Chochote unachomtendea mtu yeyote hata uwe humfahamu ujuehicho ndicho unacho mtendea YESUKRISTO !


Jiulize unawatendea nini ?,  watu mbalimbali unaowajua au usio wajua hicho ndicho unamtendea MUNGU!.

Haipingiki kuwa kuna kwenda mbinguni kama umemkubali YESU au kwenda kwenye moto wa milele kama umemkataa baada ya kifo.

Imeandikwa “32 na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi;

 33 atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto.
 34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;

 35 kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha;
 36 nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia.

 37 Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha?
 38 Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika?

 39 Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia?
 40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.

 41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;

 42 kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe;
 43 nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama.

 44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie?

 45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.

 46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.”-mathayo 25:33-46.
Anaposema nilikuwa uchi mkanivisha nilikuwa na njaa mkanilisha  na kadhalika,Hayo yote ni matendo ya upendo na Hii  inamaanisha kuwa Upendo wa kweli ndio utamfanya mtu aweze kwenda mbinguni,

Jiulize unamtendea nini  jirani yako,nduguyo,rafiki yako,hata adui wako ?,Chochote unachomtendea mtu yeyote hata uwe humfahamu ndicho hicho unamtendea YESUKRISTO.

Imeandikwa “40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.”-Mathayo 25:40

Je kuna baadhi ya watu unawadharau ?, Jua unamdharau YESUKRISTO au kunabaadhi ya watu unawaona sii kitu yaani wewe uko juu yao jua unamshusha YESU.

Imeandikwa “akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.”- Mathayo 18:3

Waweza jiuliza inamaanisha nini ?
Watoto hawatunzi chuki,hawa hesabu mabaya ya mtu, watoto ni wepesi wa kusahau mabaya waliotendewa ,hawahesabu hata mazuri waliowatendea watu . . . .hizi ni baadhi tuu ya  tabia ambazo wanazo watoto ambazo MUNGU pia anataka tuwe nazo ilituu kuweza kumpenza YEYE.

Tunatakiwa tuwe na upendo wa kweli ,upendo wa vitendo kutoka moyoni.Imeandikwa "Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu" Wakolosai 3:14

Mbinu pekee ya kuingoja parapanda ya mbinguni / kuja kwake YESUKRISTO !!.

Unaweza kujua kabisa siku hata muda wa kufa kwako lakini hakuna atayejua siku wala muda wa kuja kwake YESUKRISTO mara ya pili .

Zaidi ametupa kujua ishara zitazotokea katika nyakati hizoo  tuu na sio muda au siku kamili ya kuja kwake duniani tena !!.

Imeandikwa “32 Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba.  33 Angalieni, kesheni, ombeni, kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo.”- Marko 13:32-33.

YESU anatupenda sana kwa kuwa pamoja na kutotaja muda wala nyakati za ujio wake lakini ameeleza mbinu ya kufanya ili tusije aibika pindi atakapokuja mbinu yenyewe ni kukesha, kuwa macho kiroho.

Hakuna binu tofauti na hii kama wewe uu msafiri kuelekea mbinguni hii ndio pekee mbinu.

Imeandikwa “Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa”-mathayo 25:13.Unaweza kujua mambo yajayo mengi sana hata kujua siku zako kwa idadi yake ulizopewa hapa duniani lakini hakuna mtu yeyote wakujua muda au saa kamili ya kuja kwake YESU .

Siri na mbinu kuu ya kumsubiri YESUKRISTO nikukesha yaani kuwa macho kiroho masaa yote kwa kuwa hatujui saa wala muda.Imeandikwa “Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu.”-mathayo 24:42.

Imeandikwa “(Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)”-ufunuo 16:15.

Sababu ya kukesha yaani kuwa macho kiroho ni kwa kuwa hatujui na hakuna anayejua muda wala saa pia atakuja kama mwivi.

Hata ndoa aliyoianzisha MUNGU mwenyewe ilikuwa inasababu kubwa za kuvunjika lakini ..... ... . . . .

Toka ndoa ya kwanza ,yaani ile aliyeifungisha na kuianzisha MUNGU mwenyewe ilikuwa inasababu za kutosha kuvunjika kama adam na hawa asingejua kuwa hawana ukamilifu.

Imeandikwa"Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake, na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.

 Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.”-Mwanzo 2:21-23

Hapo tunaona MUNGU mwenyewe anamtafutia adam mke toka ubavuni mwake yaani mke kutoka kwa BWANA.
Lakini ndoa yao ilikuwa inasababu  za  kutosha kuvunjika ,kwa kuwa Hawa alifanya makosa na kudanganywa na nyoka mpaka akala tunda ambalo aliamriwa asile na MUNGU hata kumkosesha mumewe adam kwa kumpa naye ale tunda hilo.

Imeandikwa" Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala.Bwana Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, . . . . . . " –Mwanzo 3:12-13

Ndoa za leo ambazo mwanamke au mwanaume akifanya kosa moja anapata talaka,au anapigwa, anaachika au anateswa na kusemwa na mumewe au mkewe vibaya jifunzeni kuwa hakuna ndoa iliyokuwa kamilifu ila kila mwanandoa anachukulia udhaifu wa mwenziye.

Adam alikuwa na sababu ya kuachana na hawa kwa kuwa hawa ndio aliyesababisha machungu ya kulaaniwa na MUNGU lakini kwa kuwa alijua na kutambua kuwa yeye si mkamilifu na anamapungufu hivyo alimchukulia kwa hayo mkewe.Kwa wanandoa waleo na wanaoingia kwenye ndoa hivi karibuni yapasa kujua kuwa hakuna aliyemkamilifu  hata yule atokaye kwa MUNGU (mke mwema/mume mwema).

Ndoa ya Sara na Ibrahim ilikuwa na utasa kwa muda mrefu hata uliwafanya wao wenyewe kukata tamaa,hiyo ingeweza kuwa ni sababu au kigezo cha ibrahimu kuachana na Sara kwa kuwa alikuwa hazai. Lakini hakuachana naye kwa kuwa alikuwa akijua kuwa hakuna aliye mkamilifu kila mtu anamapungufu.

Sasa kuna wanandoa wanaachana kisa tuu mwanamke au mwanaume ni tasa ,Imeandikwa“Na Sarai alikuwa tasa, hakuwa na mtoto”- Mwanzo 11:30. Ibrahimu hakumuacha mkewe wala hakuchukua kama sababu ya kumuacha mkewe Sara.

Hakuna popote duniani ndoa isiyopitia misukosuko ,toka agano la kale mpaka leo agano jipya hakuna ndoa isiyokuwa na changamoto ila tuu inatofautiana namna ya kuzikabili changamoto hizo kwa kuwa wengine hukabili changamoto hizo kwa kuachana na ndoa zao,wengine huvumilia na kuzishinda.

Imeandikwa “Yakobo akamghadhibikia Raheli, akasema, Je! Mimi ni badala ya Mungu, aliyekuzuilia uzao wa mimba?”- Mwanzo 30:2.  tena Imeandikwa “Naye Raheli alipoona ya kuwa hamzalii Yakobo mwana, Raheli alimwonea ndugu yake wivu. Akamwambia Yakobo, Nipe wana; kama sivyo, nitakufa mimi.”- Mwanzo 30:1

Si kwa yakobo bali hata  Raheli alikuwa yuko radhi hata kuachana na ndoa hiyo,hataalikuwa yuko tayari hata kufa kwa matatizo aliyokuwa nayo yakutukuwa na mtoto na aibu aliyokuwa anakabiliana nayo kipindi hicho,lakini alivumilia na kuikabiliana na hiyo changamoto iliyo tendganisha ndoa yake.

Hakuna ndoa isiyokuwa na changamoto ,kama changamoo yakupata mtoto huna basi itakuwepo kuwa na mume /mke mkali ,utakuwa na changamoto ya kuwa na mume/mke asiye eleweka kazi yake ni kuleta hasara tuu.

Imeandikwa “.Isaka akawa mwenye miaka arobaini alipomtwaa Rebeka binti Bethueli, Mshami, wa Padan-aramu, ndugu wa Labani, Mshami, kuwa mke wake. Isaka akamwomba Bwana kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. 

Naye Bwana akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba.Watoto wakashindana tumboni mwake. Naye akasema, Ikiwa ni hivi, kuishi kwanifaa nini? Akaenda kumwuliza Bwana.” Mwanzo 25:20-22

Kuna mtazamo tofauti kwa dunia ya sasa pale watu wanapo oa au kuolewa wanahisi kama wakiolewa na mume sahihi wa maisha yao  au mke sahihi ambao Bwana amewatengea kwa ajili ya maisha yao hawatapata kuona kikwazo chochote hawatapata shida kitu ambacho si kweli.

Kila wanandoa unaowaona wanasababu kubwa kabisa ya kuachana na ndoa zao ila haachi kwa kwa kuwa wanatambua ya kuwa hakuna aliye mkamilifu.

Imeandikwa
 “Palikuwa na mtu mmoja wa Sora, wa jamaa ya Wadani; jina lake akiitwa Manoa; na mkewe alikuwa tasa, hakuzaa watoto.”- Waamuzi 13:2



Kama hakuna aliyemkamilifu baasi hakuna ndoa ambayo itakuwa ni kamilifu yaani hakuna anayemkosea mwenziye ,bali wanavumilia huku wakijua hakuna aliyemkamilifu.


Ndugu ukiona ndoa ni mbayaa labda kwa sababu ya mwanaume au mwanamke na unatamani ndoa ya mwingine au uolewe /kuoa  mke au mume mwingine ,ujue wazi kuwa unayeitamni inamatatizo kama  kawaida labda tuu yametofautiana tuu kwa jinsi anavyo yachukulia.

Kwanzia leo kaaa chunguza utagundua hata wale wanao sherehekea  ndoa zao kuwa zimeduumu kwa miaka mingi  utagundua kuna shida ziliwahi wakumba na zilikuwa ni sababu tosha za kuachana kwao ila wakazivumilia na wakazishinda .

Ukichunguza hata ukiweza wauliza we waulize wao wanao sherehekea miaka mingi ya ndoa zao utagundua kuna ukweli kabisa mume au mke alikuwa anatabia ya kutoka nje ya ndoa lakini mume au mke alimuonya alimvumilia akijua yeye pia si mkamilifu.

Anza kwa uzuri kutazama changamoto katika ndoa yako na kuzitatua na sio kukimbilia kuachana kwa kuwa kila ndoa hapa duniani inasababu za kutosha kuvunjika lakini  kwa ajili ya kutambua hata ikivunjika hakuna aliye mkamilifu hiyo pekee husababisha kuvumiliana katika ndoa bila kujali mapungufu makubwa aliyonayo mume wake au mke wake.





Ukweli ambao waweza kuufanyia uchunguzi /uthibitisho wa YESUKRISTO maishani mwetu !!.



Duniani tuko kwa muda mfupi sana kitu ambacho watu wengi hatupendi kukisikia ingawa ni kweli,  Imeandikwa “Mwanadamu siku zake zi kama majani; Kama ua la kondeni ndivyo asitawivyo.”-Zaburi 103:15 .

 Na ndani ya hiyo miaka michache tunayoishi hapa duniani kwa ujumla imejaa shida na dhiki. Imeandikwa “Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu.”-Ayubu 14:1

Mtu anazaliwa anahangaika anasoma anajenga majumba ,anaoa/kuolewa anazaa watoto ,anakuwa hata nakila fahari yoyote lakini mwishowe anakufa.

Baada ya mtu kufa kuna machaguo mawili (2) ama kuishi milele katika moto wa milele kama ulimkataa YESU hapa duniani au kuishi na BWANA YESU kwa amani na furaha milele endapo ulipokuwa duniani ulimkubali YESU. 

Imeandikwa “Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake.”-Mathayo 25:41

 Hakuna njia yoyote tofauti na njia ya YESUKRISTO ili kwenda mbinguni(makazi ya milele na ya raha baada ya kifo hapa duniani).Imeandikwa “Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.”- Yohana 14:6.

Kama umekusudia kuishi milele na kutokuangamia na moto wa milele katika siku za mwisho baasi wewe chagua leo kumfuata YESU na uachane na njia tofauti ambazo zinadai eti utaenda mbinguni pasipo kumtambua YESU kama MUNGU na kama njia pekee.

Ukweli ambao waweza kuufanyia uchunguzi: YESUKRISTO anajithibitisha mpaka leo kwa kutenda miujiza ya kuponya watu,kufufua watu, hata kutoa mapepo kupitia watumishi wake mbalimbali waliomkubali katika makanisa mbalimbali.

YESUKRISTO ni mkweli kabisa kwa kuwa YESU amezungumza ukweli kuwa duniani kuna dhiki na kweli tunaiona dhiki.Imeandikwa “ . . . . . . . Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.”-Yohana 16:33.

Hakuna ambapo YESU anasema kuwa mbinguni  kuna dhiki ,lakini anatushauri tumchague YEYE ili tufurahie pamoja naye mbinguni tusije angamia kwa kuzifuata njia tofauti na YEYE.Imeandikwa “Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni . . . . . . . . . .”-Mathayo 5:12.

Imeandikwa “Amin, amin, nawaambia, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti milele.”- Yohana 8:51. Kuna mauti ya kwanza ambayo kila mtu itampata na baada ya hapo kuna mauti ya pili ambayo ni ya hukumu kutoka kwa MUNGU mwenyewe.Kwahiyo kwa walio mfuata YESU hiyo mauti ya pili haitawapata.

Faida zitokanazo na vita yako


Faida zitokanazo na vita yako

Mtu anapopitia vita kali au magumu katika maisha yake na akamtegemea Mungu katika muda wote wa vita yake, Kuna faida zitokanazo na vita yake hujitengeneza ndani yake.

Kuna faida nyingi sana za vita yako moja wapo ni njia ya kutangaza injili ya Bwana, fikiria pale watu wanapoona ulivyokuwa na matatizo makubwa sana na Bwana akakupigania ukashinda kabisa.

Watu wanamjua Mungu wa kweli kupitia wewe kwa kuwa wameona jinsi alivyokuokoa.

i.Bwana  anakufundisha  vita

Faida moja wapo kubwa ambayo mtu anaweza kuipata ni kufundishwa vita na Bwana.Bwana anakufundisha vita mpaka uweze kupambana na kupata ushindi.Imeandikwa “Na ahimidiwe Bwana, mwamba wangu, Anifundishaye mikono yangu vita, Vidole vyangu kupigana. ” Zaburi 144:1

Unapopitia vita Mungu anakuwa anakuandaa kwa kusudi alilokuwekea kulifanya hapa duniani.Bwana anakufundisha vita kwa namna ya rohoni, anakuongoza nakukutia nguvu kuelewa namna ya kutumia silaha za rohoni. Imeandikwa “Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili;”2 wakorintho10:3

Imeandikwa. “Ananifundisha mikono yangu vita, Mikono yangu ikaupinda upinde wa shaba.” Zaburi 18:34 .Mtu anapopitia mambo magumu,vita kubwa kwenye maisha yake naye Bwana humfundisha vita hata aweze kusimama mpaka ushindi unapotokea katika hayo ayapitiayo.

Mtu ambaye kawaida yake ni mtu wa kujikweza. Wakati wa vita na mambo magumu yatakapomfika naye Bwana atamfundisha kujishusha.Imeandikwa Bwana hufukarisha mtu, naye hutajirisha; Hushusha chini, tena huinua juu.” 1 Samweli 2:7.

Mungu hufundisha pasipo hata mtu mwenyewe kujua kuwa ni Mungu ndiye amfundishaye, kwa mfano watu wengi huanza kufunga na kuomba sana pale  vita inapokabili maisha yao.
Watu wengi hukumbuka kuutafuta uso wa Bwana pale tuu wanapopitia vita katika maisha yao.

Imeandikwa “Kulikuwa na njaa siku za Daudi muda wa miaka mitatu, mwaka kwa mwaka; naye Daudi akautafuta uso wa Bwana. . . . . . . . . .  . .” 2 Samweli 21:1

Imeandikwa  Awafunge masheki wake kama apendavyo, Na kuwafundisha wazee wake hekima.” Zaburi 105:22. Bwana hufundisha watu wake hekima ya kuvumilia, hekima ya kusema na watesi wako na hata hekima ya kupenda wale wote waliokuumiza kipindi cha vita yako.

Imeandikwa “Tazama, Mungu hutenda makuu kwa uweza wake; Ni nani afundishaye kama yeye?Ayubu 36:22.Mambo magumu yanapotokea,vita inapojiinua katika maisha yetu ujue kuna jambo ambalo Mungu anataka kutufundisha kupitia vita hiyo.

Mungu hutufundisha mambo makuu na hayo mambo makuu atufundishayo hutufanya kugeuka na kuwa watu tofauti yaani watu wenye kumuheshimu Mungu ili aweze kutenda kazi pamoja nasi.

Imeandikwa “Nami nitakufanya kuwa kama ukuta wa boma la shaba juu ya watu hawa; nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, ili nikuokoe, na kukuponya, asema Bwana.” Yeremia 15:20

Kwa hiyo faida inayotokana na vita yako ni kufundishwa na Bwana vita.Mungu  humtengenezea mtu uwezo wa kusimama vyema kwa kuwa humfundisha namna ya kushinda vita yake.“Ananifundisha mikono yangu vita; Hata mikono yangu yaupinda upinde wa shaba”2 Samweli 22:35.

ii.Mungu anatukuzwa kupitia vita 
yako

Mungu hutukuzwa kupitia vita yako.Pale ambapo ulikuwa una matatizo, ulipokuwa unakabiliwa na vita kubwa ya kusemwa vibaya katika maisha yako ndipo hapo hapo Mungu hujitwalia utukufu.
Watu wanapoona ulikuwa na vita kubwa na wakaona jinsi Mungu         alivyokushindia, hapo Mungu anatukuzwa kweli kweli.

Mungu kutukuzwa  ni moja ya faida kubwa zitokanazo na vita yako.
Mungu alijitwalia utukufu katika vita iliyokuwa ikimkabili shadraka,meshaki na Abednego.

Imeandikwa “Nebukadreza akanena, akasema, Na ahimidiwe Mungu wa Shadraka, na Meshaki, na Abednego; aliyemtuma malaika wake, akawaokoa watumishi wake waliomtumaini, wakaligeuza neno la mfalme, na kujitoa miili yao ili wasimtumikie mungu mwingine, wala kumwabudu, ila Mungu wao wenyewe.”Danieli 3:28

Bwana Mungu hupenda kutukuzwa kupitia vita yetu.Imeandikwa“Nami, tazama, nitaifanya mioyo ya Wamisri kuwa migumu, nao wataingia na kuwafuatia, nami nitajipatia utukufu kwa Farao, na kwa jeshi lake lote, kwa magari yake na kwa wapanda farasi wake.
  Na Wamisri watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, nitakapokwisha kujipatia utukufu kwa Farao, na magari yake, na farasi zake.” Kutoka 14:17-18

Mungu hujitwalia utukufu katika vita au magumu tuyapitiayo katika maisha yetu.Mungu ni Mungu wa utukufu.Imeandikwa “Ni nani Mfalme wa utukufu? Bwana mwenye nguvu, hodari, Bwana hodari wa vita”. Zaburi 24:8.Yeye Mungu hupenda kutukuzwa kupitia vita tuipitiayo katika maisha yetu.

Mungu alitukuzwa kupitia vita iliyokuwa ikimkabili Danieli pale alipookolewa na Bwana kwenye tundu la simba.Imeandikwa “Mimi naweka amri, ya kwamba katika mamlaka yote ya ufalme wangu watu watetemeke na kuogopa mbele za Mungu wa Danieli; maana yeye ndiye Mungu aliye hai, adumuye milele, na ufalme wake ni ufalme usioharibika, na mamlaka yake itadumu hata mwisho.” Danieli 6:26

iii.Kuinuliwa na Mungu katika kiwango usichotarajia

Faida nyingine ambayo hutokana na vita yako ni Mungu kukuinua kutoka pale ambapo upo kwenda kwenye kiwango cha kipekee, kiwango usichokitarajia.

Imeandikwa “Ndipo Farao akapeleka watu, akamwita Yusufu, wakamleta upesi kutoka gerezani. Akanyoa, akabadili nguo zake, na kuingia kwa Farao” mwanzo 41:14.

Vita iliyompata Yusufu ilimuachia faida ya kuinuliwa na Mungu kutoka kuwa mfungwa gerezani mpaka kuwa waziri mkuu.Imeandikwa “Farao akamwambia Yusufu, Tazama, nimekuweka juu ya nchi yote ya Misri. Farao akavua pete yake ya muhuri mkononi mwake, akaitia mkononi mwa Yusufu
; akamvika mavazi ya kitani nzuri, na kumtia mkufu wa dhahabu shingoni mwake. 

Akampandisha katika gari lake la pili alilokuwa nalo. Na watu wakapiga kelele mbele yake, Pigeni magoti. Hivyo akamweka juu ya nchi yote ya Misri.” mwanzo 41:41-43.

Faida iliyotokana na vita iliyompata Danieli ni kuinuliwa na Bwana kutoka kwenye hatari yakuuwawa na mfalme hadi kuwa mkubwa wa nchi.Imeandikwa “Basi ile amri ikatangazwa, na hao wenye hekima walikuwa karibu na kuuawa; watu wakamtafuta Danieli na wenzake ili wauawe.” Daniel 2:13.


Basi mfalme akamtukuza Danieli, akampa zawadi kubwa nyingi sana, akamfanya kuwa mkubwa juu ya uliwali wote wa Babeli, na kuwa liwali mkuu juu ya wote wenye hekima wa Babeli.” Danieli 2:48

Vita iliyowapata shadraka ,Meshaki na Abednego iliwaachia faida ya Bwana kuwainua kutoka kutaka kuuwawa mpaka kuwa wasimamizi wa wilaya.Imeandikwa“Kisha mfalme akawakuza Shadraka, na Meshaki, na Abednego, katika wilaya ya Babeli.” Danieli 3:30

Hakuna mtu yeyote aliyewahi kupitia magumu, kupitia vita huku akimtegemea Bwana katika vita yake naye Bwana alipomshindia akabakia kwenye ngazi ile ile.Kuinuliwa ni faida kubwa itokanayo na vita unayopitia.

Kwanini uoe au uolewe ?



Somo:Hatujijui kama yeye MUNGU anavyotujua!-part 1

Walengwa: couple/single

Neno:  “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, . . . .  .” Mwanzo 1:26

Theme:Sababu kuu ya kuoa au kuolewa

“Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi MUNGU atawahukumia adhabu” Waebrania 13:4

MUNGU ndiye aliyetuumba sisi sote,yaani watu wote wale wanao mjua MUNGU na wasio mjua.Imeandikwa “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini,
na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.” Mwanzo 1:26

Hivyo hatujijui kama yeye MUNGU aliotutengeneza, aliyetuumba anavyotujua!.Hatujui hata siku za maisha yetu kwa nguvu zetu bali ni kwa unabii utokao kwake MUNGU tena kwa mapenzi yake.

Imeandikwa “(Kwani sisi tu wa jana tu, wala hatujui neno, Kwa kuwa siku zetu duniani ni kivuli tu;)” Ayubu 8:9.
Yeye MUNGU anajua kila kitu juu yetu, anajua uwezo tulionao,anajua tuishi namna gani ndio itakuwa vyema zaidi,anajua kitu gani tusifanye kisije kikaharibu uumbaji wake juu yetu kwa namna yoyote ile.
MUNGU aliyetuumba anasema sii vyema mtu aishi pekee yake na akamfanyia msaidizi.
Imeandikwa“BWANA MUNGU akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.” Mwanzo 2:18
Ni nani  wakumpinga MUNGU yeye aliyetuumba  kwa kuwa yeye amesema sii vyema mtu kuishi pekee yake.
Hakuna mtu aliyejiumba ,hakuna hata mtu mmoja aliye jitengeneza.Na yule aliyetuumba anajua ni jinsi gani tunatakiwa tuwe mke na mume.

Katika maisha ya kawaida tuu,Mtu anayefinyanga (mfinyanzi) akitengeneza chungu cha udongo ,hata kile chungu kiende wapi yeye mfinyanzi akikiona tuu anakijua, tena kwa undani sana.
Atakijua na kukumbuka alitumia udongo gani ?,anajua  uwezo wa chungu hicho,kinaweza kufa ukikigonga na kitu kigumu,anajua aliweka mapambo gani ? na vyote katika chungu hicho yeye mfinyanzi anajua kwa sababu yeye ndiye aliyekifinyanga.

Je ? kama sisi wanadamu tunajua mambo yote hayo juu ya kile kitu tunacho kitengeneza,Si zaidi ajuavyo MUNGU juu yetu kwa kuwa YEYE ndio aliyotuumba.
Yeye anayetujua zaidi anatuambia si vyema mtu aishi pekee yake.Kwa hiyo kuna haja ya mtu kooa au kuolewa kwa kuwa yeye MUNGU anayetujua zaidi anatuambia kuwa sii vyema mtu kuishi pekee yake.
Hivyo BWANA asema mwanamke kuishi pasipo kuolewa sii vyema na mwanaume aishiye bila kuoa sii vyema.
Sababu ya mtu kuoa au kuolewa ni moja tuu kuwa yeye hajajiumba na aliyemuumba ambaye ni MUNGU anasema sii vyema mtu kuishi pekee yake.
“Kwa sababu hiyo ........................................................” Waefeso 5:31.
Andiko limeanza kwa kusema kwa sababu hiyo,sababu yenyewe ni “Kwasababu hatujijui sana na kiundani kama MUNGU aliyetuumba anavyotujua,na kwa agizo lake si vyema mtu aishi pekee yake..”

SIRI YA KUWA NA NGUVU KUBWA YA MUNGU

SIRI YA KUWA NA NGUVU KUBWA YA MUNGU
Imeandikwa"Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka."-Mathayo 11:12 .
MUNGU hajaishiwa nguvu za kutenda miujiza bali sisi kama wakristo hatuja amua kuchukua nafasi zetu ili kutembea na nguvu ya MUNGU.

Uhusiano mkubwa na MUNGU huleta nguvu kubwa ya MUNGU katika maisha yetu.
Watu wote kwenye biblia ambao walikuwa na nguvu kubwa ya MUNGU walikuwa na uhusiano mkubwa na MUNGU.

Imeandikwa "Mara saba kila siku nakusifu, Kwa sababu ya hukumu za haki yako."-Zaburi 119:164
Huyu ni mtumishi wa MUNGU Daudi anatueleza uhusiano wake na MUNGU ulivyo mkubwa na MUNGU wake anasema yeye kila siku anamsifu MUNGU mara saba.Hayo ni mahusiano makubwa sana na MUNGU.

Hakuna asiyejua nguvu ya MUNGU juu ya Daudi iliyo muangusha Goliath na kuwa ogopesha wafilisti, lakini kumbe siri ya Daudi kutembea na nguvu kubwa ya MUNGU ni uhusiano mkubwa aliokuwa nao na MUNGU uhusiano wa kumsifu MUNGU mara saba kila siku.
Imeandikwa". . . . . . .  akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo."-Danieli 6:10
Hapa tunaonauhusiano wa Daudi na MUNGU ulivyokuwa mkubwa,kwa kusali mara tatu si kila siku na sio kwa sababu ya matatizo lakini ndio ilikuwa kawaida yake kusali mara tatu kwa siku.

Danieli alikuwa na nguvu kubwa ya MUNGU kiasi kwamba simba wenye njaa kali hawakuweza kumla wala kumdhuru ,lakini siri yake  ya kuwa na nguvu kubwa ya MUNGU kiasi hiko ni kwa kuwa alikuwa na uhusiano mkubwa na MUNGU.Uhusiano wa kumuomba MUNGU kila siku mara  tatu na kumshukuru.

Hao ni baadhi tuu ya watumishi wa MUNGU lakini ukichunguza utakuta watumishi wote wenye nguvu za MUNGU walikuwa na uhusiano mkubwa na MUNGU.

ukisoma kwa habari ya Nabii Eliya alikuwa ni mtu wa maombi sana maombi ya bidii-Yakobo 5:17 .Ukisoma habari za YESU japo alikuwa ni MUNGU lakini alituonyesha mfano wa kuishi na kuwa na uhusiano mkubwa na MUNGU kwa kukesha mara kwa mara kwa kuomba.

Imeandikwa"Basi Petro na Yohana walikuwa wakikwea pamoja kwenda hekaluni, saa ya kusali, saa tisa."Matendo ya mitume 3:1 Hata wanafunzi wa YESU walishafundishwa namna ya kujitengenezea uhusiano mkubwa na MUNGU na ndiyo sababu walikuwa na nguvu kubwa ya MUNGU maishani mwao.

Kama kweli unataka kuwa mkristo ambaye si wakawaida basi wewe jijengee leo tabia za kuanzisha mahusiano makubwa na MUNGU ,sio jumapili kwa jumapili ndio unasali au ndio unasoma biblia . 

Jijengee tabia ya kutoenda kazini pasipo kusoma neno la MUNGU na kulitafakari, Jijengee tabia ya kufanya maombi ya maisha yako wewe binafsi kila siku kwa muda wa kutosha kila siku ,hata kama huna matatizo wewe ya kuombea wewe waombee wengine katika familia yako yenye matatizo au watu wanaokuzunguka hata ombea nchi.

Kama unasali tuu pale unapopatwa na tatizo bado hauna uhusiano mkubwa na MUNGU!,
Kama unamsifu MUNGU jumapili mpaka jumapili  bado huna uhusiano mkubwa na MUNGU.
Kama unasoma biblia jumapili kwa jumapili yaani hauna muda wa kujisomea mwenyewe biblia ,wewe bado una uhusiano mdogo na MUNGU.

MUNGU hataki umuombe siku moja tuu, hataki umsifu kwa muda kidogo tuu, hataki usome neno lake jumapili kwa jumapili tuu,
 bali anataka umuombe kila siku,umsifu kila siku na usome neno lake na kulitafakari kila siku na kwa muda wa kutosha huku ukitii maagizo yake.

Angalizo:
usishangae kuona miujiza na mambo makuu utapo anza kuwa na uhusiano mkubwa na MUNGU,usishangae kuanza kuona maono ya MUNGU wazi wazi-live, au kuombea mgonjwa na akawa huru papo hapo, hata kuwa na nguvu ya ajabu usiyotarajia pindi utapojitengenezea mahusiano makubwa na MUNGU.

Kwa neema ya MUNGU Nyimbo mpya 2015 nimeiachia rasimi:ninachofanya

Nyimbo inaitwa :Ninachofanya
Producer :Emmanuel mabelle
Imeandikwa :JASIRI
Imeimbwa na jasiri 
Year of release :2015
Sina budi kumshukuru MUNGU kuniwezesha mpaka leo nimeweza kuachia nyimbo mpya mwaka huu rasmi unaoitwa :ninachofanya.
pia ipo katikamtandao:mkito.com/artist-profile/jasiri-mbarikiwa/3022
MUNGU ni MUNGU

MAOMBI YA KUUKOMBOA WAKATI KWA HEKIMA YA MUNGU YA KUANZA NA KUMALIZA

Maombi ya kumuomba MUNGU hekima yake katika maisha yako hasa katika siku hizi za mwisho
Katika hizi siku za mwisho ,Wakristo ambao wataitikisa dunia kwa injili sii tu kwa kuwa ni wanamaombi bali pia wenye hekima ya MUNGU katika kuitenda kazi yake.Kwa kuwa hekima ni chachu ya kuukomboa wakati , Imeandikwa katika Wakolosai 4:5- Enendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati.Kitu ambacho ungekifanya (labda nikujenga ) kwa kutumia  hekima ya MUNGU kwa muda wa miaka miwili.Kitu hicho hicho kinaweza kugharimu miaka kumi na tano(15) kikifanyika pasipo hekima ya MUNGU. Mhubiri 2:13-Ndipo nilipoona ya kuwa kweli hekima hupita upumbavu, kwa kadiri nuru ipitavyo giza;

Maombi ya kumuomba MUNGU hekima yake katika maisha yako hasa katika siku hizi za mwisho.

Anza Maombi “MUNGU wewe uliye NIKO ambaye NIKO wewe uliyeniumba mimi na vyote vilivyomo duniani ninakushukuru kwa wakati huu ,nakutukuza MFALME wa wafalme nakusifu kwa ukuu wako,nakujia leo nikiomba unisamehe dhambi zangu zote nilizozifanya kwa siri na kwa uwazi uniokoe na kunifanya mpenzi WAKO BABA MUNGU.
Nakuomba unipe hekima yako MUNGU katika siku hizi za mwisho ,kama ilivyoandikwa katika Ayubu 12:13-Hekima na amri zina yeye Mungu; Yeye anayo mashauri na fahamu.
Naomba unipe hekima ya kufanya maamuzi mazuri ninapo pitia magumu ,unipe hekima ninapo ongea,uniunganishe na  watu wako wenye hekima kutoka kwako kama ilivyoandikwa katika Mithali 13:20 Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; Bali rafiki wa wapumbavu ataumia .Katika jina la YESU ninajiungamanisha na watu wenye hekima ya MUNGU katika maisha yangu.Imeandikwa  1 Wakorintho 2:5 ili imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu.Ninaikataa hekima ya dunia hii hekima ya kujivuna ninaikataa katika jina la YESU ,ile hekima ambayo inaonekana kama yatoka kwako lakini kumbe haitoki kwako ninaikataa katika jina la YESU.Imeandikwa katika Isaya 5:21-Ole wao walio wenye hekima katika macho yao wenyewe, na wenye busara katika fikira zao wenyewe!.BABA MUNGU ninakataa hekima kama hiyo itayonipelekea kuangamia bali ninajiunganisha na hekima yako kuu kutoka juu mbinguni itakayonifanya niishi vyema katika uhai siku zote za maisha yangu katika jina la YESU ,amen.Nakushukuru MUNGU kwa kunipa zaidi ya niombavyo jina lako lihimidiwe siku zote kwa hekima uliyoiweka katika maisha yangu siku hii ya leo.


Wewe si wadunia hii ,sababu kubwa ya kuchukiwa kwako !!

Theme: Wewe si wadunia hii -sababu kubwa ya kuchukiwa kwako !!
Neno:
"Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua."Mathayo 10:16

Ili kuishi kondoo katikati ya mbwa-mwitu  inahitajika kuwa na busara na upole ili kufikisha ujumbe ule tuliopewa kuufikishia dunia.

Inamaana kuwa kwa mkristo kupeleka kuishi hapa duniani anahitaji sana kuwa na hekima na busara kwa kuwa toka awali ulimwengu huu hupingana na injili ya YESUKRISTO.
 Imeandikwa "Ndugu zangu, msistaajabu, ulimwengu ukiwachukia"1 Yohana 3:13

Sababu kubwa ya kuchukiwa na watu hasa wa mataifa(watu wasiomfuta MUNGU) kama mkristo ni Kwa kuwa wewe si wa dunia hii .Hauendani nao.

Kama mkristo hautakiwi kushangaa ukiona unachukiwa ,au una bezwa kwa ajili yake YESUKRISTO.Yeye YESU alitendewa hayo huku akiwa humu duniani ,ilithibitika kuwa hana kosa lakini bado aliteswa alionewa.
  "Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na subira ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu." Ufunuo wa Yohana 1:9
Je wewe na mimi tu na nini mpaka tusiichukiwe ?

Imeandikwa "Ushiriki taabu pamoja nami, kama askari mwema wa Kristo Yesu." 2 Timotheo 2:3

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...