KIFO KILICHOVAA SURA YA UCHUMBA/NDOA.


Kuna lilo chungu kuliko mauti nalo ni hili “Kuoa au kuolewa na mtu mwenye imani tofauti nawe”-Hiki ndicho kifo kinachoumiza kuliko vyote kwa kuwa mtu atakuwa anakufa huku akishindwa jinsi ya kujisaidia kuepuka kifo hicho kwa majuto na kila aina ya uchungu ,mbali na yote ni kuacha kizazi chako chote kikiumia na migogoro mingi ulioianzisha wewe.


Imeandikwa “Nami nimeona lililo na uchungu kupita mauti; yaani, mwanamke ambaye moyo wake ni mitego na tanzi, na mikono yake ni kama vifungo; yeye ampendezaye Mungu atamponyoka, bali mwenye dhambi atanaswa na yeye.”-Mhubiri 7:26

Hapa sisemeni sana mkristo wa dhehebu fulani anaoana na wa dhehebu tofauti na yeye hapana bali nazungumzia watu wawili wa dini tofauti wanapooana huzaa mapooza na kushindwa tuu katika maisha yao.

Suleimani alikuwa mtu wa MUNGU lakini alikoseshwa na wanawake wa kigeni yaani wanawake wasiokuwa na imani moja naye ,Imeandikwa “Je! Sulemani, mwana wa Daudi, hakufanya dhambi kwa kutenda hayo? Lakini katika mataifa mengi hapakuwa na mfalme mwingine mfano wake. Tena alipendwa na Mungu wake, naye Mungu akamfanya mfalme juu ya Israeli; walakini wanawake wageni walimkosesha hata yeye.”-Nehemia 13:26

MUNGU alie hai hapendi mtu wake aoe au aolewe na mtu wa imani isiyo mwamini YEYE MUNGU wa kweli kwa kuwa watu hao hupofusha maono yao wenyewe.

Mfano wa mtu aliyeoa mtu wa imani tofauti naye ni huyu samsoni Imeandikwa “Ndipo baba yake na mama yake wakamwambia, Je! Hapana mwanamke hata mmoja katika ndugu zako, au katika jamaa zangu zote, hata uende kumwoa mwanamke kwa hawa Wafilisti wasiotahiriwa? Samsoni akamwambia baba yake; Mnipatie huyo, kwa maana ananipendeza sana.”-Waamuzi 14:3

Mfano Samsoni alikuwa ni mtu wa MUNGU aliyekua amepewa nguvu kubwa ya MUNGU kwa ajili ya huduma yake lakini hata kabla ya kumaliza huduma ile alikufa baada ya kumuoa Delila ambaye alikuwa ni mwanamke wa imani ingine naye alimbembeleza ili atoe siri zote ; 

Na alipotoa ndipo alipomkabidhi kwa wafilisti wamtese na mpaka kufa kwake.
 Imeandikwa “Delila alipoona ya kuwa amemwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akatuma mtu akawaita wakuu wa Wafilisti, akisema, Njoni huku mara hii tu, maana ameniambia yote aliyo nayo moyoni mwake. Ndipo wakuu wa Wafilisti wakamwendea wakachukua ile fedha mikononi mwao.” Waamuzi 16:18

KUPENDA NI UPOFU LAKINI HAITAKIWI KUWE NI UPOFU KWA MTU ANAYEMJUA MUNGU.
Kwa wewe ambaye unamjua MUNGU hutakiwi kuwa kipofu katika kupenda mwanamke au mwanaume bali katika kila kitu tunatakiwa kuwa waangalifu kwanza.
Imeandikwa “..........; Wala usiwe mpumbavu; Kwani ufe kabla ya wakati wako? “-Mhubiri 7:17

Hata kabla hujamuomba MUNGU kuhusu mtu anayekupenda kama mchumba unatakiwa wewe mwenyewe upime. Je mtu huyo anaendana na viwango vya kiMUNGU au la!?,

Ndio yawezekana ana viwango vizuri vya kidunia mfano fedha,vyeo ,mzuri lakini kama hana viwango vya kiMUNGU hutakiwi kujihisha naye kwenye mahusiano yeyote.

Kitu unachotakiwa kuangalia Je imani yake ni sawa na imani yangu?,kama sivyo unabidi uachane naye hata kama unampenda kiasi gani!
Upendo wenye macho na usio na upofu ndio huu unaoangalia imani, kwa mfano wewe dada ni mkristo na anayetaka kukuchumbia ni mpagani/mbudha au muislamu hapo unabidi uachane naye kwa kuwa atakusumbua popote pale siku za mbeleni.uachane naye hata kama unampenda!.

Asilimia 99.9% ya wanandoa walioana wakiwa na imani zao tofauti mfano mwislamu ameoana na mkristo wamejikuta wakilia na kujutia maisha yao yote kutokana na migogoro isiyokwisha vizazi hata vizazi vyao vyote.

Angalizo:Watu wengi wakiona wamekataliwa kuchumbia kwa sababu ya imani zao mmoja wao hudai kubadilisha dini ili tuu apate kuolewa au kuoa ,Ukweli jambo hilo husumbua wengi kwa kuwa mtu huyo alibadilisha dini hakubadilisha akiwa anamaanisha hivyo baada ya ndoa hurudi alipotokea yaani hurudi dini yake ya awali ambayo alikuwa nayo kabla ya kuolewa /kuoa.

HASARA ZINAZOTOKEA KATIKA NDOA YA WATU WALIO NA DINI TOFAUTI
Hakuna faida kabisa ya kuoa au kuolewa na mtu wa dini yaani imani tofauti nawe hata iwe mnapendana kiasi gani kwa sababu:-

1.Mtashindwa vita zote za kiroho kwa kuwa hamna imani yenye umoja
Kutokana na dini kwa tofauti ndani ya ndoa na imani kuwa tofauti hakuna vita ya kiroho ambayo mtaishinda humo ndani ya nyumba.
Mfano: “biashara yenu imetupiwa mikosi ili isifanye vizuri,”Ninyi kama wanandoa ambao mnadini tofauti hamuwezi kutoa hiyo mikosi hata siku moja kwa kuwa mmoja ataomba kwa jina la YESU;
 mwingine ataomba kwa jina lingine ambalo si la MUNGU kiasi kwamba  hakuna kitakachojibiwa kwa kuwa MUNGU wetu hapendi kushirikiana utukufu na miungu mingine.
Kwa hiyo mtaishi katika mikosi hiyo pasipo kuweza kuitoa mikosi hiyo.

2.Kutokea kutafuta miungu mipya ya kuiabudu.
Watu wengi hujikuta wakijuta na kulia huku wakisema moyoni hawakudhani kama mpenzi wake huyo angebadilika au angekuwa hivyo;
Na hatima yao katika kutafuta suluhu ya vita ya kiroho zinazo wakabili hujikuta wakitafuta miungu mingine jambo ambalo huwaletea shida zaidi.

3.Usishangae kusalitiwa muda wowote / KUTELEKEZWA .
Ukiwa kwenye mahusiano ya mtu asiye na imani au dini moja ujue kabisa na tena ujiandae kabisa kusalitiwa muda wowote ule kwa kuwa pale ambapo wewe utaona amekusaliti labda kwenye dini yake inaruhusiwa!!!.

Utasalitiwa kwa staili za kila namna na muda mwingine utakuwa ukibembelezwa na kuhisi ni mapenzi kumbe unatafutiwa njia ya kusalitiwa Imeandikwa “Yakulinde na mwanamke mwovu, asikupate, Na kukuponya na ubembelezi wa mgeni.”- Mithali 6:24
Delila ambaye alikuwa ni mke mwenye imani tofauti na samsoni alimbembeleza sana Samsoni mumewe ili amtajie siri za nguvu zake ikiwa kama njia ya kumsaliti  pasipo samsoni kujua ,Imeandikwa “Basi mkewe Samsoni akalia mbele yake, akasema, Wewe wanichukia tu, wala hunipendi; wewe umewategea kitendawili hao wana wa watu wangu, nawe hukuniambia mimi. Naye akamwambia, Angalia, sikumwambia baba yangu wala mama yangu, nami nikuambie wewe?” Waamuzi 14:16

Naye samsoni alisalitiwa na delila baada ya kumtajia siri ya nguvu zake.Hii ndiyo hasara kubwa ya kuoa au kuolewa na mtu asiye kuwa na imani moja pamoja nawe kwa kuwa muda wowote utajikuta ukisalitiwa.

4.KUFA KABLA YA WAKATI.
Imeandikwa “..........; Wala usiwe mpumbavu; Kwani ufe kabla ya wakati wako? “-Mhubiri 7:17.Hasara ingine ambayo ni kubwa kuliko kawaida kwa watu wanaoana wadini mbili tofauti ni “kufa kabla ya wakati wake” mtu anaweza akawa amekufa ila bado anaishi kama  kopo tuu,

Kwa kuwa maono yake yamefutika ,lengo la yeye kuishi duniani hawezi kulitimiza na kama ana watoto hawezi kuwasomesha tena wala kuwasaidia kwa lolote lile.
5.MIGOGORO ISIYOKWISHA KIZAZI HADI KIZAZI.
Kutokana na uhusiano wa kuwa si watu wa dini moja au imani moja ya kueleweka hivyo ndivyo itavyokuwa migogoro kila kukicha mfano watoto waabudu wapi anaposali baba? au anapo sali mama?Huo ni mgogoro ambao unajitegemea.Na migogoro mingine mingine chungu mzima!.

KITU CHA KUFANYA KAMA KWELI HUTAKI KUJUTA:
i.Kataa kuolewa na mtu asiye wa dini sawa nawe au ambaye anabadilisha dini kwa kuwa anataka akuoe au aolewe na wewe hata kama unampenda.
Kwa msimamo wako huo MUNGU atakupa mtu ambaye atakufaa kuliko huyo ambaye atakuletea maumivu maisha yako yote.
ii.Kama upo kwenye mahusiano na mtu ambaye ni dini tofauti nawe na hamjafunga ndoa pia hamna mtoto,Amua kuachana na huyo kwa kuwa kuna safari kubwa ya majuto inakuvizia kupitia huyo mtu.
Kwako wewe mapenzi hayatakiwi yawe upofu kwako ,ili usijelia vilio ambavyo wengine wanalia sasa hivi duniani kote.
 Kuwa na msimamo kwa kuwa MUNGU wako anaweza kukutafutia mtu ambaye ni mzuri zaidi ya huyo ambaye si wa dini yako ,
MUNGU anachosubiri kutoka kwako ni kuona kama una imani  na kama una imani utakuwa na msimamo wa kujenga hatima ya maisha yako kwa kuachana na mwanamke/mwanaume asiye wa dini moja nawe na kusubiria kuona MUNGU anavyokupatia wakufanana nawe!.

JE UNAONA HUNA UWEZO WA KUMUACHA HUYU ASIYE WA IMANI YAKO?,AU JE UNADHANI HUTAPATA MWINGINE UKIMKOSA HUYO ?
Omba maombi haya kwa imani na kumaanisha nawe utaona matokeo makubwa sana na ya ajabu maishani mwako:
Omba sema kimoyo moyo au kwa sauti “Baba MUNGU katika jina la YESU ninakuomba uondoe moyo wangu kwa mtu yeyote au sehemu yeyote ulipofungwa ambapo si sahihi kwa maisha yangu.Nakuomba ee MUNGU wangu ufungue moyo wangu ili uwe huru .
Nawe Baba MUNGU katika jina la Yesu nakuomba unipe mume/mke wa maisha yangu mwenye imani ya kukuamini wewe MUNGU na sio miungu mingine ,unipe huyo mume/mke ambaye atakaa nami kwa furaha na amani sikuzote.Ninakushukuru sana MUNGU kwa kuwa kwa maombi haya mtandaoni  unakwenda kunipa mtu wa kufanana nami na kuniunganisha naye kuwa mke/mme wangu milele kwa utukufu wako. Asante YESU kwa kunipa ushuhuda.”
Kupitia maombi haya moyo wako umefunguliwa nawe utakaa na kushangaa kumpata mtu sasa ambaye ni wa imani moja nawe ambaye ndiye MUNGU amependezwa wewe kuwa naye.Utashangaaa maajabu ya BWANA !!.

KWA WANADAMU NI SIRI LAKINI SI KWA MUNGU"KUPIGA PUNYETO"


KWA WANADAMU NI SIRI LAKINI SI KWA MUNGU
“KUPIGA PUNYETO / PUCHU / PULI / KUJICHUA“masturbation”.
Kweli yaweza kuwa ni siri kwa wanadamu lakini haiwezi kuwa siri kwa MUNGU kwa kuwa MUNGU anajua mambo yote hata yale yaliyositirika na kufichika.

Kitendo cha kujichua yaani masturbation kina starehe ndogo na kuwa na madhara mengi kuliko kawaida, kujichua kuna madhara ya kimwili na kiroho pia.

Tatizo la kujichua si kwa wanaume tuu bali ni hata kwa wanawake ,na sii kwa wasiooa na kuolewa bali hata kwa walio olewa na walio oa baadhi yao hujikuta wakipendela kujichua pasipo kujua kuwa kuna roho za giza ambazo ni maalumu kwa ajili ya kuwasababisha waendelee kujichua tuu.

Kuna wakristo wanawake zao lakini bado wanaona bora kujichua kuliko kulala na wake zao,Kuna wanawake ambao wana waume zao kabisa lakini hawaoni raha ya kufanya tendo la ndoa na waume zao kama vile wakijichua wao binafsi.
Wewe haujajiumba bali umeumba na MUNGU kwa ajili ya kumtukuza yeye MUNGU pekee kwa kuwa mwili wako ni hekalu la ROHO mtakatifu “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;”- 1 Wakorintho 6:19

Mbaya zaidi ni kwamba shetani anazidi kuboresha utendaji wa dhambi kwa kuwa tengenezea watu mashine za kujichua kwa kuwa anajua kwajinsi wanadamu wanavyozidi kutenda dhambi na ndivyo yeye anaweza kutenda kazi ndani yao.

Kujichua au kupiga puchu kumekuwa kwa staili mbali mbali  mpaka zingine zimekuwa ni za kitaalamu sana zilizoendelezwa  na shetani ili watu wajichue kupitia mashine,midoli yaani setoyz maalumu kwa ajili ya kujichua .Kujichua husababisha matatizo ya kisaikolojia na kuathiri mfumo wa mwili na roho pia!.

Ukweli ni kuwa kujichua ni chukizo mbele za MUNGU. Imeandikwa “Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili;

 27 wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.”- Warumi 1 :26-27

Hawezi kufanya punyeto/kujichua/masturbation pasipo kuwa na hisia za kutamani kufanya tendo la ndoa na kwa kuwa na mawazo tuu ya kutamani kufanya ngono ni dhambi mbele za MUNGU kwa kuwa imeandikwa“lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.”- Mathayo 5:28

Hivyo si mpango wa MUNGU watu wakae katika maisha ya kujichua ,kupiga puli, kurusha ndege na kuwaka tamaa.

Ni afadhali tena ni heri mtu aoe au aolewe kuliko kuendelea kujichua “Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa”- 1 Wakorintho 7:9

Vitu vinavyosababisha kujichua.....
Tamaa ya kufanya,uzinzi, uasherati na tamaa kubwa ya kufanya mapenzi huchangia kujikuta unajaribiwa kufanya masturbation yaani punyeto.Kuna vitu vinachochea kujichua vitu hivyo ni pamoja na:-

i.Kuangalia picha za kawaida zenye hisia kali au hata picha za ngono yaani (PORNOGRAPHY).
Picha zenye unusu uchi za kwenye mitandao au tamthilia zenye kuonyesha matamanio matamanio hupelekea mtu kuwaza kuanza kujichua

ii.Kushawishika kumakinika na mavazi ya uchi na yenye hisia kali kuyatazama.
Mavazi ya ajabu ajabu yenye kuwekaushawishi kutokana na kukaa wazi kwa mwili.

iii.Mapepo na majini
Kuwa makini kwa kuwa kujichua ni moja ya kazi ambazo shetani anapata nafasi kujiingiza katika maisha ya watu kwa kuwa kuna mapepo na majini kwa ajili ya kuwafanya watu wasipende kuolewa wala wasioe ila wapende kujichua tuu.

Watu wengi wana mapepo na majini yanayosimamia kabisa kuwahamasisha kujichua mara kwa mara na hata kuwafanya wasiwe na hamu na wake zao wala wasiwe na hamu na waume zao bali wawe na hamu kubwa tuu ya kujichua.

iv.Upweke ulio na uvivu mkubwa.
Uvivu ni hali mbaya sana kwa kuwa mara nyingi mtu anaokuwa mvivu naye shetani humtafutia kazi au jambo la kipuuzi ili ulijaribu na hapo unapojaribu siku moja nivyo inavyo endelea siku zote kukuathiri katika maisha yako.

Kwanini unatakiwa uache kujichua?/Hasara za kujichua !
Kujichua kunaleta madhara kimwili na kiroho pia yaani kujichua kwa mtu wa jinsia ya aina yeyote ile huleta madhara kattika mwili wake pia na roho yake.

Madhara ya kimwili yatokanayo na kujichua / kupiga punyeto ni:- 
1.Kusahau sahau kusikokuwa kwa kawaida
Kujichua kukute kule kuna sababisha madhara makubwa kisaikolojia ambayo hupelekea kushindwa kukumbuka vizuri.Sio kana kwamba ni kusahau kwa kawaida bali ni kule kusahau kusikokuwa kwa kawaida.

2.Kunyonyoka au kuishiwa na nywele.
Kufanya sana kujichua kulikokithiri husababisha kutokuuota kwa nywele kichwani na kwapani hasa kwa wadada.

3.Kichwa kuuma na kutapika mara  kwa mara
Mtiririko wa damu huathirika sana pindi mtu anapojichua kwa kuwa mwili wa mtu huyo utahitaji ajifikirishe kama yupo na mwanamke kumbe hana mwanamke.Au yupo na mwanaume kumbe hana mwanaume.

Mwishowe mfumo wa damu huleta kutokusawazika na kuchangia maumivu makali ya kichwa(chronic head-ache)

4.Kuishiwa nguvu za mwili sana
Mtu anayejichua huishiwa na nguvu isivyo kawaida kwa kuwa kabla anakuwa anauwezo mkubwa wa kujichua mara nyingi sana akijisikia raha pasipo kujali nguvu zinazopotea. 

5.Kutokupenda kuwa na ushirika na wengine
Mtu anayejichua huwa mara nyingi hapendi sana kushirikiana na wengine kwa kuwa tendo hilo la kujichua hufanyika sirini pasipo mtu yeyote.

6.Huchangia matatizo ya nguvu za kike na kiume.
Watu wengi hawajui kuwa matatizo mengi ya nguvu za kike/kiume hutokana na kujichua.

Madhara ya kiroho yatokanayo na kujichua / kupiga punyeto ni:- 
Moja ya tatizo kubwa la kiroho litokanalo na kujichua au kupiga punyeto ni kukosa ukaribu na MUNGU wako unakosa ushirika na MUNGU wako.Ni mbaya kuwa kijana mzuri lakini uzuri wako hauonekani mbele ya MUNGU kwa sababu ya kujichua.

i.Unakuwa najisi.
Imeandikwa “Na kila nguo, na kila ngozi, ambayo ina shahawa, itafuliwa kwa maji, nayo itakuwa najisi hata jioni.”- Mambo ya Walawi 15:17.Unapojichua unafanya MUNGU akuone wewe u najisi utaona ni hasara kubwa kiasi gani kwa aliye kuumba akuone kuwa u najisi.

ii.Unashindwa kudumu kutokana na kukosa neema ya MUNGU…
Imeandikwa “Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.”- 1 Yohana 2:17.Duniani si makazi yetu bali tu wapitaji kwa kuwaktu akifa atahukumiwa kwa yale aliyoyatenda kipindi alipo kuwa hai duniani.

Kwa hiyo kwa sababu ya dhambi ya kuwaka tamaa ya ngono inayopelekea hadi kufanya punyeto inaweza sababisha wewe kuto enda katika makazi ya mbinguni na kukufanya uende makazi ya motoni milele.
iii.Kujichua ni kunaabudu sanamu pasipo kujijua…
Unapojichua unakua unaabudu sanamu pasipo kujijua,huwezi amini bali neno la MUNGU ndivyo linavyotueleza kuwa kila afanyaye tamaa mbaya ni sawa na anaye abudu sanamu.

Imeandikwa “Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu;”- Wakolosai 3:5

Ikwepe hatari hii ya kujiona kana kwamba unamwabudu MUNGU wa kweli na kumbe MUNGU haoni kama unamwabudu yeye bali sanamu, kwa sababu ya kujichua ambako ni sawa na kuabudu sanamu.

JINSI YA KUACHA KUJICHUA NA KUDHIBITI MADHARA YAKE KUACHANA NA VISABABISHI NA KUUTUMIA MUDA NA WENGINE KWA UZURI
Ukiweza kuzuia tamaa ya mwili ujue umeweza kuzuia kufanya kujichua Imeandikwa “Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu?”- Yakobo 4:1.

BADILI MWENENDO WAKO KWA KUKATAA KUWA HUNA LA KUFANYA.
Amua leo kuacha kabisa kujichua /kupiga punyeto/kupiga puchu/kurusha ndege/ kwa kuwa MUNGU ana mipango mizuri na mikubwa nawe ila kinacho kuchelewesha ni huku kujichua.

Kuna vijana wengi tena ambao hawajaoa au kuolewa na bado wajitahidi na kuweza kuacha kabisa kujichua na wanafurahia uhusiano wao na MUNGU.Nawe unaweza amua leo,amua sasa!

Baadhi ya hatua za kuacha kujichua ni hizi:-
1.Muda uliokuwa ukiutumia kuangalia porno tumia muda huo huo kusikiliza na kuangalia mafundisho ya neno la MUNGU kutoka kwa watumishi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa.

2.Badala ya kuangalia video za ngono sasa angalia video za mahubiri ya injili

3.Badala ya kusoma magazeti yenye picha za uchi yaani zenye kuleta msisimko sasa anza kusoma BIBILIA kusoma magazeti yenye neno la MUNGU.

4.Acha kufuatilia mitandao ya ngono sasa anza kufuatilia mitandao ya watumishi wa MUNGU soma mafundisho yao na udownload video zao zisikilize.

5.Tumia muda wako ule ule uliokuwa unajichua /kupiga punyeto kuanza kuomba MUNGU.Kama ulikuwa unajichua mara 5 kwa siku ndivyo hivyo hivyo unabidi ubadilike na uanze kuomba MUNGU mara 5 kwa siku.

6.Ulikuwa ujifunza staili mbali mbali za kujichua sasa ziache zote na uanze kujifunza njia mbali mbali za kumjua MUNGU,jifunze namna ya kusoma neno la MUNGU, jifunze namna ya kuomba na kufunga kisahihi, jifunze namna ya kuombea wengine kisahihi.

7.Pendelea kufanya mazoezi ya mwili kama vile kukimbia kila jioni na asubuhi kwa ajili ya kupunguza taratibu madhara yaliyopata mwili kutokana na kujichua/kupiga punyeto.

--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------     “Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo.”- Wagalatia 5:13
-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Kuacha KUJICHUA/KUPIGA PUNYETO inawekana kabisa badilika sasa utakuwa kijana ,mwanamke/mwanaume bora mwenye kupendeza zaidi  katika afya yako,roho yako hata kwa MUNGU wako.

Usiishi kama wengine wanavyoishi bali ishi kwa kuwa wewe ni wa MUNGU basi unabidi umfuate MUNGU kweli kweli  kwa kuzikimbia tamaa zote za ujanani.

 Imeandikwa “Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.”- 2 Timotheo 2:22



Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...