USIKUBALI KUDAIWA DAMU YA MWINGINE

“………………………. lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako.
19 Lakini ukimwonya mtu mbaya, wala yeye hauachi ubaya wake, wala njia yake mbaya, atakufa katika uovu wake; bali wewe umejiokoa roho yako.”
- Ezekieli 3: 18-19

Unapojua sasa kuvaa suruali kwa wanawake,mawigi,wiving,kubandika kope bandia,nywele bandia au kuziweka nywele dawa na kubadili asili yake,kutumia njia za uzazi wa mpango,kondomu,miziki ya kidunia,muvi za kidunia hata kutumia vito(jewelery) yaani bangili, hereni, mikufu,
pete nakadhalika ni DHAMBI tena ni MACHUKIZO makubwa mbele za MUNGU.

Kama ukimuona mtu anatumia hivyo vitu na ukaacha kumwambia kuwa hivyo vitu BWANA YESU hapendi uvitumie basi damu yake iitadaiwa kwako hata kama wewe huvitumii vitu hivyo na umtakatifu bado utakuwa na damu ya mwingine mikononi mwako.


Hata kama ni mama yako,dada yako,mke wako,mchungaji, mwanakwaya au rafiki yeyote anatumia vitu hivyo wewe unatakiwa umwambie ili usidaiwe damu yake.Yeye akibisha au akikataa au akifanya vyovyote vile baada ya kumwambia hiyo haikuhusu kwasababu utakuwa umeshajitoa kudaiwa damu yake.
Na hapo damu yake itakuwa juu yake mwenyewe.Usikubali kwenda kuzimu eti tuu kwa sababu ulishindwa kumwambia mtu ukweli wa MUNGU na kubeba damu ya mwingine.

Unachopaswa Ni KUWAAMBIA na usiwe sehemu ya mabishano kwa sababu kwa kumwambia tuu utakuwa umeshajiokoa kudaiwa damu yake.

 Hata kama unaogopa tafuta njia yeyote ya kumwambia waweza kupiaga chapa(print) baadhi ya shuhuda na kumpelekea au kumuwekea video kwenye DVD au simu akasikilize shuhuda hiyo.Akibadilika au asipobadilika hilo halikuhusu bali utalolijali ni kujiondoa usidaiwe damu yake mikononi mwako kutokana na wewe kutokumwambia.
Kuwa makini sana kwa kuwa safari ya mbinguni haijali mahusihano kwa kuwa kila mtu atahukumiwa kwa uovu wake[Ezekieli 18:20].Hivyo mume anaweza kwenda mbinguni na mke kwenda kuzimu au vyovyote vile yawezekana.


Jihadhari kwakuwaambia, hata kama ni mchumba , mke ,bibi hata awe mama mkwe MWAMBIE kwa njia yeyote ile akibadilika au asipobadilika hilo halikuhusu kwa kuwa wafanya hivyo ili damu yake usidaiwe akawa kwazo kwako kuingia mbinguni.


Kumbuka: MAAMUZI NI HAPA DUNIANI, BAADA YA HAPA NI HUKUMU YA MILELE, Ukikosea ni milele na ukipatia ni milele kuwa MAKINI usidanganyike na ulimwengu huu upitao.




Asante kwa kufuatilia mafundisho haya ,pia waweza kubofya kwenye link ili kufuatilia masomo kama vile:-

1. IBADA YA SANAMU HAIWEZI KUOKOA

2.UBATIZO KATIKA USAHIHI WAKE

3.MAMBO YA KUFANYA ILI UONDOKANE NA TABIA MBAYA INAYOKUSUMBUA   

4.utukufu wa MUNGU tuliopewa.

 

5.Hata ndoa aliyoianzisha MUNGU mwenyewe ilikuwa inasababu kubwa za kuvunjika lakini ..... ... . . . .

 

'Na masomo mengineyo mengi utayapata ukizidi kufuatilia.Ubarikiwe'

Shirikisha wengine na usisite kutoa maoni yako......

 


No comments :

Post a Comment

Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...