Maono
aliyoonyeshwa na Bwana, ndugu Othusitsie Mmusi kutoka Botswana kuhusiana na
Siku za mwisho, Mateso ya majaribu, Dunia katika vita, Uchumi utavyoanguka, Malango
ya kuzimu yamefunguliwa, Mashambulizi ya
kiroho, Hali ya kanisa, utayari wa unyakuo, mbingu na kuzimu.Maonyo makuu
kutoka kwa Bwana ili wote wenye masikio wasikie ili wajiandae wenyewe.
Jumapili
ya mwezi wa 8,tarehe 30 mwaka 2015 mida ya saa 9 usiku.Nilikuwa kitandani
mwangu na ghafla macho yangu ya kiroho yakafunguka Nikaona nje ya paa la nyumba
wakati nipo ndani ya nyumba, nikaona nyota na anga.Ghafla nikawa nje ya
mwili,nikasafiri katikakatika anga kwa mwendo mkubwa.Nikaona nyota na anga.
MATESO YA MAJARIBU KWA WAKRISTO
Bwana MUNGU akaanza kunionyesha mateso ya siku za mwisho kwa
waKristo, Nikawaona waKristo wamekamatwa, wanapelekwa jela, Nikawaona
wachungaji wamekamatwa, Nikaonyeshwa kwenye gazeti na majina ya wachungaji na
makanisa waliofungwa.Nikaona watu wamekaa chini wakipanga nani anayefuta
kufungwa.Haya yalikuwa yakionekana sehemu mbali mbali duniani,Hasa mashariki na
kati.Nilionyeshwa wanawake, watoto na waume wakiuwawa kwa njia mbalimbali, wakikatwa,
roli lililojaa watu waliotekwa,watu walikuwa wakilia na kuogopa wengine
walikuwa wakikimbia kujaribu kujificha na hao watesi.ilikuwa inaumiza
sana.Bwana akasema nami, “Hii ni ishara ya ujio WANGU u karibu”.
Mathayo 24:9-“Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakuwa
watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu.
10 Ndipo wengi watakapojikwaa, nao watasalitiana, na kuchukiana.
11 Na manabii wengi wa uongo
watatokea, na kudanganya wengi.
12 Na kwa sababu ya kuongezeka
maasi, upendo wa wengi utapoa.
13 Lakini mwenye kuvumilia hata
mwisho, ndiye atakayeokoka.”
Mathayo 24:33-“33 nanyi kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya
kuwa yu karibu, milangoni.”
VITABU
VYA KIKRISTO, MAKANISA NA FACEBOOK PEJI
Bwana MUNGU akanionyesha stoo ya vitabu vya kiKristo Nikaangalia
katika mashelfu na vitabu vingi na vilivyoandikwa na waKristo lakini vyote
vinahusu “Furahia maisha”, “Mafanikio katika maisha”, “Funguo za
utajiri”.Nikaangalia karibu vitabu vyote vilikuwa vina masomo hayo ya
kufanana.Nikauliza tafadhali naweza
kupata kitabu kinachohusu Kuzimu ,Mbinguni au Unyakuo.Nikashangaa sana katika
stoo kubwa yenye vitabu vingi sana vya kikristo nikaletewa kitabu pekee kimoja
tuu nacho ni kidogo sana ndicho pekee kinachohusu mambo ya kuzimu na mbinguni.
Bwana MUNGU akanichukua na kunionyesha majina ya makanisa tofauti
tofauti na waanzilishi wake.Katika hayo nikaonyeshwa ujumbe mkuu na unahubiriwa
mara kwa mara katika hayo yote makanisa ni ujumbe unaohusu “Mafanikio katika maisha”.Nikaonyeshwa
kanisa moja lilikuwa dogo sana ndilo lilikuwa linajali kuwa andaa watu wake kwa
ajili ya ujio wake Bwana YESUKRISTO.
Uwiano wa makanisa yaliokuwa yanahubiri bibilia kikamilifu na
kuweka msisitizo kuhusiana na mambo ya milele, ilikuwa ni kama 1:20 kama hesabu
ya makanisa yote ya ile orodha.
Ndipo Bwana akafungua kioo, Nikaona Fesibuku peji(Facebook page)
nyingi sana, Na nyingi zake zilikuwa zikijikita kufundisha watu kuishi
vyema,kufurahia sasa maisha, kupokea baraka na fedha, Baada ya hayo nikaona
peji (page) iliyojikita kufundisha watu nini kinachofuata baada ya haya
maisha,kuzimu, unyakuo, mbinguni na utakatifu.
Nikaangalia watu walio (like) hiyo peji(page) niliona
majina ya marafiki zangu wawili tu,na hao wengine nilikuwa siwa
fahamu.Nilishangaa kwa nini peji(page) zenye ujumbe wa maana zina watu wachache
ukilinganisha na zingine.Na kwanini wakristo wachache sana ninao wafahamu walio
like
peji hizo.
Bwana akaniambia “Mwanangu,
Hii ni hali ya kanisa LANGU, Hii inakuonyesha watu wangu wengi wasivyokuwa
tayari kwa ujio WANGU.Wengi wanasumbikia vitu vidogo badala ya kusumbukia
kunipendza MIMI.Watu wangu wachache sana ndio wako tayari kwa unyakuo
WANGU,Kama ndio ningekuja sasa ,wachache ndio wangenyakuliwa, Waonye sasa, Muda
ni mfupi sana sana.”
2 Timotheo 4:1-4 “1
Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na
waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake;
2 lihubiri
neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya
kwa uvumilivu wote na mafundisho.
3 Maana
utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia
zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya
utafiti;”
4 nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za
uongo.”
YOHANA MBATIZAJI, UNYAKUO, MTAZAMO WA
MBINGUNI NA KUZIMU.
Jumatatu,
mwezi huo huo,31,2015.Asubuhi Bwana akafungua macho yangu ,Nilikuwa nimesafiri
kwenye dunia ndipo likaja jangwa, Nikamuona mtu ambaye inaonekana kama anaishi
hapo katika hiyo nchi.Alikuwa ana mavazi yaliyotengenezewa na ngozi ya mnyama
na manyoya.Nywele zake zilikuwa ndefu,Naye alikuwa akipaza sauti katika jangwa
kama vile akihubiri,Bwana akafanya nielewe kuwa alikuwa ni Yohana mbatizaji,
Nikaona watu wengi wanamjia ili kusikia ujumbe wake.
Bwana
akaniambia, “Ninatuma wahubiri ambao watakuwa kama Yohana mbatizaji na wataandaa
njia kwa ajili ya kuja kwake BWANA, Hao wahubiri wataohubiri TOBA na kufanya
watu WANGU wawe tayari kwa ujio WANGU”.
Malaki 3:1 “1 Angalieni, namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu;
naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu lake ghafula; naam, yule mjumbe wa
agano mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema Bwana wa majeshi.”
Mathayo 3:1-6 “1 Siku
zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na kusema,
2 Tubuni;
kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.
3 Kwa
sababu huyo ndiye aliyenenwa na nabii Isaya, akisema, Sauti ya mtu aliaye
nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake.
4 Naye
Yohana mwenyewe alikuwa na vazi lake la singa za ngamia, na mshipi wa ngozi
kiunoni mwake; na chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu.
5 Ndipo
walipomwendea Yerusalemu, na Uyahudi wote, na nchi zote za kandokando ya
Yordani;
6 naye akawabatiza katika mto wa Yordani, huku wakiziungama dhambi zao.”
JE, UNYAKUO TAYARI ?
Bwana MUNGU akanichukua na kunionyesha
siku hizi hizi duniani, nikiwa nimesimama na viumbe vya kimbingu na nilipo inua
macho yangu juu ,Niliona jambo la ajabu nikaona upinde mkubwa , wingu
linalong`aa na utukufu wa MUNGU ulikuwa unang`aa.Nikaona mianga myeupe
inatembea tembea kwenye mawingu na
niliweza kusikia sauti kutoka huko,Nayo ilikuwa inakuwa kila sekunde ndipo
nikajua hili ni wingu la kupokea ujio wa YESUKRISTO.Nikajua muda wowote tokea
sasa unyakuo unaweza tokea hivyo vitu katika anga vikazidi kukua na kuongezeka hasa
anga la mashariki.Nikaangalia duniani, nikaona watu wengi, wakristo, nao
walikuwa hawaoni lolote walikuwa wakiendelea na shughuli zao wako bize kila
siku na shughuli zao za siku kwa siku wako huru hata kutenda dhambi kama siku
nyingine.Kwa wao ni siku kama siku zingine.Nilijua kuwa muda wowote unyakuo
utatokea.
Bwana akaniambia “Mwanangu,angalia, hawakeshi wala
kuomba,Sio wakeshaji kwa ajili ya ujio WANGU,Wako kwenye usingizi wa kiroho
pamoja na dunia, Hawajui ishara hata ishara zangu za ujio Wangu,Hawajui si muda
nachukua KANISA”
Mwili wangu ukawa mwepesi kwa uzito
nikajisikia kama nimebadilishwa, Nikajiona mwepesi kwa uzito, mwili unaweza
ukawa kwenye hewa na kuja chini, kama vile putolinalo nyanyuliwa na upepo na kushushwa chini tena,Nilikuwa naenda juu
na chini kama vile kuna kitu kinataka kutokea.
-Luka 21:36 “Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika
haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.”
-Ufunuo 22:7 “Na tazama, naja
upesi; heri yeye ayashikaye maneno ya unabii wa kitabu hiki.”
MBINGU
Mara nikapelekwa mbinguni, Kitu cha kwanza nilichokiona kilikuwa ni paradise
hali ya hewa ya mule ilikuwa nzuri sana yenye amani kutoelezeka.Kulikuwa na
mianga kila kona,niliona maeneo makubwa na mashamba yanayoonyesha ni vigumu
kuona mwisho wake.Niliziona bustani nzuri na zenye kupambwa kwa maua na chemi
chem za maji, Nikaona mwanga wa dhahabu unaongaa kwenye bustani, niliona miti
ya mapori iko sawa sawa.Nikaona wanyama wenye nguvu na afya, Nikaona ndege wa
kila aina ,vitu vya mbinguni vya shangaza kupita kawaida nilibaki kujisemea
“wow”, “vizuri sana” “utukufu”.nikasikia furaha na amani isiyo ya kawaida
katika roho yangu.
Nikaja kwenye mji wa Mbinguni , Nikaona mitaa ya dhahabu ,nikaona
majumba,jumba la kwanza nililoliona lilikuwa kubwa sana na zuri mno
lililochukua eneo kubwa ,nilijua kwa ufunuo litakuwa na vyumba vya kulala mia,
vifaavilivyotumiwa kujengea nyumba hiyo havijawahi onekana hapa duniani.
Lilikuwa likiwaka waka,lenye rangi mbali mbali na refu , Nyumba ingine ilikuwa
kubwa kuliko ya kwanza niliyoiona, na yatatu niliyoiona ilikuwa kubwa kuliko ya
pili.Zote zilitengenezwa kwa malighafi za mbinguni.Bwana akaniambia: “Hao
ni watumishi Wangu walionitumikia kwa uaminifu duniani,Pia kuna majengo makubwa
zaidi ya hayo”.
Bwana akaniambia; “Nitakuchukua wewe muda mwingine na
kukuonyesha jumba la Ibrahim na Paulo”.Nikajua majengo yao yatakuwa
makubwa sana kulingana na vile Bwana alivyo nieleza na kutokana na uaminifu wao
na kazi kubwa walioifanya kwa MUNGU imewapa majumba makubwa mbinguni.
Bwana akaniambia “Kuwa mtii na mwaminifu katika kufanya kile
nilichokuitia kukifanya”
-Yohana 14:1-3 “1
Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.
2 Nyumbani
mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda
kuwaandalia mahali.
3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe
kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.”
-1 Wakorintho 4:1-2 “1 Mtu na
atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu.
2 Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa
mwaminifu.”
Niliona sehemu, ambako kila kitu kilikuwa kinang`aa dhahabu, Mwanga wa
dhahabu wa uwepo wa udhihirisho Wake, Maua pia yalionekana ya dhahabu.Sikutumia
muda mwingi hapo.
Mji wote wa mbinguni ulikuwa unamwanga,rangi nzuri,uzuri na
uhai.Nilikuwa nikipiga kwa sauti msifu
MUNGU!,msifu MUNGU !,Pia vitu vingi vilijitokeza kipindi ambacho
nilichokuwa naenda kwa spidi ya mawazo,Nakuwa mara moja katika sehemu MUNGU
aliyotaka mimi niwe.
MTAZAMO
WA KUZIMU
Mara nikajikuta nje ya mbingu ,nkapelekwa sehemu za chini za dunia
,nikaona Kuzimu, kulikuwa na giza la kutisha lililo samba,mapepo wa kila aina,
watu walikuwa wakiteseka na moto na wakilia na kupiga kelele kwa uchungu , “awf
!, awf !” na kuomboleza kwa roho zao kupotea.
VIPAO MBELE VYA MILELE
Mara nikatolewa nikawa ninakuja.Nilikuwa nina paa kwa spidi isiyo ya
kawaida dunia nzima ,nikiona mataifa mbali mbali, wakila tamaduni,watu wa rangi
zote.Nikasikia sauti kutoka kwa MUNGU mbinguni ikisema “Nenda na uwaambie watu wadunia
kuwa umeiona mbingu na kuzimu.Nenda na uwaambie hao,kuwa umeona viumbe mbinguni
na umeona mapepo ya kutisha Kuzimu pia,Nenda na uwaambie wanatakiwa wajiandae
kwa ujio WANGU,Waambie nimetuma ujumbe huu,Waambie nitathibitisha pindi
mtumishi WANGU atapohubiri ujumbe huu,Waambie saa hii, nnaweka thamani zaidi
kuhubiri kuhusu utakatifu na ujio wangu kuliko mafanikio”.
- Zaburi 9:17 “Wadhalimu watarejea kuzimu, Naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu.”
- 1 Petro 1:13-16“Kwa
hiyo vifungeni viuno vya nia zenu, na kuwa na kiasi; mkiitumainia kwa utimilifu
ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo. 14 Kama
watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu;
15 bali
kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika
mwenendo wenu wote;
16 kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.”
- 1 Timotheo 6:10 “Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo
wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu
mengi.”
Ghafla nikaoka katika maono.Nilishangazwa na kuanza kuongozwa kwa kile
nilichokiona na kupitia.
MALANGO YA KUZIMU, roho ZA GIZA, SAUTI YA
BWANA YESUKRISTO.
Jumamosi,Mwezi wa 9, tarehe 19,2015 saa kumi na moja(11) asubuhi.Macho
yangu ya rohoni yalifunguliwa kwa uwazi ,Na kuangalia chini nikaona malango ya kuzimu, Mara nikaona kundi
la roho za giza zilikuwa zikitoka kwa kasi ,nilipoangalia kwa karibu
,nikagundua mapepo ya kila aina wengine wapo kama viumbe warukao na mbwa.Nao
walikuwa wakipanda kuja duniani.
Ndipo
nikasikia kwa sauti ya YESUKRISTO ikiongea wazi wazi kutoka mbinguni ikiongea
kwa sauti kubwa setensi hiz tano.
1. “MALANGO YA KUZIMU YAKO WAZI,
2. LAKINI HAWATAWEZA KUSHINDA,
3. WATU WENGI WATAANGUKA
4. NA WATU WENGI WENGINE WATAINUKA
5. LAKINI ATAKAYEVUMILIA MPAKA MWISHO ATAOKOLEWA”
Ghafla
nilipokuwa nikaona kitu kilichonishtua nikaona wachungaji wengi wakubwa na
maarufu, baadhi wakianguka katika dhambi , na hawakutubu na hakuna anayejua na
wengi kushindwa kuingia mbinguni.
Ilikuwa
ni mchanganyiko ,wa mbio tofauti tofauti, niliweza kerejesha kwa kiasi tu
kumbukumbu yake.Zile roho zilizokuwa zinatoka kuzimu , nyingi zake zilikuwa ni
roho zinazoleta kuhamasisha dhambi za uasherati,uzinzi na kila aina ya
matamanio, ndiyo maana watu wengi walianguka.Nilikuwa nikiruka karibia na
mwisho, kulikuwa na kila aina ya mapepo duniani,kwa kutongoza, na kufanya kila
aina ya uovu.
Nakumbuka
nililia nikisema “Bwana YESU, niokoe niokoe mimi kutoka kwenye huu mtego wa
shetani, tafadhali, tafadhali nisaidie
kuwa mwaminifumpaka mwisho”.Nilikuwa katika machozi nikiomba,kuona jinsi gani
shetani anawaharibu watu.Niliangalia maisha yangu kama nacheza na movi,sasa
mpaka karibia mwisho, kutembea na Bwana,Na ilipofika mwisho ,maono
yalinyanyuliwa juu kwa haraka.Nilitetemeka kutokana na kilichoko duniani na
kuhusu wakristo wengi ambao wanaanguka na kushindwa kuingia mbinguni ,hata wale
wachungaji wakubwa na maarufu sana.
Niliwahi
rudi nyuma na kuacha wokovu kipindi nilipokuwa kijana,Bwana alinionyesha sehemu
na kunipa nafasi ingine.
Katika
hizi siku za mwisho tunatakiwa kila siku kuwa na ushirika mkubwa na
MUNGU,Tunatakiwa kusoma neno la MUNGU,kufunga na kuomba, Tunatakiwa tuwe na
marafiki/makundi mazuri, hatutakiwi kukosa kusanyiko la wapendwa (Kanisa na
Ushirika).
“21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana,
atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba
yangu aliye mbinguni.
22 Wengi
wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa
jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu,
ninyi mtendao maovu.”-Mathayo 7:21-23
- “8 Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba
angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.” 1 Petro 5:8
VITA YA TATU(III) YA DUNIA, GIZA
NA KUANGUKA KWA UCHUMI
Jumatatu ya mwezi septemba,21,2015.Asubuhi mishale ya saa mbili.Nilionyeshwa
kuna wanajeshi wengi sana wakiwa kutoka nchi mbali mbali wakiwa na gwanda
tofauti tofauti kulingana na mpangilio wa nchi zao.Wakiwa tayari kwa
vita,Marekani na walioungana nao,China na walioungana nao,Kulikuwa na bunduki
nyingi sana, wanajeshi wa miguu,Silaha za kila aina.Inaonekana vita ya dunia ya
tatu(3) ikiwekwa tayari kuanza.
Niliona giza la ajabu lililofunika ardhi,anga,na umemeulikuwa haupo kwa
baadhi ya maeneo,Watu wengi wakaenda kujificha katika makanisa ili wapate
ulinzi.Niliona Nikaona sehemu watu wakiwa maelfu ya watu, vijana, watotot na
wakubwa ,wako wakiwa wakimbizi katika nchi zao wenyewe.
Niliona uchumi ulioshuka , kuwa mbaya na watu wakishindwa kutoa fedha
kwenye ATM.Katika maono hayo hali iliyo karibu sana na kujua mapema mapema tarumbeta
italia, kanisa litanyakuliwa na dunia ikaachwa katika dhiki kuu.Ghafla nikatoka
katika maono hayo.
-“ 25 Tena, kutakuwa na ishara katika jua, na
mwezi, na nyota; na katika nchi dhiki ya mataifa wakishangaa kwa uvumi wa
bahari na msukosuko wake;
26 watu wakivunjika mioyo kwa hofu, na kwa
kutazamia mambo yatakayoupata ulimwengu. Kwa kuwa nguvu za mbinguni zitatikisika.
27 Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu
akija katika wingu pamoja na nguvu na utukufu mwingi.
28 Basi mambo hayo
yaanzapo kutokea, changamkeni, mkaviinue vichwa vyenu, kwa kuwa ukombozi wenu
umekaribia.”-Luka 25-28
SHARE KWA WENGINE
Hello there! I could have sworn I've been to this website
ReplyDeletebefore but after reading through some of the post I realized it's new to me.
Anyhow, I'm definitely glad I found it and I'll
be bookmarking and checking back frequently!
Thank you!.Your welcome🙏
DeleteUbarikiwe mtumishi,endelea kuwahimiza watu kuhusu toba
ReplyDeleteAmina sana.Mungu atupe nguvu
Delete