sababu mpira wa miguu ni mchezo ulioundwa na shetani ili
kudanganya wengi waende kuzimu.
Nikaonyeshwa mechi mbali mbali za mpira za makanisani na nikaona
mtu mmoja akaenda kumuona mganga wa kienyeji ili washinde mechi.Alipewa saa na
muda wa kwenda makaburini na kulala kutokea
saa 6 usiku mpaka saa 12 asubuhi. Akaweka saa karibu na pembezoni mwa kanisa lililo
kinyume nao ili waweze kushinda hiyo mechi.
Na timu ingine pia ikaenda kwa mganga wa kienyeji aliye wapa
kimiminika cha ajabu alicho kinyunyiza kwenye jezi zao.Ndipo mapepo yalipokuwa
yakiwatawala wachezaji hao.
WATU
WENYE TATUU(TATTOOS)
Nikaona mvulana wa miaka 17 wa kimarekani aitwae Phillip.Huyu
mvulana alikuwa na tatuu ya buibui(spider) kwenye mgongo wake.naye alisema
rafiki yake alimwambia yeye kuwa yaweza
kumlinda kutopata magonjwa.Nikamuona shetani akimpita na kumkejeli.Huyu kijana
alikuwa kanisani na alidhani ataenda mbinguni.Bahati mbaya huyu kijana yupo
kuzimu sasa kwa sababu ya tatuu(tattoo).Shetani alisema “Wote wanaotumia
tatuu(tattoos) wananitumikia mimi”.Nimeona wengi kwenye hiyo sehemu wapo kuzimu
kwa sababu ya tattoo katika miili yao.
Nilimuona shetani akijigeuza yeye binafsi na kuwa mtu mdogo mwenye
tatuu nyingi sana mwilini mwake,Alikuwa akiwatoboa ,akiwachana chana ndani ya
moto na huku akiwakejeli kwa kunukuu Mambo ya walawi 19:28 “Msichanje chale yo yote
katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini
mwenu; mimi ndimi Bwana”.
Kuzimu kuna vyuma vyekundu vinavyoshikizwa kila sehemu ambapo mchoro wa tatuu umepita,
na kunakuwa na maumivu makali sana.Nikamuona kijana mmoja aliyesema hakujua
shida itayompata, yeye aliiga tuu kuchora tatuu kutoka kwa rafiki yake naye
akafanya hivyo hivyo.Hata hivyo huyo kijana yupo kuzimu na maumivu mengi kwa ajili ya kuchora tatuu.
WANAUME WANAOVAA HERENI
Nikasogea
sehemu ile kidogo na nikaona kijana mdogo kwenye moto akiungua akiwa amevaa
hereni masikioni.Alisema alikwenda kutafuta nguvu ya giza kwa ajili ya
kutongoza wasichana.Alikuwa na pete aliyokuwa akiitumia kutongoza wanaume na
wanawake ili afanye nao mapenzi.Wavulana na wanaume wengi wanatumia hivyo vitu kutongoza wasichana ili
kufanya nao mapenzi.Hiyo ni njia ingine ya kufanya ushirikina kwa sababu nguvu
za giza huingia kwa wavulana na wanaume wanaofanya hivi maisha yao huongozwa
kuhamasika tofauti na ilivyo kawaida.
VITABU
VYA KISHETANI NA KIKRISTO.
Nilionyeshwa
maktaba kuzimu na ilikuwa nyeusi na kulikuwa na mishushumaa myekundu,bluu na
myeusi lakini ilikuwa ikiyeyuka ilivyokuwa ikiungua.Nikaona kitabu cha
Momoni(Mormon), Vitabu vya utabiri wa nyota (astrology), Uchawi mweupe, bibilia
ya kishetani, vitabu vya uumbwaji(books of evolution), Kitabu cha sita na cha
saba cha Musa, bibilia ya Hip-hop, Kitabu cha mabadiliko na vitabu vingine
,baadhi vvilikuwa vikitumiwa na dini mbali mbali.Wote wanaotumia vitabu hivi
huishia kuzimu.Nikaona pia vitabu vingi vya kikristo na shetani akisema roho
yangu na nguvu yangu inaishi kwenye hivyo vitabu na kwa kitabu chochote ambacho
hakina ROHO wa MUNGU.Shetani alisema pia kitabu chochote kinachopeleka watu
kuzimu huwekwa kwenye hiyo maktaba ya kuzimu.Watu wanabidi wawe makini sana na
vitabu wanavyosoma hata kama vikiwa na kichwa cha habari kinachoonyesha ni
kitabu cha kikristo.
MAASKARI
Baada ya hayo nikatoka kwenye hicho chumba,nilipelekwa kwenye
sehemu kuzimu ambako kuna maaskari.Hawa ni maaskari kutoka nchi mbalimbali
duniani kote.Walikuwa katika dimbwi la moto.Hao walikwenda kwa waganga kutafuta
nguvu za giza ili kujilinda na kupigwa risasi,na silaha zingine.Baadhi yao
walikwenda kwa waganga wa kienyeji ili kupata nguvu za giza za kuyeyuka,wengine
walikuwa na mavazi ambayo yametoka kwa shetani ili kuzuia risasi zisiwapate.
Walifanya kila aina ya maendo ya ushirikina walipokuwa
duniani.kila mmoja wao alikuwa na namba 666 kwenye mapaji ya nyuso zao.
Kulikuwa na mapepo wakubwa aliokuwa akiwa garagaza na kuwapa
mateso.Mapepo yaliokuwa yanahusika kutoa
mateso yalikuwa yana urfu wa futi 19naye alikuwa akionekana kama chura na macho
matatu.nilimuona askari wa Ghana aliyekuwa na habari ya kusikitisha yeye
alikuwa kwenye michezo ya ngumi(martial arts) na alipokufa mapepo yakamvuta
mpaka kwenye hiyo sehemu kuzimu.Watu wengi hawajui kuwa michezo hiyo ina
husisha na imani za kishetani,wale wanaocheza michezo hiyo ya martial arts
hushia kuzimu.
WAVUTAJI
Na
baadaye nikaomnyeshwa watu wawili(2) ambao wako kuzimu kwa sababu walikuwa ni
wavutaji.Hivyo watu wanabidi waache kuvuta kwa kuwa kuvta kwa weza kukupeleka
kuzimu.
WATU WANAO OMBA KWA WATAKATIFU
Nikaona mtu ambaye anaomba kwa majina ya watakatifu alipokuwa
duniani.na vitendo hivi viwekwa kama ushirikina na mtu huyo alikuwa akipata
mateso makubwa sana motoni .Baada ya hapo nilichukuliwa na kutolewa kuzimu kuja
duniani.
SALA
YA TOBA
Mpendwa Baba MUNGU uliye mbinguni, ninakuja kwako katika jina la
YESUKRISTO.Nina kiri na kutambua kuwa ni mwenye dhambi zote, nisamehe dhambi
zangu na maisha niliyoishi;Nahitaji msamaha wako.Naamini wewe YESUKRISTO
ulimwaga damu yako pale msalabani kalivari na kufa kwa ajili ya dhambi
zangu.Sasa niko tayari kugeuka kutoka kwenye dhambi.Umesema katika neno lako
takatifu Warumi10:9 “Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa
chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika
wafu, utaokoka.”
Sasa nakiri kuwa YESUKRISTO ni Bwana wa roho yangu,Kwa moyo wangu
wote.Naamini kuwa MUNGU alimfufuaYESUKRISTO kutoka katika wafu.Wakati huu
nakupokea YESUKRISTO kama mokozi wangu binafsi na kutokana na Neno lako hivi
sasa nimeokolewa.Asante YESU kwa neema isiyopelekea lesni bali mar azote
hupelekea kutubu.Bwana YESU badilisha maisha yangu ili nilete utukufu na
heshima kwako pekee na sio kwangu.Asante YESU kwa kufa kwa ajili yangu na
kunipa uzima wa milele.Amen
Shuhuda nyingine nyingi za ufunuo wa
mbinguni na kuzimu waweza kuzipata kupitia mtandao ambao ni:WWW.JASIRIMBARIKIWA.BLOGSPOT.COM